ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha tano: Katika Safari ya Mungu

ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha tano: Katika Safari ya Mungu

Balangkas: Elisha, Daniel, Jonah, Nehemiah, Esther. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.

Bilang ng Talata: 422

Wika: Swahili: Tanzania

Tema: Sin and Satan (Deliverance, Sin, disobedience); Christ (Life of Christ, Authority); Character of God (Word of God (the Bible)); Living as a Christian (Worship, Obedience, No other gods, idols, Victory, Faith, trust, believe in Jesus); Bible timeline (Gospel, Good News, People of God); Problems (Problems, troubles, worries)

Tagapakinig: General

Layunin: Teaching

Features: Monolog; Bible Stories; Extensive Scripture

Katayuan: Approved

Ang mga script ay panimulang gabay para sa pagsasalin at pagre-record sa ibat-ibang wika.Ang mga ito ay ay dapat na angkupin kung kinakailangan para maunawaan at makabuluhan sa bawat kultura at wika. Ilang termino at konsepto na ginamit ay maaaring gamitin para maipaliwanag o maaari di na palitan o tanggalin ng ganap.

Salita ng Talata

Utangulizi

Utangulizi

Habari zilizopo katika kitabu cha kijani cha picha zimetoka katika kitabu cha Mungu, Beblia. Pia habari hizo zina tuambia juu ya watu wa Mungu, ambao walipata msaada kutoka kwa Mungu walipokuwa na matatizo. Sasa chukua kitabu chako na ufungue katika picha ya kwanza . Unaposikia sauti hii ___________ ufungue picha inayofuata.

Picha ya Kwanza: Naamani Atembelea nyumbani kwa Elisha

Picha ya Kwanza: Naamani Atembelea nyumbani kwa Elisha

2 Wafalme 5:1-12

Kulikuwa na nchi iliyo kuwa karibu na Israeli aliyoitwa Shamu. Washamu walikuwa maadui wa Waisrae na mara kwa mara Washamu na Waisraeli walikuwa na vita. Na palikuwa na viongozi mkuu wa majeshi aliyeitwa Naamani. Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu Mkubwa, na mwenye kuheshimiwa, tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. Katika nyumba ya Naamani alikuwapo mwanamke aliye fanya kazi ya utumishi katika nyumba hiyo, naye alikuwa ametoka katika nchi ya Israeli, naye akawambia juu ya mtumishi wa Mungu aliyeitwa Elisha. Naye akasema, ikiwa Naamani ataenda kwa Elisha mtumishi wa Mungu, ataweza kupona ugonjwa wake. Naamani hakumjua Mungu. Alikini aliposikia habari za Elisha aliamua kwenda kumuona. Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha. Naye Elisha akutoka nje ili aongee na Naamani, lakini alimtuma mjumbe, kwa Naamani akisema, "Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi." Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka nje, na kusimama, na kuomba kwa jina la BWANA, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma. "Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi?" Akageuka, akaondoka kwa hasira kwasababu maji ya Yordani yalikuwa si masafi sana.
**MB** Rafiki mpendwa, Elisha akufanya hayo kwa nia mbaya. Ila alitaka Naamani atambue kwama Mungu peke yake ndiye anaye weza kumponya-si Elisha. Naamini alitakiwa kuweka imani kwa Mungu tu lakini yeye hakuwelewa.

Picha ya Pili: Naamani katika mto

Picha ya Pili: Naamani katika mto

2 Wafalme 5:13-19

Naamani alikasirika sana alipo ambiwa akajioshe katika mto Yordani. Lakini watumishi wake wakamsihi wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si nirahisi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi? Ndipo Naamani akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. Naamani akamrudia Elisha mtu wa Mungu, yeye na watu wote walimfuata. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli. Basi Naamani akaenda zake kwa furaha.
**MB** Rafiki mpendwa, Habari hii inatufundisha kwamba Mungu anapendwa watu wote. Naamani alikuwa adui wa Israeli, lakini Elisha hakukataa kumsaidia. Bila shaka Naamani alijifunza siku hiyo kwamba, ukitaka Mungu akusaidia yakupasa umtegemee yeye tu. Pia habari hii inatufundisha sisi umuhimu wa kuwaambia watu wengine habari za Mungu. Yule mwanamke aliyetoka katika nchi ya Israeli akuogopa kuwaambia wengine habari za Mungu, ingawa alikuwa katika nchi ya ugenini. Yesu anataka sisi tuwaambie watu wengine kuhusu Yeye. Pia anataka watu waje kwake na wamsifu Yeye kama alivyo fanya Naamani.

