ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha tatu: Hushindi kupitia Mungu

ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha tatu: Hushindi kupitia Mungu

Samenvatting: Joshua, Deborah, Gideon, Samson. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.

Scriptnummer: 420

Taal: Swahili: Tanzania

Thema: Eternal life (Salvation); Character of God (Nature, character of God, Word of God (the Bible), Power of God / Jesus); Living as a Christian (Obedience, No other gods, idols, Victory, Faith, trust, believe in Jesus); Bible timeline (Gospel, Good News); Sin and Satan (Spiritual Warfare, Deliverance, Judgement)

Gehoor: General

Stijl: Monolog

Genre: Bible Stories & Teac

Doel: Teaching

Bijbelse verwijzing: Extensive

Toestand: Publishable

Tekst van het script

Utangulizi

Utangulizi

Waisraeli wakaa katika nchi ya Misri, lakini Mungu akawatoa kutoka katika nchi ya utumwa na kuwarudisha katika nchi iliyo itwa Kanaani. Mungu aliwaahidi kwamba nchi ya Kanaani itakuwa ni nchi yao Katika kaseti hii tutajifunza zaidi habari za watu wa Israeli na vile Mungu alivyo wasaidia kurudi katika nchi ya Kanaani. Angalia katika kitabu chako chako. Unaposikia sauti hii ___________ ufungue picha inayofuata. Sasa ufungue katika picha ya kwanza kisha tutaanza.

Picha ya kwanza: Yoshua afanya vita na Waamaleki

Picha ya kwanza: Yoshua afanya vita na Waamaleki

Kutoka 17:8-13

Kiongozi wa Israeli ambaye aliitwa Musa, alikuwa na msaidi wake na jina laki aliitwa Yoshua. Na Waisraeli walipokuwa katika safari yao ya kuelekea Kanaani walikutana na maadui, walioitwa Waamaleki. Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kila, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. **MB** Rafiki mpendwa, Yesu ni kiongoze wa vita katika jeshi la Mungu. Shetani ni adui mbaya nawadangana watu wache kumfua Yesu. Lakini tukimwita Yesu atusidie, Yeye atatusidia.

Picha pili: Wapelezi walirudi na matunda kutoka Kanaani

Picha pili: Wapelezi walirudi na matunda kutoka Kanaani

Hesabu 13:1-33

Musa akawatuma wapelelezi ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Nendeni sasa mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au wengi; na nchi wanayoikaa kwamba ni njema au mbaya. Iweni na moyo mkuu, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza. Basi wakapanda wakaipeleleza nchi toka yote. Wakafika bonde la Eshkoli, na huko wakakata tawi lenye kishada kimoja cha zabibu, wakalichukua kwa mti kati ya watu wawili; wakaleta makomamanga pia, na tini. Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini. Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi. Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko. Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza. Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu anapotuahidi kufanya kitu furahi, huamini kwambwa yeye atafanya. Kuna ahadi nyingi ambazo ametupa katika Neno lake. Nilazima tuamini kwamba yey atafanya.

Picha ya tatu: Watu wa Israeli walivuka mto Yordani

Picha ya tatu: Watu wa Israeli walivuka mto Yordani

Yoshua 3:1-7

Watu wengi walikufa kabla ya kuingia katika nchi ya Kanaani. Musa pia alikufa kabla ya kuingia katika nchi ya Kanaani. Watu wengine wengi walikufa kwa ajili ya kumuashi Mungu. Baada ya Musa kufa Yoshoa akawa iongozi wa Israeli.Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. Yoshua akwaambia watu Waisraeli waanze safari. Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipokanyaga katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno), ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana. Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la BWANA wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani. Hivyo wana Waisraeli wakavuka mto wa Yordani kwa ushindi mkuu wa Mungu.
**MB** Rafiki mpendwa, Ni muhimu sana kujifunza Neno la Mungu na kulifanyia kazi. Wakati mwingine tunao ni vigumu kufanya yale mambayo Neno la Mungu limutuambia kufanya. Nitupasa tumtegeme Mungu iliatuwezeshe kufanya. Baada ya kufauru tutapa amani na furaha. Mungu tu ndiye atakaye tuwezesha kushinda.

Picha ya nne: Ukuta wa Yeliko ulianguka

Picha ya nne: Ukuta wa Yeliko ulianguka

Yoshua 6:1-27

Wana wa Israeli walikuwa wameingia katika nchi waliyo ahidiwa na Mungu yaani nchi ya Kanaani. Jambo la kwamza ambalo waliitaji kufanya ni kuwafukuza watu wote walio ingia katika nchi yao. Mungu aliwaamba Waisraeli kwamba wao walikuwa taifa teule, na wasichangamane na watu wa mataifa mengine.

Yoshua, akawatuma watu wawili kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi. Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi. Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka.

Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? Akasema, La, mimi ni amiri jeshi wa Bwana. Yoshua akasujudu, akamwuliza, Huyo amiri jeshi wa BWANA akamwambia Yoshua, nchi hii impomikononi mwenu. Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. Walipokuwa wakiukaribia mji Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele. Basi akalipeleka sanduku la BWANA liuzunguke huo mji, likauzunguka mara moja, kisha wakaenda kambini wakakaa kambini. Waliuzunguka mji kila siku wa siku sita. Ilipofika siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba Hata mara ya saba ilipofika makuhani wakazipiga tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana BWANA amewapeni mji huu. (SE) Watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ukuta wa mji ukaanguka kabisa (Local SE thump). Watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kupiga kalele, wakautwaa huo mji. Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji. Waka wauwa watu wote, ilawalimuacha hai Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo. Wana wa Israeli walipata ushindi mkubwa sana. Kwakamsifu Mungu kwa ushindi huo.

Picha ya tano: Israeli walishinda na watu wa mji wa Ai

Picha ya tano: Israeli walishinda na watu wa mji wa Ai

Yoshua 7:1-12

Wana wa Israli walikuwa na furaha kubwa, kwasababu waliushinda mji wa Yeriko. Lakini kulikuwa na maadui wengine waliokaa katika mji wa uliyoitwa Ai. Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ili waupeleleze mji. Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, Wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige mji wa Ai, maana watu hao ni wachache tu. Basi watu wakaenda huko wapata elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele ya watu wa Ai. Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; na waisraeli wakakimbia. Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao. Yoshoa akamlilia Bwana juu ya mjambo hili. BWANA akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi? Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe. (maana Bwana aliwaambia wasichuke kitu hata kimoja katika mji wa Yeruko) Ndiyo maana wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
**MB** Rafiki mpendwa, Akani ndiye aliye chukua kitu hicho na alifikiri akuna mtu aliye muona. Lakini Mungu alimuona. Kwasababu ya dhambi hiyo ya kuiba na kuficha taifa lote la Israeli aliadhibiwa kwa kushindwa vita. Sisi pia yatupasa tuishi maisha ya kumpendeza Mungu alitusiwakoseshe wengine. Akani alimchukuza sana Mungu. Sisi tusimchukize Mungu maana atatuadhibu.

Picha ya sita: Hukumu ya Akani

Picha ya sita: Hukumu ya Akani

Joshua 7:14-26

Siku ya pili yake Yoshua kawakusanya watu wa Israeli na kuongea nao. Yoshua aliwaambi watu hao kwamba walipigwa na watu wa Ai kwasababu mtu mmoja kati ya watu wa Israeli walikuwa amemuasi Mungu na kuficha vitu vilivyo wekwa wafu. Basi Yoshua, akawasogeza Israeli kabila kwa kabila; kabila ya Yuda ikatwaliwa. Akazisogeza jamaa za Yuda, akaitwaa jamaa ya Wazera; akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa. Akawasogeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, wa kabila ya Yuda akatwaliwa. Yoshua akamwambia Akani, Mwanangu, nakusihi, usitufiche kitu useme yalio kweli mbele za Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche. Akani akamjibu Yoshua, akasema, Kweli nimefanya dhambi juu ya BWANA, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na haya. Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake. Basi Yoshua akatuma wajumbe wakapiga mbio mpaka hemani; na tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, na ile fedha chini yake. Wakavitoa kutoka hapo katikati ya hema, wakavileta kwa Yoshua, na kwa wana wa Israeli wote, nao wakaviweka chini mbele za BWANA. Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.
**MB** Rafiki yangu unae nisikiliza, hatuwezi kupata ushindi tukiwa na dhambi katika maisha yetu. Nilazima tuziungame dhambi zetu na kugeukia Mungu, ndipo atakapo tupa nguvu za kushinda.

Picha ya saba: Jua na Mwezi vili simama

Picha ya saba: Jua na Mwezi vili simama

Yoshua 10:1-14

Bwana akawapa nguvu waisraeli nao wakaushinda mji wa Ai. Basi watu waliokaa katika nchi ya kanaani walipo sikia vile waisraeli walivyo angamiza mji wa Yeriko na Ai aliogopa. Wafalme wa miji mitano wakaunganika ilikupigana na waisraeli. BWANA akamwambia Yoshua, Usiwache wala usiwaogope watu hao; kwa kuwa mimi nimekwisha kuwatia mikononi mwako; hapana mtu awaye yote miongoni mwao atakayesimama mbele yako. Basi Yoshua akawafikilia ghafula; BWANA naye akawatawanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kwenda Beth-horoni. Kisha ikawa, hapo walipokuwa wakimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa katika kutelemkia Beth-horoni, ndipo BWANA alipowatupia mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao, nao wakafa; hao waliokufa kwa kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko hao waliouawa na wana wa Israeli kwa upanga. Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni. Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha angamia mbele ya adui zao. Basi Yoshua na wana wa Israeli wakarudi na ushindi mkuu.
**MB** Rafiki mpendwa, habari hizi ni za kweli, zinatusaidia tuelewe uwezo mkuu alionao Mungu. Hata leo hii nguvu za Mungu ni zile zile yeye ni mwenye nguvu milele. Mungu ameahidi katika Neno lake kwamba atawapa nguvu watu wano mtii na kumpenda, watu hao Mungu atawapa nguvu na uwezo wa kumshinda shetani.

