ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha pili: Watu wenye nguvu ya Mungu
Тойм: Jacob, Joseph, Moses. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.
Скриптийн дугаар: 419
Хэл: Swahili: Tanzania
Сэдэв: Sin and Satan (Deliverance, Judgement, Sin, disobedience); Christ (Jesus, Our Substitute, Sacrifice / Atonement); Eternal life (Salvation); Character of God (Nature, character of God, Word of God (the Bible)); Living as a Christian (Obedience, No other gods, idols, Forgiveness, Faith, trust, believe in Jesus); Bible timeline (Law of God, Gospel, Good News); Problems (Problems, troubles, worries)
Үзэгчид: General
Зорилго: Teaching
Features: Monolog; Bible Stories; Paraphrase Scripture
Статус: Approved
Скрипт нь бусад хэл рүү орчуулах, бичих үндсэн заавар юм. Тэдгээрийг өөр өөр соёл, хэл бүрт ойлгомжтой, хамааралтай болгохын тулд шаардлагатай бол тохируулсан байх ёстой. Ашигласан зарим нэр томьёо, ухагдахууныг илүү тайлбарлах шаардлагатай эсвэл бүр орлуулах эсвэл бүрмөсөн орхиж болно.
Скрипт Текст
Utangulizi
Katika kaseti hii tutajifunza habari za watu wa Mungu mwenye nguvu. Angalia katika kitabu chako chako. Unaposikia sauti hii ___________ ufungue picha inayofuata. Sasa ufungue katika picha ya kwanza kisha tutaanza.
Picha ya kwanza: Yakobo mdanganyifu
Mwanzo 25:20-34, 27:1-29
Ibrahimu alikuwa ni mtu aliye mtii Mungu sana. Ibrahimu aliacha nchi yake na kwenda katika nchi aliyo ambiwa na Mungu aende, na nchi hiyo iliitwa Kanaani. Mungu alimpa Ibrahimu ahadi ya kwamba uzao wake utaongezeka. Isaka alikuwa mtoto wa Ibrahimu. Ibrahimu alikuwa mzee sana alipo mzaa Isaka. Na Isaka alimuoa msichana aliyeitwa Rebeka. Isaka na Rebeka waliishi kwa miaka mingi bila kupata mtoto. Na Isaka alimuomba Mungu ali apate mtoto. Na Mungu akamsikia na kumjibu, na mkewe Isaka yaani Rebeka akapata mimba. Na wakati wa kuzaa ulipo karibia, Rebeka alihisi watoto wawili walikuwa wakigombana ndani ya tumbo lake. Mungu akamwambia Rebeka kuwa alikuwa na watoto wawili wa kiume. Na wote wawili watuwa mataifa makubwa. Na mdogo atamtawala mkubwa. Mtoto wa kwanza kuzaliwa aliitwa Esau. Esau alipokuwa mtu mzima alifanya kazi ya kuwinda wanyama. Esau akufikiri sana kuhusu Mungu. Kama kawaida ya watoto wa kwanza, Esau alitarajia kupata urifi kutoka kwa baba yake, napia angekuwa kiongozi wa familia. Lakini Mungu alisema mdogo ndiye atakaye kuwa mtawala. Na yule mdogo aliitwa Yakobo. Yakobo hakuwa muwindaji. Yakobo alikuwa ni mtu mkimya na aliye penda kufanya kazi karibu na baba yake. Yakobo alijaribu kumpenza Mungu. Na alijua Mungu angemfanya awe taifa kubwa. Baba yao aliye itwa Isaka, yeye alitaka kumbariki Esau, kwasababu Esau alikuwa mtoto wa kwanza. Siku moja Esau alitoka kuwinda na hakufanikiwa kupata kitu. Na alipo rudi nyumba alikuwa amechoka sana na njaa ilikuwa inamuuma sana na Yakobo alikuwa amepika chakula. Esau akaja kutoka nyikani Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Yakobo akamwambia, niapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
**BM** Yakobo alifikiri kwamba alitumia njia nzuri ya kupata urithi, lakini hakujua kwamba njia aliyotumia ingeweza kumfanya yeye na Esau kuwa maadui. Yakobo hakumtegemea Mungu katika jambo hilo. Mungu alitaka kutimiza ahadi yake. Rafiki mpendwa Mungu anatimiza ahadi zake. Tumwamini yeye na kumtegemea Yeye. Yatupasa tumsubiri Mungu na mapenzi yake.
