ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha Saba: Yesu ni Bwana na Mwokozi

ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha Saba: Yesu ni Bwana na Mwokozi

Outline: From Luke and John. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.

Script Number: 424

Language: Swahili: Tanzania

Theme: Sin and Satan (Judgement, Sin, disobedience); Christ (Resurrection of Jesus, Son of God, Saviour of Sinful Men, Birth of Christ, Death of Christ, Life of Christ, Authority); Eternal life (Salvation, Eternal / everlasting life); Character of God (Grace and Mercy, Nature, character of God, Word of God (the Bible), Power of God / Jesus); Living as a Christian (Worship, Second Birth, Peace with God, Forgiveness, Faith, trust, believe in Jesus, Spiritual Life, Christian values); Life event (Death); Bible timeline (Gospel, Good News); Problems (Sickness, Problems, troubles, worries)

Audience: General

Style: Monolog

Genre: Bible Stories & Teac

Purpose: Teaching

Status: Publishable

Script Text

Utangulizi

Utangulizi

Rafiki, Nataka kukwambia habari za Bwana Yesu, na mambo ya ajabu aliyo yafanya miaka mingi iliyo pita. Kanda hii imetolewa na Language Recordings International, Usikilize kwa makini na kuangalia picha katika kitabu ya rangi ya pinki. Unaposikia sauti hii ___________ ufungue picha inayofuata. Sasa ufungue katika picha ya kwanza kisha tutaanza.

Picha ya Kwanza: Kuzaliwa kwa Yesu

Picha ya Kwanza: Kuzaliwa kwa Yesu

Joho 1:1-14; Luka 2; Wakolosai 1:16

INjili ya Yohana Mtakatifu ninaanza na maneno haya, "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo likuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu." Katika Injili hii tunajifunza kwamba Neno alikuwa ndiye Yesu Kristo. Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu alikuwa ameposwa na Yusufu, pia Mariamu alikuwa ametokana na uzao wa Abaramu. Naye aliishi katika mji wa Nazaleti. Siku moja malaika kutoka mbinguni akamtokea. Mariamu aliongopa sana, lakini malaika akamwambia, usiogepe maana Bwana yuko pamoja nawe, nawe utapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na utamzaa mtoto jina lake utamwita Yesu. Na malaika wa Bwana alimtokea Yusufu ambaye alimposa Mariamu katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Basi Mariamu alipomzaa Yesu waka muweka katika holi ya kulia ng'ombe. Yusufu na Mariamu walikuwa masikini sana. Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote,maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini, kama malaika alivyo waambia.
**MB** Rafiki yangu, Yesu aliendelea kukua katikati ya Waisraeli. Na Biblia nasema, maisha aliyo ishi Yesu yanaonyesha dhahili kwamba yeye likuwa mwana wa Mungu. Yesu alituonyesha jinsi mtu anavyo weza kuishi kwa kumpendeza Mungu. Yesu aliwawezesha watu wote waokolewe. Bibli inasema kwamba Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe (Yohana 3:16:)

Picha Pili: Yesu Abadili Maji Yakawa Divai

Picha Pili: Yesu Abadili Maji Yakawa Divai

Yohana 2:1-11

Yesu alimpofikisha umri wa miaka thelathini alianza kusafiri katika Israeli na wafundisha watu bahari za Mungu. Yesu alifanya miujiza mingi ilikuwaonyesha watu kwama yeye ndiye aliye haidiwa na Mungu. Siku moja Yesu na wanafunzi wake walikuwapo katika harusi iliyo fanyika katika mji wa Kana. Mariamu mama yake na Yesu alikuwepo katika harushi hiyo. Hata walipokuwa wakiendelea na harusi, wakaishiwa na divai. Basi Mariamu mama yake Yesu akamwendea Yesu na kumwambia, wameishiwa na divai. Mariamu alijua kwamba Yesu anauwezo wakufanya miujiza, hivyo akawambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. Katika hiyo harusi palikuwa na mitungi sita ambayo watu walitumi kwa jaili ya kuna mikono. Yesu akawaambia, ijazeni hii mitungi maji. Nao wakayajaliza hata yaka jaa. Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai.
**MB**Rafiki yangu, Kwajinsi Yesu alivyo madili maji yawe divai, watu wengi waliamini kwamba Yesu alitoka kwa Mungu. Hanuna mtu anaye wenza kufanya hivyo. Ila Mungu tu. Yesu ni mwana wa Mungu.