Picha ya Tatu: Elisha na Jeshi la Mungu

Picha ya Tatu: Elisha na Jeshi la Mungu

2 Wafalme 6:8-17

Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli akafanya mashauri na watumishi wake. Kisha mfalme wa Shamu akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ambao Elisha alikuwa akikaa, wakauzingila huo mji pande zote ili wamkamate Elisha. Lakini Elisha alijua. Hata asubuhi na mapema mtumishi Elisha alipotoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? Lakini Elisha akamjibu, usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wao. Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote. Na hao walikuwa ni Jeshi la Mungu ambalo lilikuja kumsaidia Elisha.
**MB** Rafiki mpendwa, Elisha hakuogopa. Alijua kwamba Mungu anampenda na atamlinda. Pia alijua nguvu za Mungu ni kubwa kulizo miungu wengine. Hata leo nguvu za Mungu zina uweza mkuu. Mungu anatulinda sisi kama alivyo mlinda Elisha

Picha ya Nne: Elisha na Askari walio pofuswa

Picha ya Nne: Elisha na Askari walio pofuswa

2 Wafalme 6:18:23

Na Washamu alipo karibia kumkama Elisha. Elisha liomba kwa Mungu akisema, Uwapige, watu hawa kwa upofu. Bwana akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha. Kisha Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria. Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, BWANA wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. BWANA akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria. Na mfalme wa Israeli alikuwa mbele yao. Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige? Elisha akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.

**MB** Rafiki mpendwa, Wale watu walikuwa wana mtafufa Elisha lakini Elisha aliwashinda kwa uweza wa Mungu. Watu wali walijishangaa kujikuta mbele ya mfalme wa Israeli. Na walitambua kwamba Mungu wa Elisha likuwa na nguvu. Sisi wenyewe tukimtemea Mungu kama alivyo fanya Elisha, Mungu anaweza kutu saidia kufanya matendo makuu ya ajabu. Na watu wengi watataka kumjua Mungu wetu.

Picha ya Tano: Kuzingilwa kwa mji wa Samaria

Picha ya Tano: Kuzingilwa kwa mji wa Samaria

2 Wafalme 6:24 - 7:2

Ikawa baada ya hayo, mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akaenda apigane na Israeli. Na wakati huo njaa ikawa kuu huko Samaria mji ulioko Israeli. Ikawa mfalme wa Israeli alipokuwa akipita ukutani, mwanamke mmoja akamwita akisema, Unisaidie, bwana wangu, mfalme. Na mwanamke huyo alimuomba mfalme msaada kwasababu njaa ilikuwa kali kiasi kwamba watu walianza kula hata watoto wao. Na mfalme alikasirika sana juu ya jambo hilo. Mfalme akasema kwanini Elisha ajamuomba Mungu ili atupe chakula. Basi mfalme akatuma watu wamuwe Elisha. Lakini wale watu waliotumwa kwa Elisha walipofika kwa Elisha. Elisha akawaambia, Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho Wakati kama huui, vyakula vita chuka bei na kutakuwa na kila aina ya chakula.
**MB**Rafiki yangu, Elisha alijua kwamba wakati huu ulikuwa mgumu sana kwa watu wa Israeli. Lakini pamoja na hayo alijua Mungu anatawala vyote na anauwezo umkuu. Elisha alikuwa tayari kusubiri mpaka Mungu atakapo mwamuru awaambie watu kuwa huu ni wakati wa chakula.

Picha ya Sita: Wenye ukoma wanne

Picha ya Sita: Wenye ukoma wanne

2 Wafalme 7:3-20

Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika katika kambi ya washami, kumbe! Hapana mtu. Kwa maana Bwana alikuwa amewaogopesha Washami kwa kishindo cha magari ya vita, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa(SE). Washami wakaogopa wakadhani adui zao wamefika, Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na vitu vyao vyote, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. Wakaenda nyumbani kwa mfalme wa Israeli wakambambia. Mfalme akashangaa sana.
**MB** Rafiki mpendwa, kama walivyo fanya wale wanye ukoma wanne, ndivyo tutanavyo takiwa sisi tufanye yaani kuwaambia wengine habari za juu ya habari njema. Si vema kama tukinyamaza kimya. Yatupasa tuwaambie wengine habari za Yesu, ili wamjue Yeye.