Picha ya pili: Ndoto ya Yakobo
Mwanzo 28:10-22
Esau alikasilika sana kwasababu alikosa urithi wake. Esau alimchukia sana Yakobo, na alifanya mpango wa kumuua Yakobo. Isaka ambaye ni baba alipo karibia kufa, Rebeka alisikia kuhusu mpango wa Esau wa kumuua Yakobo. Hivyo Rebeka akamwambia Yakobo aondoke nyumbani asije akauwawa na ndugu yake. Hivyo Yakobo akakimbilia nchi iliyo itwa Padan-aramu mahali ambapo mjomba wake aliye itwa Labani aliishi uko. Na Yakobo aliopokuwa nasafiri kwena kwa mjomba wake alifika mahali fulani akalala usingizi kwasababu alikuwa amechoka sana. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.Yakobo alishangaa sana. Yakobo akaweka ahadi akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.
**MB** Rafiki mpendwa, Yakobo alijaribu kufanya mibango yake, tu yaani kumlazi misha Mungu ambariki. Yakobo alitumia udanganyifu ilikupata urithi . Mungu alijua kwamba Yakobo alikuwa mdanganyifu. Lakini Mungu alimpenda na alitaka kumbadirika.
Picha ya tatu: Yakobo na Labani
Mwanzo 29:1 - 31:55
Yakobo aliendelea na safari yake ya kwenda Padan-aramu. Alipofika Padan-aramu mjomba wake Labani alifurahi sana na alimkaribisha kwa furaha. Labani alikuwa na binti wawili, mmoja aliitwa Lea na mwingine Raheli. Lea alikuwa mkubwa na Raheli alikuwa mdogo. Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri wa uso. Yakobo alimpenda Raheli na alitaka amuoe. Yakobo akamwambia Labani juu ya jambo hilo. Yakobo akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda. Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake. Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake. Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa; timiza siku zake saba, nasi tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine. Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe.
**BM** Yakobo alikaa kwa Labani miaka mingi akifanya kazi. Tunaona kwamba Yakobo alijifunza mambo mbengi alipokuwa kwa Labani. Alijifunza kuwa mvumilivu na aliona ubaya wa uongo. Mungu alimsaidia Yakobo. Na Yakobo alijifunza kumuomba Mungu kumtegemea Yeye.
Picha ya nne: Yakobo akutana na Mungu
Mwanzo 32:1-32
Baada ya miaka mingi Yakobo kufanya kazi kwa Labani, Yakobo alikuwa na watoto wengi na watumishi wengi. Mungu akamwambia Yakobo kwamba wakati wake wa kurudi katika nchi ya baba yake umefika. Basi Yakobo akaondoka, akapandisha wanawe na wakeze juu ya ngamia. Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata. Lakini alipokaribia katika nchi ya Kanaani Yakobo alianza kuogopa kwasababu alijua Esau anataka kumuua. Yakobo hakumtegemea Mungu kama angeweza kumlinda. Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na watumishi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. Akawatwaa, akawavusha mto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo. Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda. Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko. Yakobo alijua kuwa mtu yule alikuwa malaika wa Mungu. Yakobo akapata baraka na akawa baba wa taifa kubwa.
**BM** Rafiki mpendwa, Tunapo jalibu kufuata njia zetu wenyewe, tujue kuwa tunapingana na mipango ya Mungu. Ni lazima tumwamini Mungu na kumtegemea kwa kila jambo.