Picha ya Tatu: Yesu Aongea na Nikodemo

Picha ya Tatu: Yesu Aongea na Nikodemo

Yahana 3:1-36

Palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. Huyo alimjia Yesu usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Yaani nilazima Roho wa Mungu angie ndani yako, nawe ukauwa na maisha mapya. Nikodome akashanaa sana kusikia meneno hayo. Naye akalikubali Neno la Mungu. Akawa ni mmoja wa familiya ya Mungu.
**MB**Rafiki yangu, Unapo mpokea Yesu kama mwokozi wetu, Roho wa Mungu anakuja kuishi nasi. Nahii ndiyo maana yake kuzaliwa mala ya pili. Tunakuwa watu wapya na kujiunga na familia ya Mungu. Mtu hawezi kuingia katika ufamle wa Mungu kwa kufanya matendo mema. Nilazima kumpokea Roho Mtakatifu wa ili atupe maisha mapya. Naye atatupa uzima wa milele. Uzima huo hauna mwisho utadumu milele na milele. Roho wa Mungu yupo ndani yetu na hatatuacha.

Picha ya Nne: Diwani Apiga Magoti Mbele ya Yesu

Picha ya Nne: Diwani Apiga Magoti Mbele ya Yesu

Yohana 4:46-54

Basi Ysu alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi aende na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa karibu kufa. Yule diwani akamwambia, Bwana, twende asijekufa mtoto wangu. Basi Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akaliamini lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akaenda nyumbani kwake. Hata alipokuwa akienda, watumwa wake walimlaki, wakisema mtoto wako yu hai.
**MB** Rafiki yangu, Yule mtu alifurahi sana aliporudi nyumbani na kumkuta mtoto wake hupo hai. Akawasimulia watu wa nyumbani mwake pamoja na watumishi wake vile Yesu alivyomtetendea. Na wote wakaamini kwamba Yesu alitoka kwa Mungu ili awasaidie watu wote.

Picha ya Tano: Mgonjwa Aliyekaa karibu na Kisima

Picha ya Tano: Mgonjwa Aliyekaa karibu na Kisima

Yohana 5:1-47

Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo palikuwa na kisimba. Na wagonjwa wengi walikuwa wamelala, vipofu viwete, nao waliopooza, wakingoja maji yachemke. Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika like kisima, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata. Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo. Na Wayahudi wengi walikasirika sana na walisema kwanini mameponywa siku ya sabato. Lakini Yesu aliona vema kumposha mtu aliye tesaka kwa miaka mingi na hiyo ilimpendeza Mungu.
**MB** Rafiki pendwa, Yesu anaonyesha uweza wake juu ya magonjwa. Yeye ni mwana wa Mungu. Sabato si siku ya kukaa na kupumzika tu, bali ni siku ya kuwatendea wengine mema. Yesu anataka sisi tuwatendee wengine mambo mema kila wakati.

Picha ya Sita: Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

Picha ya Sita: Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

Yohana 6:1-15, 25-58

Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tiberia. Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. Naye Yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. Na Pasaka, sikukuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu. Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula? Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu. Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao. Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote. Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula. Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. Nao wakata kumfanya awe mfalme wao.
**MB**Rafiki yangu , Yesu hakufanya hivyo ili awe mfalme. Yesu akawaambia wasifurahiye chakula cha kimwili tu ambacho ni chamuda, bali wafurahiye chakula cha Kiroho. Yesu alisema mimi ndimi chakula cha uzima. Atakaye niamini mimi hataona njaa tena, wala kiu. Tunapo soma Neno la Mungu na kuomba, na hii ni kama chakula kwatu maana tunaweza kuku Kiroho.