Picha ya Saba: Yona alimkimbia Mungu

Picha ya Saba: Yona alimkimbia Mungu

Yona 1:1-17

Baada ya Elisha kufa miaka mingi, akatokea nabii mwengine katika Israeli aliyeitwa Yona. Mungu akamwambia Yona, "Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu." Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akaenda hadi mji uliyoitwa Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ili ajiepushe na uso wa BWANA. Lakini BWANA alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika. Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee. Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, natupige kura, tupate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.
**MB** Rafiki mpendwa, Yana lionenka ni mtu mjinga, je, angeweza kumkimbia Mungu? Lakini sisi pia tunafanana na Yona. Hatutaki kufanya yale ambayo Mungu anata tuyafanye. Mungu akitutuma kwenda kuwasaidia watu tusio wapenda twajua ni vigumu kufanya hivyo. Nilazima tumuombe Mungu atubadirishe mioyo yetu mioyo yao, lakini tukijaribu kumkimbia Mungu hiyo aisaidii. Tunapo mtii Mungu, Mungu anatupa furaha.

Picha ya Nane: Yona na Samaki Mkubwa

Picha ya Nane: Yona na Samaki Mkubwa

Yona 1:8 - 2:10

Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha BWANA, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa BWANA, kwa sababu alikuwa amewajulisha. Basi akamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata. Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. Ndipo wale watu wakamwogopa BWANA mno, wakamtolea BWANA sadaka, na kuweka nadhiri. BWANA akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku. Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki. Baada ya siku tatu yule samaki, akamtapika Yona pwani. Naye Yona alikuwa hai.
**MB**Rafiki mpendwa, Mungu anapenda watu wote, mara kwa mara tunapo mkosea Mungu, Yeye anatusamehe. Mungu anataka kila mtu amfuate Yeye. Yeye yupo tayari kumpokea kila mtu.

Picha ya Tisa: Yona akiwa Ninawi

Picha ya Tisa: Yona akiwa Ninawi

Yona 3:1-10

Baada ya hayo, Bwana akamwambia Yona mara ya pili, akisema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
**MB**Ndugu yangu, Sisi pia tuna fanana na Yona, pia tuna fanana na watu wa Ninawi, kwani walitenda matendo ya kumchukiza Mungu. Lakini tukitubu na kumuomba Mungu atusamehe, Yeye atatusamehe. Nilazima tuamini kwamba Yesu ni mwokozi, tuziache dhambi na kumfuata Mungu. Yesu yupo tayari kutusamehe dhambi yezu na kutupa uzima wa milele.

Picha ya Kumi: Esta na Mfalme

Picha ya Kumi: Esta na Mfalme

Esta 1:1 - 2:18

Miaka mingi baada ya Yona, ilitokea taifa lingine ambalo ilikuja kupinga na Israeli. Maadui hao waliuharibu mji wa Yerusalem na kuwateka mateka Waisraeli. Baada ya miaka mingi kupita mfalme wa nchi hiyo alikuwa akitafuta msichana mzuri wa kumuoa. Basi mfalme huyo akamuona Esta naye akampenda sana. Na Esta alikuwa mwisraeli aliyetwa kwenda katika nchi hiyo, lakini mfalme hakujua jambo hilo. Wazazi wa Esta walikufa na Esta wilikuwa na mtu aliyeitwa Mordekai. Baada ya Esta kuolewa na mfalme, Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa nyumba ya mfalme, ili ajue hali yake Esta, na hayo yatakayompata, Mordekai alikuwa akiwasiliana sana na Esta. Lakini mfalme hakujua jambo hili, wala hakujua kwamba Esta alikuwa binamu yake Mordekai. Waisraeli walipokuwa katika nchi ya ugenini walijaribu kumpendeza Mungu, na waliishi kama watu wa Mungu. Lakini ilikuwa ni vigumu kwao kwani walikuwa katika nchi ya ugenini. Watu walio kuwa wakiishi nao, wale walio kuwa wakiwatawala hawakumjua Mungu wa Israeli. Waisraeli wali hitaji kuwa waangalifu, kwasababu walikuwa na maadui wengi waliotaka kuwaangamiza. Lakini kumbuka kwamba Israeli ilikuwa taifa la Mungu, na Mungu aliwapenda. Endelea kusikiriza na utasikia jinsi Mungu alivyo waokoa.