Picha ya nane: Yoshua awapa usia watu wa Israeli

Picha ya nane: Yoshua awapa usia watu wa Israeli

Mwanzo 24:1-31

Basi Yoshua alikuwa amemaliza kazi ya kuwa ondosha audi zake katika nchi ya Kanaani. Yoshua akawagawia wana wa Israeli nchi ya Kanaani kufuatana na kabila zao. Baada ya miaka mingi Yoshua akawa mzee, akawaita wana wa Israeli ili kuongoea nao. Yoshua akasema, "nanyi mmeona mambo yote ambayo BWANA, Mungu wetu, amewatenda mataifa haya yote kwa ajili yenu; kwa maana BWANA, Mungu wetu, ndiye aliyewapigania ninyi, basi sasa sikilizeni, nilazima mumtegemee Mungu na kumpenda wala msiache kutii maagizo yake. Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA. Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache BWANA, ili kuitumikia miungu mingine; kwa maana BWANA, Mungu wetu, yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya Misri; kutoka nyumba ya utumwa; naye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya macho yetu, na kutulinda katika njia ile yote tuliyoiendea, na kati ya watu wa mataifa yote tuliopita katikati yao. BWANA ndiye aliyewafukuza watu wa mataifa yote watoke mbele yetu, naam, Waamori waliokaa katika nchi hii; basi, kwa sababu hiyo sisi nasi tutamtumikia BWANA, maana yeye ndiye Mungu wetu. Yoshua akawaambia watu, kama mkimwacha BWANA na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema. Lakini hao watu wakamwambia Yoshua, La! Lakini tutamtumikia BWANA. Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua BWANA, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi. Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii. Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.
**MB** Rafiki mpendwa, Hatuwezi kumtumikia Mungu na miungu wengine. Ni lazima tuachane na miungu mingine ndipo tumtumike Mungu. Ni lazima tumpende Mungu kwa moyo wetu wote ndipo tutakapo weza kumtumikia Mungu.

Picha ya tisa: Debora amtia moyo Baraka

Picha ya tisa: Debora amtia moyo Baraka

Waamuzi 4:1-9

Kwa miaka mingi wana Israeli waliishi katika nchi ya Kanaani. Lakini baada ya miaka mingi kizazi kipya kika zaliwa. Watu hawa hawakumjua Mungu. Wala hawakujua mafundisho ambayo Yoshua aliwafundisha babu zao. Waliishi katika dhambi. Wali mucha Mungu wa kweli na kuitumikia miungu mingine. Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya BWANA. BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, alikuwa amiri wa jeshi lake Yabini. Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa(900); naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini. Basi Mungu akawahurumia waisraeli akamtuma Debora ili awasaidie. Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, wana wa Israeli walienda kwake, ili awaamue. Huyo akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu akamwambia, Je! BWANA, Mungu wa Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawapige adui zako, huko katika mlima wa Tabori. Na Mungu mwenyewe atampiga Sisera, amiri jeshi wa Yabini, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; naye atamtia mkononi mwako. Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. Basi Debora akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe. Debora aliamini kwamba Mungu atakuwa pamoja nao.

Picha ya kumi: Mungu amsidia Baraka kumpiga Sisera

Picha ya kumi: Mungu amsidia Baraka kumpiga Sisera

Waamuzi 4:10-16

Debora na Baraka pamoja na maelfu ya askari wa Israeli wakaenda kupigana na Sisera na mfalme Yabini. Debora akamwambia Baraka, Haya! Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo BWANA amemtia Sisera katika mkono wako. Je! BWANA hakutoka atangulie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabori, na watu elfu kumi wakamfuata. BWANA akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka katika gari lake, akakimbia kwa miguu. Lakini Baraka akayafuatia magari, na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja. Huu ulikuwa ni ushindi mkubwa kwa wana wa Israeli.
**MB** Rafiki mpendwa, Baraka alijua kwa hakika kwamba Mungu anatimiza anayo sema. Tunaweza kumuamini Mungu kila wakati. Wataki mwingine nivigumu kumtegemea. Lakini Mungu amesema katika neno lake kwamba tumtumainie yeye tu.