Picha ya Saba: Yesu Atembea Juu ya Maji

Picha ya Saba: Yesu Atembea Juu ya Maji

Yohana 6:15-21

Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake Ili kuomba. Hata ilipokuwa jioni wanafunzi wake wakatelemka baharini wakapanda chomboni, wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaumu. Nako kumekwisha kuwa giza, wala Yesu hajawafikia. Na bahari ikaanza kuchafuka kwa kuvuma upepo mkuu. Basi wakavuta makasia kama ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kukikaribia chombo; wakaogopa. Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope. Basi wakataka kumpokea chomboni; na mara hiyo chombo kikaifikilia nchi waliyokuwa wakiiendea. Wanafunzi wake walishaanga sana. Kweli hakuna mtu awezae kutembea juu ya maji.
**MB** Rafiki yangu, Wataki mwingine tunaweza kuogopa. Pia kunamambo mengine yanayo tufanya tuogope. Lakini Yesu anajua kila itu. Tunaweza kumwita yeye maana yeye yupo mahali popote.

Picha ya Nane: Yesu Amponya Mtu Kipofu

Picha ya Nane: Yesu Amponya Mtu Kipofu

Yohana 9:1-41

Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana. Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, akamwambia, Nenda kanawe katika kisima. Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. Mtu aliye kuwa kipofu tangu kuzaliwa aliponywa na Yesu. Watu wote walishanga.
**MB** Rafiki yangu, Huyu mtu alikuwa kipofu na hakuweza kuona. Sisi pia ni vipofu rohoni hatuwezi kuona nuru ya Mungu katika maisha yetu. Yesu tu ndiye anaye weza kutupa mwanga katika maisha yetu. Yesu alisema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu. Na Mtu atakaye mfuata Yesu atatembea katika nuru yake, wala si gizani tena.

Picha ya Tisa: Yesu Amwita Lazaro Kutoka Kaburini

Picha ya Tisa: Yesu Amwita Lazaro Kutoka Kaburini

Yohana 11:1-46

Mariamu na Martha walikuwa na Kaka yako mmoja aliyeitwa Lazaro. Lazaro alikuwa rafiki wa Yesu. Mariamu na Martha alijua kwamba Yesu alimpenda sana Lazaro. Siku moja Lazaro alikua anaumwe sana. Basi Mariamu na Martha wakatuma ujumbe kwa Yesu wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Yesu alimpenda Lazaro na ndugu zake lakini alipo sikia habari za ugonjwa hakwenda wakati huo huo, bali alisubiri kwa siku chache. Baada ya siku mbili Yesu akawaambia wanafunzi wake akisema, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini. Basi Yesu pamoja na wanafunzi wake pamoja na watu wengine wakaelekea kaburini. Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Mariamu na Martha walihuzunika sana, na wakasema, kama Yesu angekuja mapema ndungu yao hasinge kufa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi. Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake. Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, Yesu wakamwamini.
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu alipomfufu Lazaro alionyesha kwamba yeye anauwezo wa kushinda shetani na mauti. Ikiwa umempokea Yesu na anaishi moyoni mwako, basi usiogope kifo, kwasababu Yesu anauwezo wa kukufufua siku ya mwisho. Watu wote wamaye mwamini Yesu wataishi milele. Je, wewe una mwamini?