Picha ya Kumi na Moja: Mordekai Akataa kuabudu

Picha ya Kumi na Moja: Mordekai Akataa kuabudu

Esta 3:1 - 4:17

Baada ya hayo alikuwep mtu mmoja jina lake aliitwa Hamani. Hamani alikuwa mtu mkubwa sana wa cheo na alikuwa mtu alie faamika sana katika nchi hiyo. Na kwasababu ya alikuwa mtu maalum sana watu wote waliinama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia. Mordekai alijua kwamba ni Mungu tu anaye itaji kusujudiwa. Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana. Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, akisema kuna Waisraeli humu, nao hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo nilazima tuwaangamize. Basi, mfalme akasema nivema waangamizwe; nami nitawalipa fedha watakaosimamia shughuli hiyo. Basi Mordeikai alipo sikia amri ya mfalme alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu. Pia akafika hata mbele ya mlango wa mfalme; maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa magunia. Basi Mordekai akawatuma watu kwa Esta wakamwambie, Nilazima uwatete watu wako kwa mfalme ili wasife. Lakini Esta aliposikia kwamba Mordekai yupo nje ya nyumba ya mfalme aliogopa sana, kwani ilikuwa ni sheria ya mfalme, mtu akija katika nyumba ya mfalme bila kuitwa atauawa. Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai, "Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria na kuwatetea Waisraeli; kama kufa na nife.
**MB** Rafiki mpendwa, pengine ni vigumu kwetu kufanya mapenzi ya Mungu kama alivyo fanya Mordekai. Bila shaka kuna watu wanao taka kutufanyia mambo mabaya kwa vile tunavyo mpenda Mungu. Mungu ni Mungu mwenye nguvu. Anaweza kutusaidia kufanya na sema yale anayo taka.

Picha ya Kumi na mbili: Esta Akiwa Katika Karamu

Picha ya Kumi na mbili: Esta Akiwa Katika Karamu

Esta 5:1 - 7:10

Mungu alifanya jambo la ajabu kumsaidia Esta na watu wa Israeli. Esta akaenda kwa mfalme na mfalme akamsikilia. Baada ya hayo Esta akamkaribisha mfalme na Hamani katika karamu. Na walipo fika katika sherehe hiyo mfalme akamuuliza Esta, unataka nikufanyinini? Lolota utakalo nitakufanyia. Basi Esta akasema tafadhari uniokoe mimi pamoja na watu wangu. Na ufuitilie mbali siku ile uliyo ipanga ilikuwa angamiza Waisraeli. Basi mfalme akaghaili moyoni mwake. Na Esta na Mordekai na watu wa Israeli wakawa salama.
**MB** Rafiki mpendwa, Esta alikuwa tayali kufa, ili kuwaokoa wa wa Israeli kwasababu aliwapenda watu wa Israeli na alimpenda Mungu. Je, unajua kwamba Yesu anawapenda watu wote ndio maana akafa?

Picha ya Kumi na tatu: Danieli na rafiki zake

Picha ya Kumi na tatu: Danieli na rafiki zake

Danieli 1:1-20

Hapozamani palikuwa na manabii wengi sana kama Elisha na Yona. Hawa walikuwa watu wa Mungu waliochukua ujumbe kutoka kwa Mungu na wapa Waisraeli. Na ujumbe huo ulikuwa ukiwa onya ili wasimuache Mungu na kuabudu miungu mingine. Lakini mara kwa mara Waisraeli hawakufunya yale ambayo waliambiwa. Na kila walipo muacha Mungu walijikuta wakishindwa katika vita. Lilitokea taifa lingine lililoitwa Babeli na mfalme wao aliitwaa Nebukadneza. Watu wa Babeli wali ubomoa tena mji wa Yerusalemu na waliwatesa sana waisraeli. Basi Waisraeli walikuwa katika utumwa, wakitumikishwa na mfalme Nebukadneza. Mfalme akamwambia mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana wasio na dosali, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria. Basi vijana hao wakajifunza elimu ya Wakaldayo. Danieli na rafiki zake walimpenda Mungu na walitaka kumpendesa Mungu kuliko mfalme. Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. Ndipo Danieli akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria, Danieli akamwambia, tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona. Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi. Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu.