Picha ya kumi na moja: Yaeli amuwa Sisera

Picha ya kumi na moja: Yaeli amuwa Sisera

Waamuzi 4:17-24

Sisera akakimbia kwa miguu, alaenda kujificha kwa mtu aliyeitwa Yaeli. Sisera akamwambia Yaeli naomba maji maana nina kiu, basi Yaeli akamletea kinywaji. Sisera akamwambia Yaeli, Simama mlangoni pa hema; nakuiona mtu yeyote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana. Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, (local SE)akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa. Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonyesha yule mtu unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake. Basi hivyo Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani mbele ya wana wa Israeli siku hiyo. Huu ulikuwa ni ushindi mkubwa kwa wana wa Israeli.

Picha ya kumi na mbili: Sherehe ya Wana wa Israeli

Picha ya kumi na mbili: Sherehe ya Wana wa Israeli

Waamuzi 5:-31

Waisraeli walikuwa na furaha kubwa sana baada ya kushinda katika vita. Debora na Baraka na Yaeli na watu wengine waliimbwa na kucheza kwa ajili ya ushindi mkuu. Walimsifu Mungu kwa matendo yake makuu. Waisraeli waliwashukuru Debora na Yaeli. Israeli wenyewe hawakuwa na nguvu, lakini Mungu aliwa saidia na kuwa ushindi. Israeli walimtumainia Mungu aliawape nguvu za kushinda, na Mungu alifanya hivyo.
**MB** Rafiki, Mungu anatumia watu wanoonenkana kuwa nguvu, kuwashinda wale wanojiona ni wenyenguvu. Mungu alimtuma Bwana Yesu kutuokoa kutoka kwa Shetani. Na watu wakamuwa Yesu, lakini Mungu akamfufu Yesu kutoka katika watu. Yesu alimshinda Shetani na nguvu zake. Yesu anaweza wapa nguvu watu wale wanao mpenda Mungu na kumtii. Basi na sisi tuimbe na kumshangilia Mungu wetu mwenye nguvu.

Picha ya kumi na tatu: Gideoni na Malaika

Picha ya kumi na tatu: Gideoni na Malaika

Waamuzi 6:1-24

Basi baada ya kufa kwake Debora na Baraka , Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA; BWANA akawatia mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba. Nao Wamidiani wakawate sana Waisraeli. Kisha ikawa, hapo wana wa Israeli walipomlilia BWANA kwa sababu ya Midiani, BWANA akamtuma nabii aende kwa hao wana wa Israeli. Malaika wa BWANA akaenda kwa Gideoni. Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja nawe, Ee shujaa. Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani. BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe. Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma? Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu. BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja. Gideoni akamwambia yule malaika, kama wewe ni malaika wa Bwana, basi unionyeshe ishara, ya kuwa ndiwe wewe unayesema nami. Tafadhali, usiondoke hapa hata nikujie, nikatoe zawadi yangu, na kuiweka mbele zako. Akasema, Nitangoja hata utakaporudi. Basi Gideoni akaingia ndani, akaandaa mwana-mbuzi, na mikate. Akaitia ile nyama katika kikapu, akautia mchuzi katika nyungu, akamletea , akampa. Naye malaika wa Mungu akamwambia, Itwae nyama na mikate, uiweke juu ya mwamba huu, ukaumwage huu mchuzi. Akafanya hivyo. Ndipo malaika wa BWANA akanyosha ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake, akaigusa ile nyama na ile mikate; moto ukatoka mwambani, ukaiteketeza ile nyama na mikate; malaika wa BWANA akaondoka mbele ya macho yake. Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa BWANA.
**MB** Rafiki yangu, Wakati mwingine tunakuwa kama Gideoni, tunafikiri kwamba Mungu hatusaidii. Lakini tukumbuke kwamba Mungu habadiriki. Mungu ni yeye yule jana leo na hata milele. Hata wakati mwingine tunajiona hatuna nguvu, Lakini Mungu anaweza kututumia sisi. Uendelee kusikiliza kwa makini nami nitakwambaia mambo mengi zaidi ambayo Mungu alitumia kumsaidia Gideoni.

