unfoldingWord 11 - Pasaka
개요: Exodus 11:1-12:32
스크립트 번호: 1211
언어: Swahili
청중: General
장르: Bible Stories & Teac
목적: Evangelism; Teaching
성경 인용: Paraphrase
지위: Approved
이 스크립트는 다른 언어로 번역 및 녹음을위한 기본 지침입니다. 그것은 그것이 사용되는 각 영역에 맞게 다른 문화와 언어로 조정되어야 합니다. 사용되는 몇 가지 용어와 개념은 다른 문화에서는 다듬어지거나 생략해야 할 수도 있습니다.
스크립트 텍스트
Mungu alimuonya Farao ikiwa hatawaruhusu Waisraeli kuondoka, ya kuwa atawaua wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa watu wa Misri na wa wanyama. Baada ya kusikia hayo Farao aliendelea kutomwamini wala kumtii Mungu.
Mungu alifanya njia ya kuwaokoa wazaliwa wa kwanza wa kiume kwa yeyote atakayemwamini Yeye. Kila nyumba ya Israeli ilipaswa kuchagua mwanakondoo aliye mkamilifu na kumchinja.
Mungu aliwaelekeza Waisraeli kupaka damu ya Mwanakondoo kwenye milango yao, kuichoma nyama ya Mwanakondoo na kuila kwa haraka pamoja na mikate isiyowekewa amira. Vile vile Mungu aliwaambia mara baada ya kula wawe tayari kuondoka Misri.
Waisraeli walitimiza yote waliyoagizwa na Mungu. Usiku wa manane Mungu alipita juu ya Wamisri wote na kuwaua wazaliwa wao wote wa kwanza wa kiume.
Nyumba zote za Waisraeli zilipakwa damu katika milango yake, hivyo Mungu alipita juu ya nyumba zao. Katika nyumba hizo wote waliokolewa. Walipona kwa sababu ya damu ya Mwanakondoo.
Wamisri hawakuamini wala kutii maelekezo ya Mungu. Hivyo basi Mungu hakupita juu ya nyumba zao. Akawauwa wazaliwa wao wa kwanza wa kiume.
Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Wamisri alikufa, tangu mzaliwa wa kwanza wa aliyekuwa gerezani mpaka mzaliwa wa kiume wa kwanza wa Farao. Wengi walilia na kuomboleza kwa ajili ya huzuni kubwa iliyowapata.
Usiku ule ule, Farao aliwaita Musa na Haruni na kuwaambia, "wachukueni Waisraeli muondoke haraka." Hata Wamisri pia waliwasihi Waisraeli watoke haraka.