**MB**Rafiki mpendwa, Danieli na rafiki zake walikuwa na ujasili mkubwa na waliweza kumtegemea Mungu. Wao alimtegemea Mungu tu ingawa walikuwa katika wakati mgumu. Danieli na rafiki zake walitaka kumpendaza Mungu tu.

Picha ya Kumi na nne: Danieli na Mfalme wa Babeli

Picha ya Kumi na nne: Danieli na Mfalme wa Babeli

Danieli 2:1-49

Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, hata akakosa usingizi. Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, wapate kufasiri ndoto ya mfalme. Lakini waganga na wachawi hawakuweza kuifasiri ndoto ya mfalme. Ndipo Danieli akaitwa na mfalme. Ndipo Mfalme, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake. Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu; lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi; Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na iling'aa sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. Na Hii ndiyo tafsiri yake mbele ya Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu; na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu. Na baada yako atainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; utawa wavunja-vunja adui zako. Baada ya Danieli kuifasiri ile ndoto. Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri.
**MB**Rafiki mpendwa, habari hizi zina tusaidia sisi tuelewe kwamba Mungu ndiyo anaye watawala wafalme, Naye ni mwenye mamlaka. Na uwafalme wako kutadumu milele. Danieli aliamua kumtegemea Mungu. Mungu bado anatawala hata leo. Tunaweza kumtegemea, tuna itaji kumpenda. Na kuwa waaminifu kwake kama alivyo fanya Danieli

Picha ya Kumi na tano: Muujiza wa Mungu

Picha ya Kumi na tano: Muujiza wa Mungu

Danieli 3:1-20

Mfalme Nebukadreza alifanya sanamu ya dhahabu. Na alitaka kila mtu aiabudu hiyo sanamu. Mfalme akaamulu ipigwe mbiu ili watu wote watangaziwe. Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima muanguke na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao. Lakini Danieli na Meshaki na Shadraka na Abednego walikataa kuiabudia sanamu. Na mfalme aliposikia kwamba Danieli na rafiki zake wamekataa kuisufudia sanamu, mfalme akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. Danieli na wenzake wakamwambia mfalme wakasema, Mungu wetu aweza kutuokoa na moto huu. Basi vijana hao wakatupwa katika tanuru, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto.

Picha ya Kumi na Sita

Picha ya Kumi na Sita

Danieli 3:21-30

Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa Mungu. Kisha Nebukadreza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto. Basi mawaziri na manaibu waliokuwa wamekusanyika pamoja, wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo. Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu aliye hai.
**MB** Rariki mpendwa, Neno la Mungu lina sema "Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa." (2Timotheo 3:12) Ikiwa tuna mtegemea Mungu na kumpenda hatuitaji kuogopa kwani Yeye ni mwenye nguvu na anauwezo mkuu. Naye anaweza kutuokoa.

Picha ya Kumi na saba: Danieli Amuomba Mungu

Picha ya Kumi na saba: Danieli Amuomba Mungu

Danieli 6:1-18

Alitokea mfalme mwingine aliyeitwa Dario. Basi mfalme Dario aligundua kwamba Danieli alikuwa mtu mwaminifu na mwenye hekima. Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote. Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele. "Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba."(Danieli 6:6) Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku. Walifanya hivyo kwasababau walijua kwamba Danieli hataacha kumuomba Mungu, lakini mfalme hakujua nia yao ilikuwa nini. Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake. Na wale wakuu wakataka Danieli atupwe kwenye tundu la Simba. Hivyo ndivyo walivyo mshitaki Danieli mbele ya mfalme.Laniki mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata hakupata usingizi. Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme. Hivyo Danieli, wakatupwa katika tundu la simba.