Picha ya tano: Ndoto ya Yusufu
Mwanzo 37:1-12
Mungu alibadilisha jina la Yakobo. Mungu akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila utaitwa Israeli. Israeli alikuwa na wana kumi na mbili, na mtoto aliyempenda sana aliitwa Yusufu. Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu kaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.
**MB** Yusufu alijua kwamba Mungu anampango katika maisha yake. Yusufu alionyesha moyo wa kumtii Mungu na kumpenda. Rafiki mpendwa, Mungu anampango kwa maisha yetu. Inatupasa kumpenda na kumtii kwa kila kitu kama livyo fanya Yusufu. Ndupo tutakapo ona Mungu akitumia maisha yetu.
Picha ya sita: Yusufu aliuzwa kama mtumwa
Mwanzo 37:12-36
Ndugu zake wakaenda kuchunga kondoo za baba yao huko Shekemu. Israeli akamwambia Yusufu, Njoo, nikutume kwa kaka zako. Akamwambia, Enenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akaenda mpaka bonde la Hebroni, akafika Shekemu. Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika shimo mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Reubeni amabaye ni mkubwa kwao akasikia akamwokoa katika mikono yao, akasema, Tusimwue. Reubeni akawaambia, Msimwage damu ya ndugu yetu ; mtupeni katika shimo hii, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake. Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, wakamtwaa wakamtupa katika shimo; na hilo shimo lilikuwa tupu, hamna maji. Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu katika shimo, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri. Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na uichovya kanzu katika damu. Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. Basi baba yao akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. Lakini ndugu zake Yusufu hawakusahau vile walivyo mfanyia mdogo wao, hawakuwa na amani mioyoni mwao.
**MB** Rafiki mpendwa, habari hizi za Yusufu zinatukumbusha mateso ya Yesu. Yesu alikuja kuishi haba duniani kati ya ndugu zake, lakini walimkana na walimuua. Yesu alikufa ilikulipa deni yetu ya dhambi, ilitupate uzima wa milele.
Picha ya saba: Yususfu akawa mtumwa uko Misri
Mwanzo 39:1-20
Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. BWANA akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri. Bwana wake akaona ya kwamba BWANA yu pamoja naye, na ya kuwa BWANA anafanikisha mambo yote mkononi mwake. Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake. Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa BWANA ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba. Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu. Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri. Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani afanye kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje. Ikawa alipoona ya kwamba amemwachilia nguo yake mkononi mwake, naye amekimbia nje, Basi akaiweka ile nguo kwake hata bwana wake aje nyumbani. Naye akamwambia, Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia aliingia ndani humu ilialale nami. Ikawa nilipopaza sauti yangu, nikalia, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje. Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka. Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani.
**MB** Rafiki mpendwa, jambo hili lilikuwa gumu sana kwa Yusufu. Yusufu alipatwa na mateso mengi sana, lakini tusisahau kwamba Mungu alikuwa pamoja naye. Pingi tunaweza kupatwa na mahangaiko kama liyokuwa nayo Yusufu. Nilazi tumtegemee Mungu. Yusufu alijua kwamba Mungu yupo pamoja naye.
Picha ya nane: Yusufu gerezani
Mwanzo 39:20 - 40:24
Yusufu alipokuwa gerezani aliendelea kumtegemea Mungu. Mkuu wa gereza alipoona uaminifu wa Yusufu, akamuweka Yusufu awemsimamiza wa wafungwa wote. Nayote aliyo yasimamia Yusufu alifanikiwa kwasababu Mungu alikuwa pamoja naye. Ikawa, baada ya mambo hayo, mtu aliyefanya kazi ya kutengeneze vinywaji vya mfalme wa Misri, na mtu aliyefanya kazi ya kuoka mikate, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri. Farao akawakasirikia akawafunga katika gereza alilofungwa Yusufu. Siku moja Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, Waliwatumishi wa mfalme wakamwambia Yusufu, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri ndoto ni kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie. Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu. Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva. Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake. Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake. Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu. Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu. Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu. Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako.