Picha ya Kumi: Yesu Alikufa Msalabani

Picha ya Kumi: Yesu Alikufa Msalabani

Yohana 18:1-19:42

Yesu alifanya miujiza mingi sana ilikuwaonyesha watu kwamba yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Lakini watu wengi walitaka awemfalme wao. Na viongozi wa Wayahudi hawa kupenda watu wengi wamfuate Yesu. Pia viongozi wa Wayahudi hawa kupenda Yesu awafundishe watu kwamba yeye ni mwana wa Mungu. Hivyo walitaka kumua Yesu. Kisha Yuda, aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu, alienda kwa viongozi wa Wayahudi na kuwaambia jinsi watakavyo mshika. Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari wakaenda kumkamara Yesu. Nao wakapeleka kwa Pilato ambaye alikuwa kiongozi wa Warumi. Basi Pilato akawaambia Wayahudi kwamba hakuona kosa lolote juu ya Yesu. Lakini Viongozi wa Wayahudi walikazia wakisema ni lazima Yesu afe. Mwishowe amri igatolewa kwamba Yesu afe. Askari wakamchukua Yesu na kutundika msalabani. Yesu alipigiliwa misubali na alipata meteso mengi sana. Nao askari waka mtundika Yesu msalabani katikati ya waharifu. Palikuwa nawaharifu wawili ambao walisurubiwa pamoja na Yesu, nao walikuwa wakipokea adhabu ya makosa yao.
**MB** Rafiki yangu, Yesu kafanya koso lolote. Yeye alipo kufa alibebe adhabu ya dhambi zetu na makosa yetu. Yesu alijitoa mwenyewe ili awe sadaka kwa Mungu. Na damu yake ndiyo iliyo mwagika kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu alikufa ili kila mtu atakaye mwamini awe na uzima wa milele.

Picha ya Kumi na moja: Mariamu na Yesu Kaburini

Picha ya Kumi na moja: Mariamu na Yesu Kaburini

Yohana 19:42 - 20:18

Baada ya Yesu kufa, rafiki Yesu wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika kisha waka ulaza mwili wake kaburini. Kisha askari wakaweka jiwe kubwa katika mlango wa kaburi. Yesu alikufa siku ya Ijumaa. Na baasa ya siku tatu yaani jumapili Yesu akafufu. Ilikuwa ni siku ya ajabu, malaika aliliviringisha mbali lili jiwe ililowekwa kaburini. Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. Mariamu akaanza kulia. Mala Yesu akatokea akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. Yesu akamwambia, Mariamu. Basi Mariamu alipo sikia amemwita kwa jina lake akatambua yakuwa aikuwa Yesu. Mariamu akawa mtu wa kwanza kumuna Yesu.
**MB** Rafiki yangu, Yesu alijua jina la Mariamu, Yesu anayafahamu maji na ya watu wote. Anatuita anataka tuokoke. Yesu alipokuja kushi ulimwenguni aliwaoshe watu wote kwamba yeye aliku wa Mungu. Yeye ananguvu za kushinda mauti, pia ananguvu za kushinda dhambi. Amemshinda Shetani. Hivyo basi ikiwa tuta mpokea Yesu na kumpenda na kutii Neno lake, Shetani hatakuwa na nguvu ya kutushinda sisi.

Picha ya Kumi na Mbili: Yesu Awatokea Wanafundi Wake

Picha ya Kumi na Mbili: Yesu Awatokea Wanafundi Wake

Yohana 20:30-21:19

Baada ya Yesu kukufuka, baadhi ya wanafunzi wake walirudi kuvua samaki. Na hivi ndivyo ilivyo kuwa: Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu. Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama kandokando ya maji walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu. Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, La. Akawaambia, Itupe nyavu upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Basi wakatupa; wala sasa hawakuweza kuivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki. Basi Yohana akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Naye Simoni Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake, akajitupa baharini. Na hao wanafunzi wengine wakaja katika mashua; maana hawakuwa mbali na nchi kavu. Wanafunzi walikuwa na furaha sana kuwa pamoja na Yesu tena. Kabla ya Yesu kuteswa alimwambia Petro kwamba atamkana. Na sasa Yesu alitaka kumuonyesha Petro kwamba alikuwa amemsamehe. Yesu akamwambia Petro achunge kundundi la Mungu na kuwafundisha.
**MB** Rafiki yangu, Yesu anatujua sisi sote. Yesu anajua makosa yetu. Lakini yupo tayari kutusamehe. Tunajua kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Maana ni Mungu tu ndiye anaye weza kufanya miuji kama aliyo ifanya Yesu. Yesu anakuita leo umfuate.