Picha ya Kumi na nane: Danieli Katika Tundu La Simba

Picha ya Kumi na nane: Danieli Katika Tundu La Simba

Danieli 6:19-27

Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba. Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye amevifumba vinywa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake. Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu. Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu. Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata milele.
**MB** Rafiki mpendwa, Danieli alikuwa mtu mwaminifu na alimpenda Mungu. Watu walimjaribu Danieli lakini yeye hakumkosea Mungu bali alimtii. Hata leo hii watu watajaribu kutujaribu sisi. Lakini tumpenda Mungu na tukiwa waaminifu kwake, Mungu atatulinda.

Picha ya Kumi na tisa: Nehemia Mbele ya Mfalme

Picha ya Kumi na tisa: Nehemia Mbele ya Mfalme

Nehemia 1:1 - 2:9

Baada ya miaka baada ya Danieli. Alikuwepo mtu aliyeitwa Nehemia. Nehemia alikuwa ni mwisraeli aliyeishi katika nchi ya Babeli. Kazi ya Nehemia ilikuwa ni kutengezene vinywaji kwa ajili ya mfalme. Siku moja rafiki zake Nehemia walimtembea Nehemia, Nao walikuwa wapetoka katika nchi ya Israeli. Nao walipofika kwa Nehemia walimwambia, watu waliosalia huko katika nchi ya Israeli, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto. Nehemia aliposikia habari hizo aliuzunika sana. Lakini aliendelea kufanya kazi katika nyumba ya mfalme. Siku moja mfalme akamuona Nehemia akiwa katika hali ya uzuni. Mfalme akamuuliza Nehemia, Mbona uso wako unaonyesha huzuni? Au huna ugonjwa? Basi Nehemia kamjibu mfalme akisema, nimepata habari kwamba ukuta wa Yerusalemu umeanguka, na sijui nitafanya nini. (Naye Nehemia likuwa kimuomba Mungu katika moyo kwake) Basi Nehemia akamwambia mfalme, ukion vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali uniruhusu niende mpaka Yerusalemu ili pate kuujenga ukuta. Basi mfalme akamruhusu, naye akampa vitu vyote alivyo itaji ili kukamilisha katika ya ujenzi.
**MB**Rafiki mpendwa, Nehemia aliwajari sana watu wa nchi yake. Nehemia alitaka jina la Mungu liendelee kutukuzwa. Nehemia aliamua kumtegemea Mungu kwani alijua kwamba Mungu ni mwenye nguvu nyingi, naye atamsaidia. Sisi tukiinga mfano wa Nehemia, Mungu atafanya mambo makuu kati ya watu wetu na jamii zetu.

Picha Ishiri: Nehemia Akagua Ukuta Uliobomoka

Picha Ishiri: Nehemia Akagua Ukuta Uliobomoka

Nehemia 2:11-20

Nehemia akaondoka katika nchi ya Babeli na kuelekea Yerusalemu. Mfalme akaamuru baadha ya watu wafuatane na Nehemia. Pia mfalme akaamuru askari waruatane na Neemia ili wamlinde. Basi Nehemia na watu waliofuatanane waliingia katika mji wa Yerusalemu. Lakini watu wa Israeli walikasiri waliposikia kwamba Nehemia amekuja wa watu wengine, kwani hawakutaka kusaidiwa na watu wengine. Lakini Nehemia alijua kwamba Mungu atakuwa pamoja naye. Baada ya siku chache, Nehemia akaenda usiku kukagua ukuta wa Yerusalemu. Alienda kwa siri ili maadui zake wasimuone. Kesho yake asubuhi Nehemia akawa wakusanya viongozi wa wazee wa Israeli. Naye akawambia vile Mungu alivyo mfanikisha kufika ilikuujenga huo ukuta. Pia kawaambia, Mungu ametupa nguvu na uwezo wa uujenga huu ukuta, haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tuiondoe aibu iliyo tukuta. Basi hao wazee ni viongozi wa Israeli wakakubari kuujenga ukuta. Lakini maadui zao waliwacheka walipo sikia habari hizo za kuujenga ukuta. Lakini Nehemia akasema "Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga".