**MB** Mambo yote yakatokea kama alivyo sema Yusufu. Baada ya siku tatu yule mweshaji akarudi katika kazi yake na yule muokaji akauwawa. Rafiki mpendwa, tunaona kwama Mungu alikuwa pamoja na Yusufu na kumuongoza katika kila jambo. Neno la Mungu lina sema hivi "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake" (Warumi 8:28)
Picha ya tisa: Ndoto ya mfalme
Mwanzo 41:1-45
Baada ya miaka miwili kupita. Falao mfalme wa Misri aliota ndoto. Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu. Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo. Basi mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao akisema, tulipofungwa gerezani palikuwa na kijana; Mwebrania aliyeitwa Yusufu, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake. Ndipo Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao. Farao akamwambia Yusufu, nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri. Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani. Farao akamwambia Yusufu juu ya ndoto yake mwanzo hadi mwisho. Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja. Na wale ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa. Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri. Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana. Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa. Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote. Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu alimuongoza Yusufu katika kila jambo, ikawaalikuwa katika kifungo lakini Mungu hakumwacha. Yusufu akuogopa kusema yaleambayo Mungu alimuonyesha. Sisi pia yatupasa tutambue kwamba Mungu anatujari nayeye ni mtawala wa vitu vyote. Tunapojiona kwamba tupo katika mateso, tusiache kusema yale ambayo Mungu ametupa katika Neno lake.
Picha ya kumi: Yusufu atawala Misri
Mwanzo 42:1-38
Watoto wa Israeli yaani ndugu zake na Yusufu waliokaa katika nchi ya kanaani walikuwa hawana chakula. Kwahivyo Israeli akawatuma watoto wake wande mpaka nchi ya Misri ili kununua chakula. Lakini mdogo wao aliye itwa Benjamini alibaki nyumbani. Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake. Yusufu akawaona nduguze, akawatambua, lakini alijifanya kama hawajui. Akasema nao kwa maneno makali, akawaambia, Mmetoka wapi ninyi? Wakasema. Tumetoka nchi ya Kanaani, ili tununue chakula. Yusufu akawatambua ndugu zake, bali wao hawakumtambua yeye. Yusufu akazikumbuka zile ndoto alizowaotea. Akawaambia, Wapelelezi ninyi, mmekuja ili mwuone utupu wa nchi. Wakamwambia, Hasha, bwana, watumwa wako tumekuja ili tununue chakula. Sisi sote ni wana wa mtu mmoja tu watu wa kweli sisi; watumwa wako si wapelelezi. Akawaambia, Sivyo, mmekuja ili mpeleleze nchi. Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu dugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko. Yusufu akawaambia, Ndivyo nilivyowaambia, nikisema, Wapelelezi ninyi. Mtajulikana kwa njia hii; hamtoki hapa, asipokuja huku huyo ndugu yenu mdogo. Mpelekeni mmoja wenu, aende akamlete ndugu yenu, na ninyi mtafungwa, hata maneno yenu yahakikishwe, kama mna kweli ninyi; ikiwa sivyo, basi tutajua ninyi ni wapelelezi. Akawatia wote gerezani siku tatu. Yusufu akawaambia siku ya tatu, awapa ilimkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala amtakufa. Ndivyo walivyofanya. Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosa ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia kwa hiyo shida hii imetupata. Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, msimkose kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo damu yake inatakwa tena. Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alikuwapo mkalimani kati yao. Akajitenga nao akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao. Yusufu akaamuru kuvijaza vyombo vyao nafaka, na kumrudishia kila mtu fedha yake katika gunia lake, na kuwapa chakula cha njiani. Navyo ndivyo walivyofanyiwa. Wakaweka nafaka yao juu ya punda zao, wakatoka huko. Mmoja wao alipofungua gunia lake ili ampe punda wake chakula katika nyumba ya wageni, aliiona fedha yake; kumbe! Iko kinywani mwa gunia lake. Akawaambia nduguze, Fedha yangu imerudishwa, angalia, imo humo guniani mwangu. Mioyo yao ikazimia, wakageukiana wakitetemeka, wakasema, N'nini hii Mungu aliyotutendea? Wakaja kwa Yakobo, baba yao, katika nchi ya Kanaani, wakampasha habari za yote yaliyowapata, wakisema, Mtu yule aliye bwana wa nchi alisema nasi kwa maneno makali, akatufanya tu wapelelezi wa nchi. Tukamwambia, Tu watu wa kweli sisi, wala si wapelelezi. Sisi tu ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu. Mmoja hayuko, na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo katika nchi ya Kanaani. Yule mtu, bwana wa nchi, akatuambia, Kwa njia hii nitawajua kama ninyi ni watu wa kweli; ndugu yenu mmoja mwacheni huku kwangu, kachukueni nafaka kwa njaa ya nyumba zenu, mwende zenu. Mkaniletee ndugu yenu mdogo; ndipo nitakapojua kama ninyi si wapelelezi, bali ni watu wa kweli; basi nitawarudishia ndugu yenu, nanyi mtafanya biashara katika nchi hii. Ikawa walipomimina magunia yao, kumbe! Bahasha ya fedha ya kila mtu imo katika gunia lake. Nao walipoziona bahasha za fedha zao, wao na baba yao waliogopa. Yakobo baba yao akawaambia, Mmeniondolea watoto wangu; Yusufu hayuko, wala Simeoni hayuko, na Benyamini mnataka kumchukua naye; mambo hayo yote yamenipata mimi.
**MB** Rafiki mpendwa, Tunapokosana na ndugu zetu au wagu wengine, nivizuri kama tukiwaomba msamaha kwani bila kufanya hivyo dhambi hiyo itaendelea kukua. Sisi sote tumemkosea Mungu tunahiji kumuomba msamaha kwa ajili ya dhambi zetu naye atatusamehe. Kwasababu Yesu alikufa msalabani ilitusamehewe naye atatupa furaha.
Picha ya kumi na moja: Yusufu ajitambulisha kwa ndugu zake
Mwanza 43:1 - 45:11
Njaa ikawa nzito katika nchi. Ikawa walipokwisha kula nafaka waliyoileta kutoka Misri, baba yao akawaambia, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo. Yuda akamwambia akisema, Yule mtu alituagizia sana akisema, Hamtaniona uso wangu, msipomleta ndygu yenu pamoja nanyi. Basi baba yao akawaruhusu wande pambo ja Benyamini. Na walipo fika nchi ya Misri wakasisimama mbele ya Yusufu. Na Yusufu akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mamake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu. Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo. Akanawa uso, akatoka, akajizuia, akasema, Leteni chakula. Wakamwandalia yeye peke yake, na wao peke yao, na wale Wamisri waliokula pamoja naye peke yao; maana Wamisri hawawezi kula pamoja na Waebrania, kwa kuwa ni chukizo kwa Wamisri. Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao. Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafanya furaha pamoja naye. Akamwamuru yule msimamizi wa nyumba yake akisema, Jaza magunia ya watu hawa chakula kwa kadiri wawezavyo kuchukua, utie na fedha ya kila mtu kinywani mwa gunia lake. Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu. Asubuhi kulipopambazuka, hao watu wakapewa ruhusa, wao na punda zao. Na walipotoka mjini, wala hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema? Je! Kikombe hiki, sicho anyweacho bwana wangu? Naye hufanya uaguzi kwa hicho. Mmefanya vibaya kwa kufanya hivi. Akawafuata, akawapata, na kuwaambia maneno hayo. Wakamwambia, Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, umekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu? Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu. Akasema, Basi na iwe hivyo kama mlivyosema, Mtu atakayeonekana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu, na ninyi mtakuwa hamna hatia. Wakafanya haraka, wakashusha kila mtu gunia lake, na kufungua kila mtu gunia lake. Naye akatafuta, akaanza kwa mkubwa na kuisha kwa mdogo. Kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini. Wakararua nguo zao, wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini. Akaja Yuda na ndugu zake nyumbani kwa Yusufu, naye mwenyewe alikuwamo, nao wakamwangukia kifudifudi. Na Yusufu alifanya hivyo kwa kuwajali kama tabia zao zilikuwa zimebadilika. Hapo Yusufu akajitambulisha kwa, akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake. Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha za watu.
