unfoldingWord 09 - Mungu Anamwita Musa

unfoldingWord 09 - Mungu Anamwita Musa

概要: Exodus 1-4

文本编号: 1209

语言: Swahili

听众: General

类型/流派: Bible Stories & Teac

目的: Evangelism; Teaching

圣经摘录: Paraphrase

状态: Approved

脚本是翻译和录制成其他语言的基本指南,它们需要根据实际需要而进行调整以适合不同的文化和语言。某些使用术语和概念可能需要有更多的解释,甚至要完全更换或省略。

文本正文

Yusufu alipofariki, ndugu zake walidumu kuishi huko Misri. Wao pamoja na wazazi wao, kwa miaka mingi waliongezeka na walikuwa na watoto wengi. Kabila hilo waliitwa Waisraeli

Mamia ya miaka mingi ilipita, wakazidi kuongezeka. Wamisri walimsahau Yusufu na kazi nzuri alizozifanya kwa Wamisri. Wamisri waliwaogopa Waisraeli kwa kuwa walikuwa wengi na Farao wa kipindi hicho aliwafanya kuwa watumwa kwa Wamisri.

Waisraeli walitumikishwa na Wamisri kwa kazi ngumu kwa kujenga majumba na miji mikubwa. Ugumu wa kazi ulisababisha huzuni kimaisha. Bali baraka za Mungu ziliwazidishia watoto kwa wingi.

Farao aliona kuwa Waisraeli walikuwa wanazaa watoto wengi, aliamuru watoto wa kiume wauawe kwa kutupwa katika mto Naili.

Mtoto wa kiume alizaliwa na mama mmoja wa Kiisraeli. Wazazi wa mtoto huyo walimficha kwa muda walioweza.

Mtoto huyo alipokuwa hawezi kufichika tena, ili kumuokoa wazazi walimweka katika kikapu kieleacho na kukiweka katika majani kando ya mto Naili. Ili kujua kuwa ni jambo gani lingempata mtoto huko mtoni dada yake alikuwa akifanya uchunguzi.

Mtoto wa kike wa Farao aliona kikapu na alichungulia ndani yake. Alipoona mtoto, alimchukua awe wake na kumwajiri mwanamke wa Kiyahudi amtunze. Bila kutambua, mama huyo mlezi ndiye alikuwa mzazi wa mtoto huyo. Mtoto alipoacha kunyonya alikabidhiwa kwa binti Farao naye akamwita jina lake Musa.

Akiwa mtu mzima, siku moja Musa alimkuta Mmisri akimpiga mtumwa wa Kiisraeli. Na alijitahidi kumuokoa Mwisraeli mwenzake.

Musa alimuua Mmisri na kuuzika mwili wake akidhani kwamba hakuna mtu ambaye angemwona. Kumbe mtu mmoja alimwona akifanya kitendo hicho.

Habari za mauaji zilipomfikia Farao, aliazimia kumuua Musa. Musa alitoroka kutoka Misri na kukimbilia nyikani ili kujiokoa na walinzi wa Farao.

Musa alikuwa mchungaji wa kondoo huko nyikani mbali na nchi ya Misri. Alioa huko na kuzaa watoto wawili wa kiume.

Siku moja Musa alikuwa akichunga kondoo wake, aliona kichaka kilichowaka moto bila kuteketea. Musa alisogea kuona vizuri, alipokaribia, Mungu alisikika akisema, "Musa vua viatu vyako. Ardhi uliyosimama juu yake ni takatifu".

Mungu alimwambia Musa," Nimeyaona mateso ya watu wangu. Ili kuwakomboa kutoka utumwani huko Misri, nitakutuma wewe kwa Farao ukawaondoe Waisraeli kutoka utumwani Misri. Nami nitawapa nchi ya Kanaani, niliyowaahidia Ibrahimu, Isaka na Yakobo."

Musa akauliza, watakapotaka kujua Ni nani aliyenituma kwao nisemeje? Mungu akasema, "MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Waambie AMBAE NIKO amenituma. Mimi ni YEHOVA Mungu wa baba zenu Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Jina langu ndilo hilo milele."

Musa hakutaka kwenda kwa Farao kwani aliogopa, kwa sababu alihofia kutoweza kuongea vizuri. Mungu alimruhusu Haruni nduguye amsaidie. Aliwaonya kuwa Farao atakuwa na moyo mgumu.

相关信息

人生箴言 - GRN提供几千种语言的福音音频信息,包含圣经信息,救赎和基督徒生活。

免费下载 - 免费下载传福音及发展教会所用的录音、图片、文本和其他相关资料。内容包括福音与圣经故事,并已被翻译成上千种语言。

环球录音网音频图书馆 - Mp3,CD和磁带格式的福音材料和圣经教学材料,满足人们不同文化的需求。录音材料的形式多样,包括简单的圣经故事,福音信息,经文朗诵和歌曲。

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares it's audio, video and written scripts under Creative Commons