Picha ya kumi na nne: Gideoni alibomoa madhabau ya baali

Picha ya kumi na nne: Gideoni alibomoa madhabau ya baali

Waamuzi 6:25-32

Gideoni alikua kwamba Mungu aliongea naye, na Mungu alitaka Gideoni awaongoze Waisraeli katika vita na Wamidiani. Gideoni alishangaa ni kwajinsi gani Mungu atafanya hivyo. Lakini BWANA akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope. Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu maana yake ni, BWANA ni amani. Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni.Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na Watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku. Hata watu wa mji walipoamka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa. Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata wa lipokuwa wa kiuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili. Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao yaani Gideoni, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali. Lakini roho ya BWANA ikaja juu yake Gideoni; naye akapiga tarumbeta; na Abiezeri walikutanika na kumfuata. Kisha akatuma wajumbe waende kati ya Manase yote; wao nao walikutana pamoja ili kumfuata. Kisha Gideoni akawaambia watu waliofuatana naye, mambo ambayo Mungu alimuagiza, yaani kuwapiga Wamidiani. Na watu wale wakamsikiliza.
**MB**Rafiki yangu, Labda unaishi na watu wasio penda kukuona ukimpendaza Mungu. Nilazi tuwaonyeshe watu hao kwamba Mungu wetu ni Mungu mkuu nasi tuna paswa kumtumika yeye tu. Gideoni aliharibu madhabahu ya miungu wengine na hakuogopa watu. Nasi tusi waongope watu bali tumtii Mungu.

Picha ya kumi na tano: Gideoni na Askari wake walikunya maji

Picha ya kumi na tano: Gideoni na Askari wake walikunya maji

Waamuzi 7:1-7

Wamidiani wakajiweka tayari ilikupigana na Waisraeli. Basi Gideoni kawakusa watu wake pamoja. BWANA akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, tumijioko sisi wenyewe kwa wengi wetu. Nataka kuwaonyesha Israeli uwezo wangu na jinsi mkono wangu ulivyo na nguvu. Basi sasa nenda, uwatangazie watu hawa, na kusema, Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu ishirini na mbili elfu wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi. BWANA akamwambia Gideoni; Hata sasa watu hawa ni wengi mno. Basi akawaleta watu chini majini. BWANA akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa. Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji. BWANA akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu nyumbani kwake.
**MB** Rafiki yangu, mara kwa mara tumapopigana na adui yetu shatani tunafikia uwezo na nguvu tulizo nazo. Hatupaswi kujifikiria sisi na uwezo wetu, tunapaswa kumtegemea Mungu. Yeye ni mwenye nguvu kuliko miungu mingine. Tukimtegemea tutashia.

Picha ya kumi na sita: Gideoni na Askari wake waizingira kambi ya Waminidani

Picha ya kumi na sita: Gideoni na Askari wake waizingira kambi ya Waminidani

Waamuzi 17:16-25

Basi wale watu mia tatu wakachukua vyakula vyao mikononi mwao, na tarumbeta zao. Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia adui zako katika mikono yako. Bwana akamwambia Gideoni asogee katika kambai ya Wamidiani (maana Wamidiani walipiga kambi zao karibu na makambi ya Israeli. Basi Gideoni akasikia mtu mmoja akamsimulia mwenzake yuu ya ndoto yake, akasema, Habari hii haikosi kuwa upanga wa Gideoni, mwana wa Yoashi, mtu wa Israeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote katika mkono wake. Wamidiani waliposikia ndoto hiyo waliogopa sana. Lakini Gideoni aliposikia habari ya ile ndoto, akasujudu; akarudi katika jeshi la Israeli akasema, Inukeni, kwa maana BWANA amelitia jeshi la Midiani mikononi mwenu. Kisha akawapanga wale watu mia tatu wawe vikosi vitatu, akatia tarumbeta katika mikono ya watu wote, na mitungi isiyo na maji, na mienge ndani ya hiyo mitungi. Akawaambia, Nitazameni, mkafanye kama nifanyavyo mimi; angalieni, nitakapofika mwisho wa kambi, itakuwa, nifanyavyo mimi nanyi fanyeni vivyo hivyo. Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote walio pamoja nami, basi ninyi nanyi zipigeni tarumbeta pande zote za kambi, mkaseme, Kwa BWANA, na kwa Gideoni. Basi Gideoni, na wale watu mia waliokuwa pamoja naye, wakafika mwisho wa kambi, wakazipiga hizo tarumbeta, wakaivunja vipande vipande ile mitungi iliyokuwa mikononi mwao. Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kuume ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa BWANA na wa Gideoni. Wakasimama kila mtu mahali pake kuizunguka kambi pande zote; jeshi lote wakakimbia; nao wakapiga kelele, wakawakimbiza. Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia.
**MB** Rafiki yangu, Tunaweza kumtumaini Mungu ili atusaidie. Hatupaswi kuogopa maadui zetu. Nilazima tumfikirie Mungu kwasababu yeye ni mwenye nguvu. Mungu atatusaidia ilikuweze kuishi kama anavyo penda.