Picha ya Ishirini na moja: Kuujenga Ukuta

Picha ya Ishirini na moja: Kuujenga Ukuta

Nehemia 3:1 - 6:18

Lakini ikawa maadui wa Israeli waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu zinaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno; wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo. Na Nehemia alipo sikia juu ya sharui lao akaomba dua Mungu, tena akaweka askari wa ulinda, mchana na usiku, kwa sababu yao, ili kuwapinga. Basi Nehemia kawaambia wakuu, na mashehe, na watu wengine waliobaki, Msiwaogope; mkumbukeni Bwana, aliye mkuu mwenye kuogofya, Yeye atatusaidia. Kisha ikawa, adui zeo waliposikia ya kuwa wamekwisha kupata habari, na ya kuwa Mungu amelibatilisha shauri lao, ndipo watu wote wakarudi ili uujenga ukutan, kila mtu kwa kazi yake. Basi Nehemia na watu wake wakamaliza kazi ya uujenga ukuta.
**MB** Rafiki mpendwa, Tumbuke kwamba, tunapo mtumikia Mungu tunaweza kukutana na mambo magumu. Lakini tusife moyo, Mungu wetu ni Mungu mkuu na mwenye nguvu nyingi kuliko adui yetu, Naye anaweza kutusaidia.

Picha ya Isharini na mbili:Ezra Asoma Tolati

Picha ya Isharini na mbili:Ezra Asoma Tolati

Nehemia 8:1 - 13:31

Baada ya ukuta wa Yerusalamu kujengwa. Waisraeli waliweza kuishi kwa usalama. Na watu wote wa Israeli wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha torati ya Musa, BWANA aliyowaamuru Israeli. Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu, basi watu wote wakalia, walipoyasikia maneno ya torati maana walijua kwamba hawakumtii Mungu. Lakini Nehemia, Ezra na makuhani, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Hivyo Walawi wakawatuliza watu wote, wakasema, Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu; wala msihuzunike. Baada ya siku chache Nehemia akawachukua watu wote ilikwenda kuuwe wakfu ukuta wa Yerusalemu. Ndipo Nehemia akawapandisha wakuu wa Yuda juu ya ukuta, akawaagiza watu wote wauzunguke Basi Israeli walianza kusifu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi.
**MB** Rafiki mpendwa, Nehemia alijua kwamba Mungu atamsaidia, na aliwahimiza Waisraeli kumtumaini Mungu. Sasa wote wakawa wakimfisu Mungu kwa pamoja. Hata sisi tunapo kuwa katika hali ngumu tunaweza kumtegemea Mungu ili yeye atusidie, na tunaweza kuwatia moyo wengine ili wamtememee Mungu.

Picha ya Ishirini na tatu: Yesu msalamani

Picha ya Ishirini na tatu: Yesu msalamani

Yohana 19:17-30; Warumi 5:8

Baada ya miaka mingi kupita, yaani baada ya Danieli na Nehemia, Mungu alimtuma wanawe Yesu, ulimwenguni. Yeu alileta Neno la Mungu kwa Wasraeli. Aliwa onyesha vile inavyo fapasa waishi ilikumpendeza Mungu. Yesu alimpenda na kumtii Mungu katila kilakitu alicho fanya. Kama tulivyo jifunza habari za Elisha na Danile na manabii wengine, Yesu pia likuwa na maadui wengi sana. Viongozi wa Israeli alikuwa wakitafuta sababu ya kumuua. Atimaye aliamua kumsulubisha. Watu walimpega Yesu na kumdhihaki, na mwishowe serikali ya kirumi alimchukua Yesu na kwenda kumsulumisha, ingawa hakufanya kosa lolote. Mwalimuwa Yesu lakini yeye alifufu tena. Maadui wa Yesu walifikiri kwamba akifa Yesu ndio mwisho wake wa kuishi, lakini Mungu alifufu Yesu kutoka katika wafu. Ulikuwa ni mpango wa Mungu kwamba Yesu afe na kufufuka tena. Kukikuwa hakuna njia nyingine ya kumokoa mwanadamu isipokuwa, Yesu kutoa uhai wake kwa ajili ya mwanadamu. Hii ni mpanga wa wokovu. Ingawa shetani alijaribu kuharibu mpango wa Mungu. Lakini alishindwa. Mungu ni mwenye nguvu, kuliko Shetani. Yesu alikufa msalambani na akafufu baada ya siku tatu, naye alishinda mauti. Yesu alikufa ili sisi tupate uzima wa milele. Tikumuomba Yesu atusamehe dhambi zetu yeye atafanya hivyo.
**MB**Rafiki unaye nisikiliza,Wakati mwengine watu wasio mjua Mungu wanaweza kutufanya mambo mabaya kwasababu tunamfuata Yesu. Lakini Yesu alisema, atakuwa pamoja nasi. Naye ataishi ndani yetu na kutupa uwezo. Mruhusu Yesu atawale maisha yako leo.