UTANGULIZI: Picha ya Kumi na tatu hadi Ishirini na nne: Yesu ni Mwokozi

UTANGULIZI: Picha ya Kumi na tatu hadi Ishirini na nne: Yesu ni Mwokozi

Luka

Mungu aliwap ahadi Wayahudi, kwamba atamtuma Mwokozi. Na kwa miaka mingi Wayahudi walikuwa wakimsubiri Mwokozi aliye ahidiwa. Wayahudi walifikiri kuwa mtu atakaye kuja kuwakombo atakuwa kama mfalme Daudi mbaye aliwasaidia Waisraeli na kuwatoka katika utawala wa Kifilisti. Mungu alimtuma Yesu kuwaokoa Waisraeli na watu wote. Lakini Yesu alikuwa mtu wa tofauti sana, hakuwa kama viongozi wengine. Na habari tutakazo jifunza katika kitabu cha Luka zitatusaidia kuelewa zaidi juu ya Yesu Mwokozi wetu.

Picha ya Kumi na tatu: Yesu Awafundisha Marafiki Wawili

Picha ya Kumi na tatu: Yesu Awafundisha Marafiki Wawili

Luka 24:13-35

Baada ya Yesu kufufuka katika wafu alimtokea Mariamu. Naye aliwaambia wanafunzi wake kwamba amemuona Yesu, lakini hawakuamini. Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote, tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo, tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, aliokwenda kaburini asubuhi na mapema, wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Basi walipokuwa wakiendelea kutembea, wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao. Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? Wakaondoka saa ile ile, wakarejea Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja wamekutanika, wao na wale waliokuwa pamoja nao, wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli.

Picha ya Kumi na nne: Kijana Aliye Ishi na Nguruwe

Picha ya Kumi na nne: Kijana Aliye Ishi na Nguruwe

Luka 15:11-19

Siku moja Yesu akafundisha wanafunzi wake akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya ulithi wangu. Basi hule baba akampa yule mdogo sehemu ya ulithi wake. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati. Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako, sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi. Basi yule kijana akaamua kurudi nyumbani kwa baba yeke.

Picha ya Kumi na tano: Mwana Mpotevu Arudi Nyumbani

Picha ya Kumi na tano: Mwana Mpotevu Arudi Nyumbani

Luka 15:20-32

Basi yule kijana akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi, kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu aliwafundisha hadithi hii na alitake waelewe kwamba Mungu ndivyo alivyo. Mungu nikama yule baba. Sisi tumemuasi Mungu na kwenda mbali naye na kufanya dhambi. Lakini Mungu anatusubiri turudi kwake na kutubu dhambi zetu. Tunapo muomba Mungu atusamehe dhambi zetu, Yeye anatusamehe, tena anafurahi sana.

Picha ya Kumi na sita: Utajiri wa Mtu Tajiri

Picha ya Kumi na sita: Utajiri wa Mtu Tajiri

Luka 12:13-31

Yesu aliwaambia watu kwamba ni muhimu kuandaa maisha yao baada ya kufa. Naye akawaahidithia hadithi hii: Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana, akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Mtu huyu halijua kuwa akiwa tajijili basi yeye hamhitaji Mungu. Yule tajili alitaka kujiwekea mali nyingi hapa duniani, lakini alisaha kujiwekea hazina yake baada ya kufa, yaani pale mbinguni. Hutaji wake wa hapa duniani haukuweza kumzuia hasife. Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini. Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo."
**MB** Rafiki yangu, Tunajua kwamba Mungu ndiye aliye na vitu vyote, anao utajiri, hekima na anavitu vyote. Tumwamini yeye naye anaweza kutupa maitaji yetu. Tukionyesha upendo kwa watu wengine na kuwasadia watu walio masikini, tunawabariki wao. Tunaweza tusiwe matajili katika dunia hii, lakini Yesu alisema tutakuwa na utjali mkubwa pale mbinguni.