**MB** Rafiki mpendwa, wakahi huu ulikuwa mgumu kwa ndugu zake Yusufu. Mungu waliwapa shida na majaribu mbali mbali ili kubadirisha maisha ya ndugu zake Yusufu. Mungu anaweza kutumia mateso na majaribu ili kutufundisha.
Picha ya kumi na mbili: Israeli na Yusufu wakutana tena Misri
Mwanzo 45:25 - 50:26
Wakatoka Misri, wakafika nchi ya Kanaani kwa Yakobo, baba yao. Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadiki. Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka. Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla sijafa. Akasafiri Israeli, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. kasema, Mimi hapa. Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kuenda mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. Mimi itaenda pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. Israeli akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye. Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, baba yake, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kizima. Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai. Israeli akakaa katika nchi ya Misri, katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali humo, wakaongezeka na kuzidi sana. Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako hawezi; akawachukua wanawe wawili, Manase na Efraimu, ali awabarikia. Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza. Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase. Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake. Baba yake akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa. Akawabariki siku ile akasema, Katika ninyi Waisraeli watabariki.
**MB** Tunapo tafakari habari hizi za Yusufu, tutambue kwamba Yusufu alikuwa mwaminifu kwa Mungu hata lipokuwa na matatizo makubwa. Na Mungu alikuwa pamoja naye. Yusufu alimpenda Mungu na Mungu alimsaidia. Rafimi mpendwa, Unapokuwa na matatizo makubwa ujihadhali usimsahau Mungu. Uamini kwamba Mungu atakusaidia na uwemwaminifu kwa Mungu yeye atakuwa pamoja nawe. Tuwapende watu wa familia zetu, marafiki zetu na watu wengine hatakama ni wabaya. Na tuwaambiea habari za Yesu.
Picha ya kumi na tatu: Mtoto Musa
Kutoka 2:1-10
Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao. Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai. Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi.Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto. Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma mtumishi wake kwenda kukileta. Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. Basi mtimishi akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? Binti Farao akamwambia, Haya! Enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema. Musa alipokuwa mtu mzima alipata elimu. Lakini alijua kwamba yeye si misri yeye ni Mwisraeli.
**MB** Rafiki mpendwa, Huu ulikuwa wakati mgumu sana kwa watu wa Israeli. Hawakuelewa kwanini wanateseka. Lakini Mungu alikuwa na mpango wake. Wakati mwingine hatuwezi kuelewa mpango wa Mungu. Tunafikiri tunateseka tu. Lakini Mungu anatupenda na mipango yake ni mizuri kwetu.
Picha kumi na nne: Musa na kijiti kilicho waka moto
Kutoka 2:11 - 3:12
Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga. Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako? Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana. Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.Waisraeli hawakuelewa kwamba Musa alitaka kuwasaidi. Musa alikaa uko miaka arobaini akichunga kondoo wa mkwe wake maana alioa huko. Siku mojo Musa alipokuwa akichunga kondoo Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Mala akasikia sauti ikisema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. Musa aliogopa sana.
