unfoldingWord 32 - Yesu Amponya Mwanamume Aliyepagawa - pepo na Mwanamke Mgojwa

unfoldingWord 32 - Yesu Amponya Mwanamume Aliyepagawa - pepo na Mwanamke Mgojwa

概要: Matthew 8:28-34; 9:20-22; Mark 5; Luke 8:26-48

文本编号: 1232

语言: Swahili

听众: General

类型/流派: Bible Stories & Teac

目的: Evangelism; Teaching

圣经摘录: Paraphrase

状态: Approved

脚本是翻译和录制成其他语言的基本指南,它们需要根据实际需要而进行调整以适合不同的文化和语言。某些使用术语和概念可能需要有更多的解释,甚至要完全更换或省略。

文本正文

Siku moja Yesu na wanafunzi wake walipanda mashua kuelekea mjini, ambako waliishi watu wa Gerasini.

Na walipofika upande wa pili wa ziwa, na alikuwako mtu mwenye mapepo alimkimbilia Yesu.

Mtu huyu alikuwa mwenye nguvu na hapukuwa na mtu yeyote wa kumdhibiti. watu walimfunga kamba mikonom na miguuni mwake lakini bado aliweza kuzikata.

Mtu huyo aliishi maeneo ya makaburi na mtu huyu alitetemeka mchana na usiku kwa sababu hakuvaa nguo zozote na mwili wake alijikata kwa mawe.

Mtu huyo alipokuja kwa Yesu, alianguka mbele ya magoti yake. Na Yesu akaliaamuru lile pepo "limtoke mtu huyo".

Mtu huyo mwenye pepo akalia kwa sauti " unataka nini kwangu Yesu, mwana wa Mungu aliyetukuzwa juu? tafadhali usinitese" ndipo Yesu akaliuliza lile pepo " je unaitwa nani"? akajibu " jina langu ni legioni" na kwa sababu tupo wengi ( " legioni" kikundi cha wanajeshi maelfu katika vikosi vya rumi).

Yale mapepo yakamwomba Yesu " tafadhali usituondoe katika mji huu", na hapo palikuwa na kundi la nguruwe karibu na kilima, yale mapepo yakamwomba Yesu " tuamuru twende kwenye nguruwe hao" na Yesu akajibu "nendeni".

Yale mapepo yakamtoka yule mtu na kuwaingia wale nguruwe, Na wale nguruwe wakakimbilia huko chini bondeni kwenye ziwa........ na palikuwako na nguruwe 2000 kundini.

Na watu wale waliokuwa wakiwaangalia wale nguruwe walipoona hayo yakitokea, walikimbia na kuelekea mjini na huko wakamwambia kila mmoja yakuwa wamemkuta Yesu na aliyokuwa akitenda. Na watu wa mjini wakaenda na kumwona yule mtu aliekuwa na mapepo. Alikuwa amekaa kwa utulivu,amevaa nguo na alikuwa anaonekana kama mtu wa kawaida.

Watu waliogopa na wakamuomba Yesu aondoke, ndipo Yesu akapanda ndani ya mashua na akijiandaa kwa ajili ya kuondoka. na mtu yule aliekuwa na mapepo akamusihi Yesu aondoke pamoja naye.

Yesu akajibu " hapana, ondoka uende nyumbani na uwaeleze marafiki na familia yako kuhusu yote alivyokutendea Mungu na alivyokufanyia huruma yake kwako.

Ndipo mtu yule akaondoka na kumweleza kila mtu yale yote Yesu aliyomtendea. Na kila mtu aliye sikia simulizi hizi alishangaa na kusitaajabishwa.

Ndipo Yesu akarudi upande mwingine wa ziwa, na lipofika lilikuwako kundi kubwa la watu waliokusanyika wakimzunguka. na hapo alikuwapo mwanamke aliegua na kutokwa damu miaka kumi na miwili. Alilipa pesa yake yote kwa waganga ili wamponye lakini hali ilizidi kuwa ngumu.

Alisikia ya kuwa Yesu aliponya watu wengi na akafikiri" hakika kama nitagusa vazi la Yesu na mimi nitapona pia". hivyo akaja karibu na Yesu akamgusa vazi lake. na baada ya kumgusa tu, alipona na hakutokwa damu kwake kukaisha.

Na ndipo Yesu akagundua yakuwa nguvu zimemuishia, hivyo akageuka nyuma na kuuliza " je ni nani aliye nigusa", wanafunzi wakamjibu " kuna kundi kubwa la watu limekuzunguka na wakikugusa je ni kwa nini umeuliza "ni nani aliyenigusa"

Kisha yule mwanamke akaanguka magotini pa Yesu akitetemeka na kuogopa, akamwambia yale yote aliyo yatenda na alivyopokea uponyaji. Yesu akamwambia " enenda kwa amani, imani yako imekuponya.

相关信息

人生箴言 - GRN提供几千种语言的福音音频信息,包含圣经信息,救赎和基督徒生活。

免费下载 - 免费下载传福音及发展教会所用的录音、图片、文本和其他相关资料。内容包括福音与圣经故事,并已被翻译成上千种语言。

环球录音网音频图书馆 - Mp3,CD和磁带格式的福音材料和圣经教学材料,满足人们不同文化的需求。录音材料的形式多样,包括简单的圣经故事,福音信息,经文朗诵和歌曲。

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares it's audio, video and written scripts under Creative Commons