Picha ya kumi na saba: Samsoni Alimuwa Simba

Picha ya kumi na saba: Samsoni Alimuwa Simba

Waamuzi 13:1 - 14:19

Gideoni akawaongoza Israeli kwa miaka arobaini. Lakini baada ya kufa kwake Gideoni Waisraeli waligeuka na kufanya yalio maovu mbele za Mungu. Hivyo Mungu akaruhusu Wafilisti wawatawale Israeli. Lakini Mungu hakuwaacha Israeli. Mungu akamuandaa mtu mishi wake aliye itwa Samsoni ili awekiongozi wa Israeli na kuwasaidia na utawala wa Wafilisti. Samsoni alipo zaliwa wazazi wake walimtoa kwa Bwana. Samsoni aliweka nadhili kwa Mungu, kwakuonye kwamba likuwa emejitoa kwa Mungu kweli kweli. Samsoni aliacha nywele za bila kukata. Samsoni hakula nyama, wala kunywa maziwa. Na hii ilionyesha kwamba likuwa anaishi kwa kumtegemea Mungu tu. Na Roho yenye guvu kutoka kwa Mungu iliingia kwa Samsoni na kwasababu ya Roho hiyo Samsoni alikuwa na nguvu nyingi sana. Na nguvu hizo zingeweza kuwasaidia Israeli. Lakini Samsoni hakumtii Mungu wakati wote, wakati mwingine alifanya kama alivyo penda. Siku moja Samsoni akaenda Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Kisha akaenda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe. Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasimjua Mungu? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana. Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakaenda Timna, ilikufanya harusi wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na sehemu ili palikuwa na simba akamngurumia Samsoni. Roho ya BWANA ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua yule simba kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake.
**MB** Rafiki unaye nisikiliza, Mungu alimpa Samsoni nguvu za kumuwa simba. Na Samsoni alijua kwamba Mungu anaweza kumsaidia kumuwa sima. Na angeweza kuwasaidia Israeli pia. Samsoni alikuwa na nguvu nyingi sana zilizo toka kwa Mungu, lakini mke wake hakumjua Mungu.

Picha ya kumi na nane: Samsoni na Mbweha wenye moto

Picha ya kumi na nane: Samsoni na Mbweha wenye moto

Waamuzi 15:1-17

Samsoni alipomuoa mwanamke wa wafilisti, lakini wafilisti hawa kumpenda Samsoni walimudhi kila wakati. Mwisho Samsoni aliamua kurudi kwa wazazi wake na akamuacha mke wake kwa nyumbani kwa wazi wake. Baada ya muda Samsoni aliamu kurudi kwa wakwe, alipofika nyumba kwa mkwe kwake akataka kuingia ndani ya chumbani cha mke wake. Lakini baba yake mwanamke akamkataza akisema, Hakika mimi nalidhani ya kuwa umemchukia kabisa; basi nalimpa rafiki yako. Samsoni aliposikia hayo alikasirika sana. Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa vienge vya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia kienge kati ya kila mikia miwili. Alipokwisha kuviwasha moto vile vienge, akawaachia mbweha kati ya ngano ya Wafilisti, akayateketeza matuta, na ngano, hata na mashamba ya mizeituni. Ndipo Wafilisti wakasema, Ni nani aliyetenda hivi? Wakasema, Ni huyo Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake. Basi Wafilisti wa mfuata Samsoni ili wampige, lakini Samson akawapiga na kuwauwa Wafiliti elfu moja.
**MB ** Rafiki yangu, Mungu alimpa Samsoni nguvu nyingi iliawasaide Israeli, lakini Samsoni hakumtii Mungu sana. Endelea kusikiliza kwa makini nawe utajua ni kwanini tunasema kwama Samsoni hakumtii Mungu.

Picha ya kumi na tisa: Wafilisti walinyoa nywele za Samsoni

Picha ya kumi na tisa: Wafilisti walinyoa nywele za Samsoni

Waamuzi 16:4-22

Samsoni alikuwa kiongozi wa Israeli kwa miaka ishirini. Ingawa alikuwa na nguvu nyingi, lakini alifanya mambo mengine yasio mpendaza Mungu. Ikawa baada ya hayo Samsoni mwona mwanamke mwingine jina lake akiitwa Delila na Samsoni akampenda akampenda. Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, Delila wakamwambia, Mbembeleze mumeo, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha nyingi. Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali uniambie asili ya nguvu zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe. Samsoni akamwambia, Wakinifunga kwa kamba mbichi saba ambazo hazijakauka bado, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamletea kamba mbichi saba zisizokauka, naye akamfunga nazo. Na yule mwanamke alikuwa na watu katika chumba cha ndani, wakimwotea. Basi akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Ndipo akazikata zile kamba kama vile uzi wa pamba ukatwavyo ukiguswa na moto. Basi hiyo asili ya nguvu zake haikujulikana. Delila akamwambia Samsoni, Tazama, umenidhihaki, na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia Wakinifunga tu kwa kamba mpya ambazo hazi jatumika, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Basi Delila akatwaa kamba mpya akamfunga nazo, akamwambia, Wafilisti wanakujia, Samsoni. Na wale wenye kuotea walikuwa katika chumba cha ndani. Naye akazikata, akazitupa kutoka mikononi mwake kama uzi. Delila akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo. Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung'oa ule msumari, na ule mtande. Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi. Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku sasa hivi , maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; nguvu zake zikamtoka. Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha. Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.