**MB** Mungu akamwambia Musa arudi katika nchi ya Misri kwa watu wa Israeli. Mungu aliyaona mateso ya watu wa Israeli. Mungu akamwambia Musu ande katika nchi ya Misri naye atakuwa pamoja naye. Rafiki mpendwa tunaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu awezi kutusahau kamwe. Mungu anampangwa kwakila mmoja wetu. Mungu anapotuagiza kufanya kitu, Yeye utuambia kwama "Nitakuwa pamoja nawe usiogope"
Picha ya kumi na tano: Musa alirudi Misri
Kutoka 3:11 - 10:29
Musa aliamua kurudi katika nchi ya Misri. Musa alifikiri kwamba mfalme na watu wake hawa awata amini kwamba Musa alitumwa na Mungu. Basi Mungu akamwambia Aruni ambaye ni ndugu yake Musa wende katika nchi ya Misri. Musa na Aruni wakaenda Misri kuongea na mfalme. Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani. Lakini Falao alikataa kuwapa ruhusa. Mungu alipo ona Falao anamoyo mgumu, Mungu akabadiri maji yote ya nchi ya Misri yakawa damu. Na Mungu alipo ona moyo wa Falao bado ni mgumu, Mungu akaleta giza juu ya nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. Lakini yote haya hayakuwapata waisraeli. Falao aliona yote haya na kutambua kwamba Mungu ananguvu, lakini alikataa kuwapa ruhusa waisraeli waende.
**MB** Rafiki mpedwa, Nguvu za Mungu ni kubwa kuliko nguvu za shetani. Mungu ni mwenye nguvu nyingi na anataka kutusaidia inalazima sisi tumsikie na kumtii kupitia Neno lake. Mungu anaweza kutufanya sisi tuwe na nguvu za kumshinda shatani na watu wake.
Picha ya kumi na sita: Pasaka
Kutoka 12:1-36
Mungu alifanya miujiza mingi ilikumfanya Falao atoe fuhusa. Mungu alitaka kudhihilisha nguvu zake kwa kuuwa kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika nchi ya Misri. Mungu kamtuma malaika kwa wana waisraeli na kuwaambia kwamba, wachinje mnyama na waweke kitambaa cha damu ya huo mnyama katika miimo ya milango ya nyumba zao, kwasababu malaika wa Bwana atapita usiku na kuwaua wazaliwa wa kwanza wa binadamu na wa mnyama, na malakia akiona kitambaa hicho hataiangamiza nyumba hiyo. Israeli walifanya kama Bwana alivyo waambia. Malaika wa Bwana akapita usiku huo na kuwaua wazaliwa wakwanza wa mwanadamu na wa mnyama. Hilikuwa pigo kubwa kwa wamisri, kulikuwa na kilio kikubwa sana katika chi ya Misri. Na Waisraeli walikuwa salama, na wakaanza safari yao ya kurudi katika nchi ya kanaani.
**MB** Rafiki mpendwa, miaka mingi iliyo pita Mungu alimtuma Yesu iliafe. Yeye aliitwa mwana kondoo wa Mungu. Yesu alitoa maisha yake ili sisi tupate ukombozi. Ilitubidi sisi tufe kwa ajili ya dhambi zetu lakini Yesu alikuwa badala yetu. Tukimuomba Yesu atusemahe dhambi zetu yeye anaweza kufanya hivyo naye atatupa uzima wa milele. Wana wa Israeli waliweka damu ya mnyama katika miimo ya milango yao walionyesha kwamba alimtii Mungu. Sisi pia inatupasa kuwaonyesha wengine kwamba tunamtii Mungu.
Picha ya kumi na saba: Wana wa Israeli wavuka Bahari ya Shamu
kutoka 13:17 - 14:31
Sasa wisraeli walikuwa huru. Walichukua mali zao pamoja na watoto watu, wakaanza safari ya kwenda katika nchi ya Kanaani. Walipo fika katika bahari ya shamu Bwana akamwambia Musa. Inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu. Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu, bahari ikawa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto. Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawaangamizia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu. Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.
