unfoldingWord 48 - Yesu ndiye Masihi aliyeahidiwa
Contur: Genesis 1-3, 6, 14, 22; Exodus 12, 20; 2 Samuel 7; Hebrews 3:1-6, 4:14-5:10, 7:1-8:13, 9:11-10:18; Revelation 21
Numărul scriptului: 1248
Limba: Swahili
Public: General
Scop: Evangelism; Teaching
Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture
Stare: Approved
Scripturile sunt linii directoare de bază pentru traducerea și înregistrarea în alte limbi. Acestea ar trebui adaptate după cum este necesar pentru a le face ușor de înțeles și relevante pentru fiecare cultură și limbă diferită. Unii termeni și concepte utilizate pot necesita mai multe explicații sau chiar pot fi înlocuite sau omise complet.
Textul scenariului
Mwenyezi Mungu alipoumba ulimwengu, vitu vyote vilikuwa sawa pasipo dosari yoyote. Hapakuwa na dhambi, wala magonjwa, wala kifo duniani. Adam na Mkewe, Eva, walipendana sana na walimpenda Mungu pia. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyokusudia ulimwengu uwe.
Katika bustani ya Edeni, Shetani alijitokeza kama nyoka. Akazungumza na Eva kwa lengo la kumdanganya. Kwa njia hiyo, Adam na Eva wakawa wamemtenda Mungu dhambi, na leo watu wote duniani tunaweza kuugua na kufa kama matokeo ya dhambi.
Jambo jingine la hatari zaidi likajitokeza kama matokeo ya dhambi ya Adam na Eva. Uhusiano wao na Mungu ukaharibika na toka wakati huo, kila mwanadamu anazaliwa akiwa na asili ya dhambi, akiwa hana mahusiano mazuri na Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu akawa na mpango wa kurejesha uhusiano ulioharibiwa na dhambi baina ya mwanadamu na Mungu.
Kupitia mpango huo, Mwenyezi Mungu aliahidi kuwa mmoja wa wazaliwa katika uzao wa Eva atakiponda kichwa cha shetani, na shetani atakigonga kisigino chake. Maneno haya yana maana kwamba, shetani atamuua Masihi, lakini Mwenyezi Mungu atamfufua tena, na kisha huyo Masihi atazishinda nguvu za shetani milele. Baada ya miaka mingi kupita, Mwenyezi Mungu akaudhihirishia ulimwengu kuwa Yesu ndiye Masihi.
Katika siku zile Mwenyezi Mungu alipouangamiza ulimwengu kwa mafuriko, aliandaa chombo cha kuwaokoa na gharika hilo watu wote waliokuwa wanamwamini. Kwa sababu ya dhambi, ni kwa namna iyo hiyo, watu wote duniani wanastahili kuangamizwa. Lakini ashukuriwe Muwenyezi Mungu aliyemtoa Yesu kumuokoa kila mtu anayemwamini.
Katika kipindi cha mamia ya miaka, makuhani wakadumu katika kutoa sadaka za kuteketezwa, wakidhihirisha aina ya adhabu iliyowapasa kupewa kwa ajili ya dhambi zao. Hata hivyo, sadaka hizo hazikuweza kabisa kuwaondolea dhambi zao. Hivyo, Yesu ndiye kuhani mkuu asiyelingana na makuhani wengine. Yeye alijitoa nafsi yake mwenyewe ili awe sadaka ya pekee ya kuteketezwa kwa ajili ya kuziondoa dhambi za watu wote duniani. Yesu ndiye kuhani mkuu wa kweli maana alibeba adhabu ya dhambi iliyotendwa na watu wote.
Ndipo Mwenyezi Mungu akazungumza na Ibrahimu akamwambia, "Kupitia wewe Ibrahimu, watu wa kila kabila duniani wamebarikiwa." Naye Yesu alitokana na uzao wa Ibrahimu, na watu wa kila namna wanabarikiwa kupitia Ibrahimu. Hivyo, kila anayemwamini Yesu ameokolewa kutoka katika dhambi, na anafanyika kuwa uzao wa Ibrahimu kwa jinsi ya kiroho.
Mwenyezi Mungu alipomwagiza Ibrahimu kumtoa mwanae, Isaka, kama sadaka ya kuteketezwa na akatii, Bwana Mungu akampatia Ibrahimu mwana kondoo achinjwe na kutolewa sadaka badala ya mwanae, Isaka.Hii inatufundisha kuwa sisi sote tunastahili kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini Mwenyezi Mungu amemtoa Yesu, mwanakondoo wa Mungu ili atolewe kama sadaka na kisha kufa badala yetu.
Hata Mwenyezi Mungu alipoamuru mapigo saba katika nchi ya Misri, aliagiza kila familia ya kiisraeli kuchinja mwana kondoo asiye na kasoro na kisha kunyunyiza damu ya kondoo juu na chini ya miimo ya milango yao. Na ndipo Mwenyezi Mungu alipoiona damu katika miimo ya milango yao, aliziruka nyumba zile na hakuwauwa watoto wao wa kiume wa kwanza .Tendo hilo linajulikana kama pasaka.
Yesu hakuwa na kosa wala dhambi yoyote na aliuawa katika kipindi cha maazimisho ya pasaka. Hakika Yesu ndiye mwanakondoo wetu wa pasaka. kwa yeyote anaemwamini Yesu, damu yake Yesu hulipia dhambi za mtu huyo na adhabu ya Mungu humruka mtu huyo.
Ni kweli kuwa Mwenyezi Mungu alifanya agano na watu wake, taifa la Israel. Bali sasa Mwenyezi Mungu anafanya agano lililo wazi kwa kila mtu. Kwa sababu ya agano hili jipya, watu wote wa kila mahali, wanaweza kuwa sehemu ya watu wa Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo.
Japokuwa Musa pia alikuwa ni nabii mkubwa aliyetangaza neno la Mungu, Yesu ndiye nabii mkuu zaidi ya manabii wote.Kila jambo alilolifanya na kulisema Yesu lilikuwa ni tendo na neno la Mungu kwakuwa yeye ni Mungu. Ndio maana wakati mwingine Yesu anaitwa neno la Mungu.
Mungu alimuahidi mfalme Daudi kuwa mmoja ya wazaliwa wake atawatawala watu wa Mungu milele. Kwakuwa Yesu ni mwana wa Mungu na Masihi, yeye ndiye yule mzaliwa wa uzao wa Daudi atakayetawala milele.
Daudi alikuwa mfalme wa Israeli, lakini Yesu ni mfalme wa ulimwengu wote. Atarudi tena kuutawala ufalme wake kwa haki na amani milele.