Picha ya ishirini: Samsoni Aliwaangamiza Wafilisti

Picha ya ishirini: Samsoni Aliwaangamiza Wafilisti

Waamuzi 16:23-31

Wafilisti walifurahi sana kwasababu waliweza kumkamata Samsoni. Wafilisti wakafanya sherehe kwa kukamatwa kwa Samsoni. Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake, na alijua kwamba nguvu za zitarudi. Na Samsoni hakuweza kuona kwasababu Wafilisti walimtoa macho yake. Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee "Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili." Na wakati huo Wafilisti wengi walikusanyika katika jengo moja ili kufanya sherehe. Samsoni akazishika nguzo mbili za ile nyumba moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto, naye akazitikisha kwa nguvu. Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.
**MB** Rafiki yangu, kabla ya kuzaliwa kwake Samsoni, alikuwa amechaguliwa na Mungu kufanya kazi maalum. Mungu alimpa nguvu nyingi iliaweze kuwa saidia Israeli. Baada ya Samsoni kukamatwa na kufungwa na Wafilisti, Samsoni alimkumbuka Mungu. Samsoni akamuomba Mungu amsamehe na mpenguvu. Mungu akampa Samsoni nguvu, naye akawauwa Wafilisti wengi siku hiyo. Mungu anampango kwa ajili ya maisha yetu na anamipango maalum kwa ajili yetu, hivyo basi tumtii walatusi muasi Mungu.

Picha ya ishirini na moja: Yesu Awafukuza Pepo Wabaya

Picha ya ishirini na moja: Yesu Awafukuza Pepo Wabaya

Luka 8:26-39

Sasa umesikia mambo mengi kuhusu viongozi wa Israeli na jinsi Mungu alivyo wasidia kupata ushindi. Miaka mingi iliyo pita Mungu alimtuma mwanawe Yesu ili awaokoe watu wote. Yesu aliishi katika nchi ya Israeli. Naye alituonye sisi jinsi ya kuishi kwa kumpendeza Mungu. Yesu alimpendeza Mungu kila wakati. Yesu alikuwa na nguvu za kumshinda Shetani. Siku moja Yesu alikutana na mtu mmoja mbaye alikuwa na pepo wengi. Alikuwa mtu aliye shangaza watu, akuvaa nguo na aliishi katika makaburi. Watu wengi walijaribu kumfunga kwa minyororo lakini aliikata na kukimbia. Lakini mtu huyu alipo muona Yesu alimsujudia, na akasema Yesu usinitese. Yesu akaamuru wale pepo wamtoke. Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi la nguruwe, wakaingia ziwani kwa kasi, wakafa maji. Mtu yule akawa mzima. Kamawamiba Yesu, naomba nifuatane nawe, lakini Yesu akamwambia, "Rudi nyumbani kwako, ukahubiri yalivyo makuu Mungu aliyokutendea. Akaenda zake, akihubiri katika mji wote, yalivyo makuu mambo aliyotendewa na Yesu.
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu ni Mwokozi. Ananguvu za kusamehe dhambi. Yesu anataka kusamehe dhambi za kila mtu anaye muomba. Yesu anauwezo wa kubadirisha maisha ya watu. Yesu anapo samehe dhambi zetu maisha yetu yanabarishwa kwa nguvu zake. Hebu tuwaambie wengine kwamba Yesu anaweza kubadirisha maisha yao.

Picha ya ishirini na mbili: Yesu Awafukuza Wafanya Biashara

Picha ya ishirini na mbili: Yesu Awafukuza Wafanya Biashara

Luka 19:45-48

Siku moja Yesu alienda Hekaluni. Hekalu ilikuwa ni nyumba ya kufanyia Ibada. Ndani ya Hekalu aliwaona watu wakifanya biashara na wengine wakibadiridha fedha na kujipatia faida. Yesu alipo waona aliuzunika sana. Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara na wale walio badirisha fedha. Yesu akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
**MB**Rafiki mpendwa, Yesu ni Mtakatifu. Yeye hana dhambi. Wala waliofanya biashara katika hakalu walikuwa ni wao, na Yesu alijua mioyo yao. Hakupendezwa na maisha yao. Yesu tu ndiye anaye weza kubadirisha maisha ya watu ili waishi kwa kumpendeza Mungu.

