unfoldingWord 42 - Yesu Anarudi Mbinguni

unfoldingWord 42 - Yesu Anarudi Mbinguni

रुपरेषा: Matthew 28:16-20; Mark 16:12-20; Luke 24:13-53; John 20:19-23; Acts 1:1-11

स्क्रिप्ट क्रमांक: 1242

इंग्रजी: Swahili

प्रेक्षक: General

उद्देश: Evangelism; Teaching

Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture

स्थिती: Approved

स्क्रिप्ट हे इतर भाषांमध्ये भाषांतर आणि रेकॉर्डिंगसाठी मूलभूत मार्गदर्शक तत्त्वे आहेत. प्रत्येक भिन्न संस्कृती आणि भाषेसाठी त्यांना समजण्यायोग्य आणि संबंधित बनविण्यासाठी ते आवश्यकतेनुसार स्वीकारले जावे. वापरलेल्या काही संज्ञा आणि संकल्पनांना अधिक स्पष्टीकरणाची आवश्यकता असू शकते किंवा अगदी बदलली किंवा पूर्णपणे वगळली जाऊ शकते.

स्क्रिप्ट मजकूर

Siku ile Yesu alipofufuka, wanafunzi wake wawili walikuwa wanaenda mji jirani. Wakiendelea kutembea, walizungumza habari zilizotokea kumuhusu Yesu. Walitumaini kuwa alikuwa Masihi, lakini aliuawa. Wanawake waliwaambia yu hai anaishi tena. Nao hawakujua cha kuamini.

Yesu aliwakaribia na akaanza kutembea nao, lakini hawakumtambua. Aliwauliza juu ya mazungumzo yao, nao wakamueleza maajabu yote yaliyo tokea kumuhusu Yesu kwa siku chache zilizopita. Kwani walidhani wanaongea na mgeni asiyejua habari zilizotokea katika Yerusalemu.

Ndipo Yesu akawaelezea jinsi neno la Mungu linavyo sema kumuhusu Masihi. Aliwakumbusha manabii walivyosema, kwamba Masihi atateswa na kuuawa, na atafufuka tena siku ya tatu. Nao walipofika katika mji waliokuwa wamepanga kufikia hawa wanaume wawili, ilikuwa imekaribia jioni.

Hawa wanaume wawili walimkaribisha Yesu akae nao, naye akafanya hivyo. Walipokuwa tayari kula chakula cha jioni, Yesu alichukua kipande cha mkate, alimshukuru Mungu kwa mkate huo, akaumega. Ghafla, wakamtambua kuwa ni Yesu. Lakini wakati huo huo, Yesu akatoweka eneo hilo.

Hawa wanaume wawili waka ambiana, "Yule alikuwa ni Yesu! Ndiyo maana mioyo yetu ilikuwa inaungua wakati akielezea neno la Mungu kwetu." Punde, walirudi Yerusalemu. Nao walipofika, waliwaambia wanafunzi, "Yesu yu hai! tumemuona."

Wakati wanafunzi wanaendelea kuongea, Yesu alijitokeza katikati yao kwenye kile chumba na kusema, "Amani iwe kwenu!" Wanafunzi walidhani kuwa ni mzimu, lakini Yesu akawaambia, "Mbona mnaogopa na kuwa na mashaka? Angalieni mikono yangu na miguu. Mizimu haina mwili kama mimi." Kuwahakikishia kuwa Yeye si mzimu, aliwaomba chakula. Walimpa kipande cha samaki kilichopikwa, naye akala.

Yesu alisema, "Niliwaambia kila kitu kilicho andikwa katika neno la Mungu kunihusu mimi ni lazima kitimie." Ndipo alipofungua akili zao ili waweze kulielewa neno la Mungu. Akasema, "Iliandikwa muda mrefu uliopita yakuwa Masihi atateswa, atakufa na kufufuka kwa wafu siku ya tatu."

Iliandikwa pia katika maandiko kwamba wanafunzi, wangu watatangaza kwa kila mtu katika makundi, kwamba lazima watubu ili wapate msamaha wa dhambi zao. Nao watafanya hivyo kuanzia Yerusalem, nao wataenda kwa watu wote mahali pote. Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.

Ndani ya siku arobaini zilizofuata, Yesu aliwatokea wanafunzi wake mara kwa mara. Wakati mwingine aliwatokea watu zaidi ya 500 kwa wakati mmoja! aliwadhibitishia wanafunzi wake kwa njia nyingi kuwa Yeye yu hai, na aliwafundisha kuhusu ufalme wa Mungu.

Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, mkiwafundisha kuyatii yote niliyowaamuru. Kumbukeni kuwa nitakuwa pamoja nanyi siku zote."

Siku arobaini baada ya Yesu kufufuka kwa wafu, aliwaambia wanafunzi wake, "Kaeni Yerusalemu mpaka hapo Baba yangu atakapo wapa nguvu, pale Roho Mtakatifu atakapowajilia ninyi. Kisha Yesu akaenda mbinguni, nayo mawingu yakamfunika akatoweka kwao. Yesu alikaa mkono wa kuume wa Mungu kutawala vitu vyote.

संबंधित माहिती

Free downloads - Here you can find all the main GRN message scripts in several languages, plus pictures and other related materials, available for download.

The GRN Audio Library - Evangelistic and basic Bible teaching material appropriate to the people's need and culture in a variety of styles and formats.

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares its audio, video and written scripts under Creative Commons