Picha ya Kumi na saba: Mwombaji na Tajiri

Picha ya Kumi na saba: Mwombaji na Tajiri

Luka 16:19-31

Tena Yesu akawaambaia habari za mtu tajiri na mtu aliye kuwa masikini, jina lake aliitwa Lazaro. Basi Yesu akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa., wala hakujali maneno ya Mungu. Na Lazaro, ukaa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Na Lazaro alikuwa akitafuta kumpenda Mungu. Ikawa siku moja yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, kuna watumishi Mungu wanoa lihubiri Neno lake na wawasikilize wao.
**MB** Rafiki mpendwa, Haimaanishi kwamba mtu akiwa tajiri basi Mungu anapenzwa naye. Hajarishi mtu akiwa tajiri au masikini, jambo la muhimu ni kumpendwa Mungu na kuwaonyesha wengine upendo wa Mungu. Kama mtu atakufa bila ya kumwamini Yesu, basi atakuwa amechelewa. Wakati wetu ndio SASA wa kuanza kumfikiria Mungu na kumpendeza.

Picha ya Kumi na nane: Rafiki Aliye Mlangoni

Picha ya Kumi na nane: Rafiki Aliye Mlangoni

Luka 11:5-13

Yesu aliwafundisha wanafunzi wake yakwamba nimuhimu kumuomba Mungu kwa ajili ya maitaji yao. Yesu akawafundisha akisema, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu nimepata naye amefika kwangu, ametoka safarini, nami sina kitu wala chakula. Na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? Nawaambia ya kwamba, atatoka amme yule aliye muomba si kwasababu ni rafiki tu, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba. Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona, bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au mwanawe akimuomba samaki, atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Basi Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao.
**MB** Rafiki yangu, Habari hii inatusaidia tuelewe umuhimu wa kuomba. Mungu ujibu maombi. Wakati mweingine inatupasa kuombea jambo furahi bila kukoma. Na wakati mwingine inachukua muda kupata majibu. Wakati wowote na siku yoyote Mungu anasikia maombi yetu.

Picha ya Kumi na tisa: Watu Wawili Katika Nyumba Ya Mungu

Picha ya Kumi na tisa: Watu Wawili Katika Nyumba Ya Mungu

Luka 18:9-14

Yesu aliwafundishwa wanafunzi kwake kwamba, tunapokuwa tukiomba Mungu huangalia moyo wa mtu. Naye akawaambia mfano huu wa watu waliojidai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Yesu akaanza kufundisha na kusema watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
**MB**Rafiki, Yesu alisema, mtoza ushuru alitoka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule mwingine, kwa maana kila ajikwezaye atashushwa. Kwahivyo sisi tunapo omba tukumbuke kwamba Mungu anaangalia moyo. Tukijikweza Mungu hatasikiliza maombi yetu. Lakini tukijinyenyeke na kuwaona wengine kuwa ni bora, Mungu atasikia maombi yetu.

Picha ya Ishirini: Mpanzi Aliye Panda Mbegu

Picha ya Ishirini: Mpanzi Aliye Panda Mbegu

Luka 8:4-8

Yesu alitaka watu wote waelewe Neno la Mungu na walitii. Lakini watu wengine hawakutii Neno lake, ndipo akawapa mfano huu akisema, Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba. Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia.
**MB**Rafiki mpendwa, Wanafunzi wa Yesu walisikiliza kwa makini sana mfano huu. Wakamuomba Yesu awafafanulie mfano huo. Je, wewe unaweza kuelewa mfano huu? Ufungue katika picha inayofuata na usikilize kwa makini.

Picha ya Ishirini na mmoja: Mbegu Zikakua

Picha ya Ishirini na mmoja: Mbegu Zikakua

Luka 8:9-15

Yesu alipokuwa ameketi na wanafunzi wake, alianza kuwafafanulia juu ya mfano wa mpanzi. Na mara kwa mara Yesu alitoa hadithi iliyo kuwa na maana Kiroho. Yesu akawafafanulia wanafunza wake akisema, Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu. Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka. Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote. Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.
**MB**Rafiki yangu, Ebu ufikirie kwamani mfano huu wa mpanzi. Je, wewe umelipokea Neno la Mungu? je, maisha yako na mienendo yako inampendeza Mungu na kuwasaidia watu wengine waokoke? Yesu anataka sisi tumpende Mungu na kulishika Neno lake, na jambo hilo ni lamaana sana katika maisha yetu.