Picha ya Ishirini na Nne: Yesu Aonyesha Njia ya Uzima

Picha ya Ishirini na Nne: Yesu Aonyesha Njia ya Uzima

Mathayo 7:13; Yohana 14:6

Kaika pia unaweza kuona watu wanne wanao tembea katika njia pana. Hii njia pana nikama barabara ya maisha yetu na kila mtu anapitia njia hiyo, yaani maada yake sisi tote kumezaliwa katika hali ya dhambi, na tumetengena na Mungu, na baada ya kufa tutakwenda katika moto unaowaka milele, kama unavyo ona katika picha. Je, unaweza kuona Yesu katikapicha? Anawaonyesha watu njia nyembamba inayo enda uzimani. Yesu anasema, "mimi ndimi njia ya kweli na uzima" Yesu anataka watu wote waende mbinguni. Yesu alipokufa msalamani alitulipia deni yetu ya dhambi. Nilazima tuchague, ikiwa tunataka kupia njia ya Yesu, tunaweza kumuomba yeye. Njia ya Yesu ni nyembamba. Watu wengi wanachakua kupita njia pana. Sisi tuliochagua njia ya Yesu, Yesu yuko pamoja nasi, shetani na malaika zake hawawezi kutushinda. Nguvu za Yesu zimemshinda Shetani. Yesu atatupa nguvu ilituwe washindi. (Mtume Paulo) anasema, "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu"
**MB** Rafiki naye nisiliza, Elisha, Danieli, Nehemia na Esta hao wote ni vielelezo vizuri kwetu ambavyo tuna weza kufuata. Watu hawa walitaka kumpendaza Mungu katika kila kitu walicho fanya. Mambo mengine alikuwa magumu kwao, lakini waliona ni vema kumpendaza Mungu tu. Badala ya kuangaika walimuomba Mungu ili wasaidie. Sisi pia tunaweza kufanya hivyo. Nilazima tumtegemee Yesu katika yote kunayo yafanya atakama tunapatwa na mabaya nilazima tumtegemee yeye tu. Tukumbuke kwamba Mungu akajua kila kitu, naye anatujali sisi tulio wake. Ikiwa kumechakua kufuata njia ya Yesu hatupaswi kuogopa kitu, kwani Yesu yuko pamoja nasi.

Katulad na kaalaman

Libreng mga download - Dito ay matatagpuan ang lahat ng pangunahing scripts mensahe ng GRN sa ibat-ibang wika, at mga larawan at iba pang katulad na materyales, ay maaari ng i-download.

Audio-visual ng "Magmasid, Makinig at Mabuhay" - Ang kabuuan ng 8 programa na may 24 na larawan bawat isa para sa pag-eebanghelyo at katuruang Kristiyano. Ang serye ay nagbibigay ng aral sa mga tao ng Lumang Tipan, ang buhay ni Hesus, at ang unang Simbahan.

Paano gamitin ang mga Audio visual ng GRN - 1: Ibahagi ang Mabuting Balita sa pinadaling paraan - Ang artikulong ito ay nagbibigay panimula sa ibat-ibang paraan kung paano magagamit ang mga audio visual ng GRN sa ministeryo.

Paano gamitin ang kagamitan ng GRN Audio visual - 2: Maging mas Malalim - Ang artikulong ito ay nagbibigay ng karagdagang paliwanag kung paano natututo ang mga tao mula sa mga kwento, at bakit ang mga kwento ay walang masyadong komentaryo.

Ang GRN Aklatang Audio - Pag-eebanghelyo at panimulang kagamitan ng katuruang Bibliya na angkop sa mga pangangailangan at kultura ng mga tao sa isang iba't ibang estilo at mga format.

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares its audio, video and written scripts under Creative Commons

Creating DVDs using the GRN Slide show Videos - How to burn DVDs for specific people groups you are trying to reach