unfoldingWord 25 - Shetani Anamjaribu Yesu
概要: Matthew 4:1-11; Mark 1:12-13; Luke 4:1-13
文本編號: 1225
語言: Swahili
聽眾: General
目的: Evangelism; Teaching
Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture
狀態: Approved
腳本是翻譯和錄製成其他語言的基本指南,它們需要根據實際需要而進行調整以適合不同的文化和語言。某些使用術語和概念可能需要有更多的解釋,甚至要完全更換或省略。
文本文字
Mara tu Yesu alipokwisha kubatizwa, Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu nyikani, huko alifunga siku arobaini mchana na usiku. kisha Shetani alifika kumjaribu Yesu ili atende dhambi.
Shetani alimjaribu Yesu akisema; "Kama wewe ni mwana wa Mungu yaamuru mawe haya yawe mikate upate kula".
Yesu akajibu; "Imeandikwa katika neno la Mungu, watu hawahitaji mkate pekee ili wapate kuishi, bali wanahitaji kila neno linalosemwa na Mungu".
Kisha Shetani alimchukua Yesu mpaka juu ya mnara wa hekalu na kumwambia; "Kama wewe ni Mwana wa Mungu jirushe mwenyewe chini, kwa vile imeandikwa, Mungu atakuagizia malaika wake wakuchukue ili usijigonge mguu wako katika jiwe".
Lakini Yesu alimjibu Shetani kwa kunukuu Maandiko akisema; " Katika neno la Mungu, anaagiza watu wake, usimjaribu Bwana Mungu wako".
Kisha Shetani alimwonyesha Yesu falme zote za ulimwengu na fahari zake zote na akasema; "Nitakupa hivi vyote iwapo utanisujudia na kuniabudu mimi".
Yesu akajibu; ondoka kwangu Shetani! Katika neno la Mungu ameagiza, "Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia Yeye peke yake".
Yesu hakujitia chini ya majaribu ya Shetani, hivyo Shetani aliondoka akamwacha. kisha malaika walikuja na kumhudumia Yesu.