Picha ya Ishirini na mbili: Kumsaidia Mtu Aliye Jeruhiwa

Picha ya Ishirini na mbili: Kumsaidia Mtu Aliye Jeruhiwa

Luka 10:25-37

Siku moja Yesu alikuwa akiwafundisha watu katika mkutano na mwana-sheria mmoja alisimama ili amjaribu Yesu, akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi; wakamvua nguo, wakampika, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando. Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo, na alipomwona alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na dawa, akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. Basi Yesu akamuuliza yule mwana-sheria waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang'anyi? Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu alitaka kumuonyesha yule mwana-sheri kwamba ni muhimu sana kumpenda Mungu na pia ni muhimu kwasaidia watu wengine. Na kwanjia hii tuna weza kumpendeza Mungu zaidi.

Picha Ishiri na tatu: Bwana Mwenye Nyumba Anaporudi

Picha Ishiri na tatu: Bwana Mwenye Nyumba Anaporudi

Luka 12:35-48

Katika picha hii unawaona watumishi wa mtu tajiri. Na mwanaume aliyesimama katika mlango ndiyo bwana wa wa watumwa hao. Amerudi kutoka katika safari ya mbali. Naye amefurahi kuwakuta watumishi wake wamefanya kazi kubwa ingwa yeye mwenyewe hakuwapo. Katika Biblia kuna mafundisho ya watumishi ambao waliwa waaminifu. Yesu alisema, bwana wa watumwa hao aliporudi kutoka katika safari yake aliwakuta wakifanya kazi, na bwana wao aliwapa tuzo wale waliofanya kazi wa uaminifu. Pia bwana wao aliwafukuza wali watummwa wasio waaminifu.
**MB** Rafiki mpendwa, Watu wanaompenda Bwana Yesu hao ndiyio watumishi wake. Yesu anataka sisi tufanye kazi yake kama tunamfanyia yeye. Tutakuwa si waaminifu ikiwa hatuta fanya kazi yake kwa uaminifu. Kazi ambayo Yesu anataka sisi tufanya ni kuwaambia wengine habari njema. Yesu ameahidi kwamba hatakuwa pamoja nasi. Yesu amekwenda kutuandalia makao mbingu.

Picha ya Ishirini na nne: Mtu Juu Ya Mti

Picha ya Ishirini na nne: Mtu Juu Ya Mti

Luka 19:1-10

Naye Yesu alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na katika mji huo, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, ya mkutano waliomfua Yesu, akapanda juu ya mti wa mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu ya mti, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa dhuruma namrudishia mara nne. Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, Kwa kuwa Nemakuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.
**MB** Rafiki yangu unaye nisikiliza, Yesu ni Mwokozi wa ajabu. Anawapenda watu wote, hata watu wenye dhambi Yesu anawapenda. Yesu anauwezo wa kubadilisha maisha ya watu, kama alivyo fanya kwa Zakayo. Zakayo alikuwa mtu aliyefanya mambo mambaya hata watu hawakumpenda, lakini Yesu alimbadilisha, naye Zakayo akaanza kupendeza Mungu. Njoo kwa Yesu leo.

Related information

Free downloads - Here you can find all the main GRN message scripts in several languages, plus pictures and other related materials, available for download.

"Look, Listen and Live" audio-visual - A set of 8 programs of 24 pictures each for evangelism and Christian teaching. The series presents Old Testament characters, the life of Jesus, and the young church.

How to use GRN Audio visual resources - 1: Sharing the Gospel made easy - This article gives an introduction to some of the many different ways the GRN audio visual resources can be used in ministry.

How to use GRN Audio visual resources - 2: Going Deeper - This article gives further explanation of how people learn from the stories, and why the stories do not have a lot of commentary.

The GRN Audio Library - Evangelistic and basic Bible teaching material appropriate to the people's need and culture in a variety of styles and formats.

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares it's audio, video and written scripts under Creative Commons

Creating DVDs using the GRN Slide show Videos - How to burn DVDs for specific people groups you are trying to reach