Picha ya ishirini na tatu: Yesu alifufuka baada ya kufa

Picha ya ishirini na tatu: Yesu alifufuka baada ya kufa

Luka 24:46-48

Viongozi wa Wayahudi hawakuwami kwamba Yesu ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mwokozi wa ulimwengu. Hawakutaka Yesu awemfalme. Hivyo waka mpeleka Yesu mbele ya balaza na ili kumuliza mwaswali. Na wote wakasema asulubiwe. Hivyo Yesu akasulubiwa msalabani na akafa akazikwa katika kaburi. Lakini Yesu hakukaa katika lile kaburi bali alifufuka siku ya tatu. Yesu yu hai sasa. Yesu alimshinda Shetani, na alishinda dhambi na mauti. Baada ya kufufuka Yesu akawatokea wanafunzi wake. Aliongea nao, alikula nao. Kabla ajapaa kwenda mbinguni aliwambia wanafunzi wake, "enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata mwisho wa nchi"
**MB** Rafiki mpendwa, Nguvu za Yesu zina nguvu kuliko za Shetani. Yesu alipokufa na kufufuka, alizivunja nguvu za Shetani. Na wote wanomfuata Yesu atawapa uzima wa milele. Na nguvu zake zitatuwezesha tumshinde shetani. Pia Yesu anataka sisi tuwafanya mataifa yote wawe wanafunzi wake.

Picha ya ishirini na nne: Askari wa Mungu

Picha ya ishirini na nne: Askari wa Mungu

Wafilipi 6:10-18

Tumesikia uwezo mkuu alionao Mungu na jinsi alivyo wasaidia wana wa Israeli. Lakini inakuwaje kuhusu sisi? Mungu atatusaidiaje? Neno lake Mungu linatukumbusha kwamba nguvu zetu hazina uwezo wa kumshinda adui yetu Shetani. Lakini kama tukimuomba Yesu aondoe dhambi zetu na kukaandani yetu, Yeye atafanya hivyo na nguvu zake zitatusidhia kila siku. Wakati mwingine tunajikuta tukijarivu kutumia nguvu zetu kuwashinda wachawi na watu wabaya. Lakini tukumbuke kwamba sisi wenyewe hatu wezi. Tukumbuke kwamba Shetani anatumia uongo. Yatupasa sisi tuva ukweli kama siraha. Neno la Mungu linasema, "Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama Basi simameni, hali mmejifunga kweli..." Kweli ndiyo siraha yetu. Pia tuwambie wenginde habari za Yesu. Tukiacha kufanya hivi, Shetani atajaribu kutushawishi tumuacha Mungu. Sisi ni askari wa Mungu tunapaswa kuwa na imani. Neno la Mungu linasema " Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Imani ni kama ngao kwetu, tunaweza kuizuia mishare ya shetani. Yesu alichukua dhambi zetu naye akatupa uzima wa milele na uzima tulio nao ni ulinzi wetu.
**MB** Rafaki mpendwa, Nilazima tutumie Neno la Mungu. Tunaweza kutimia Neno la Mungu ili kumshinda Shetani. Na kila wakati tukumbuke kumuomba Mungu. Tunaweza kuomba kwa ajili ya maitaji yetu, na tumuombe ili atulinde. Kama tukivaa siraha za Mungu tutaweza kuwa washindi kila siku.

Verwante informatie

Vrij te downloaden - Download Bijbelverhalen in audio formaat en Bijbellessen in duizenden talen, afbeeldingen, scripts en andere verwante materialen die geschikt zijn voor evangelisatie en gemeenteopbouw.

De 'Kijk, Luister & Leef' audio-visuele productie - Deze set bestaat uit 8 programma's met telkens 24 afbeeldingen die uitstekend gebruikt kunnen worden voor systematische evangelisatie en christelijk onderwijs. Deze serie omvat studies van het Oude Testament, Bijbelkarakters, het leven van Jezus en de vroege gemeente. Het is beschikbaar in honderden talen.

Hoe audio-visuele materialen van GRN te gebruiken? - 1: Het evangelie op een eenvoudige manier delen met de ander - In dit artikel kunt u lezen op welke verschillende manieren u de audio-visuele materialen van GRN kunt gebruiken binnen uw bediening.

Hoe audio-visuele materialen van GRN te gebruiken? - 2: Verdieping - In dit artikel kunt u lezen hoe mensen leren uit verhalen en waarom er niet veel commentaar aan de verhalen wordt toegevoegd.

De GRN-audiobibliotheek - Evangelisatiemateriaal en basisbijbelonderricht, aangepast aan de behoeften en de cultuur van het volk, in verschillende stijlen en formaten.

Copyright and Licensing - GRN shares it's audio, video and written scripts under Creative Commons

Creating DVDs using the GRN Slide show Videos - How to burn DVDs for specific people groups you are trying to reach

Choosing the right audio or video format - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?