**MB** Rafiki mpendwa, kama tukimpenda Mungu na kumtii Yeye atatulinda katika hatari zote.
Picha ya kumi na nane: Walikula Mana na maji jagwani
Kutoka 16:1 - 17:7
Wana wa Israeli hawakuwa na chakula cha aliposafiri katika jangwa. Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung'unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote. Ndipo BWANA akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo. Kisha itakuwa siku ya sita, ya kwamba watayaandaa hayo watakayoleta ndani, nayo yatakuwa ni mara mbili kuliko wayaokotayo Musa na Haruni wakawaambia wana wote wa Israeli, Jioni ndipo mtakapojua ya kuwa BWANA amewaleta kutoka nchi ya Misri; na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa BWANA; kwa kuwa yeye asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia BWANA; na sisi tu nani, hata mkatunung'unikia? Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo BWANA atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa BWANA asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia yeye; na sisi tu nani? Manung'uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya BWANA. Ikawa wakati wa jioni, wakakaribia, kituo; na Bwana akawanyeshea mvua ya mikate iliyo itwa mikate ya Mana. Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakaokota wengine zaidi, wengine kupungua. Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa. Musa akawaambia, Mtu awaye yote asikisaze hata asubuhi. Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana. Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake. Isipokuwa siku ya sabato. Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione. BWANA akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini? Wana wa Israeli wakaendelea kusafiri wakafika sehemu kame isiyo na maji, wakamwambia Musa, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu BWANA? Bwana akamwambia Musa tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utaupiga mwamba, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. Na maji yakatoka wakanywa wao na watoto wao pamoja na wamyama wao.
Picha ya kumi na tisa: Amri za Mungu
Kutoka 19:1 - 20:17
Wana wa Israeli waliondele na safari yao na baada ya muda walifika mlima sinai. Hapo Mungu akaongea na Musa pamoja na wana wa Israeli. Mungu akashuka kutoka katika lile wingi ili aongee na watu wake. (SE) Watu waliogo kwasababu waliziona nguvu za Mungu. Musa akapanda juu ya mlima ili uongea na Mungu. Mungu akawapa wana wa Israeli amri na Musa akaziandika katika jiwe. Kisha Musa akashuka kutoka mlimani na kuwambiaa watu yale Mungu aliyo mwagiza. Na haya ndiyo maagizo yenyewe.
Mungu akanena maneno haya yote akasema,
"Mimi ni BWANA, Mungu wako, Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Usijifanyie sanamu ya kuchonga.
Usilitaje bure jina la BWANA.
Siku sita fanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA.
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Usizini.
Usiibe.
Usimshuhudie jirani yako uongo.
Usiitamani mali jirani yako, wala cho chote alicho nacho jirani yako."
**MB** Rafiki mpendwa, Hujume huu uliyo toka kwa Mungu ni wakweli. Waisraeli walipata kufahamu mambo yapi wayafanye na mambo yapi wasi yafanye. Huu ni jumbe mzuri kwetu pia. Ikiusikia na kutii Mungu atapendezwa nasi.
Picha ya ishirini: Nyoka wa shaba
Hesabu 21:4-9
Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi. Watu wa Israeli walipona kwa kumtazama nyoka wa shaba. Sisi tunapawa kumwendea Yesu naye atatupa uzima wa milele. Tuweke imani yetu katika Yesu tu.
**MB** Rafiki mpendwa Neno la Mungu linana sema "mshahara wa dhambi ni mauti" hii inamaana wametengwa na Mungu milele. Yesu alipokuja na kufa msalabani, alilipa adhabu ya dhambi zetu. Watu wote wakiweka imani yao kwa Yesu, Yesu atawasamehe na kuwapa uzima wa milele.
Picha ya ishirini na moja: Kiongozi mkuu kuliko Musa
Yohana 6:1-58
Waisraeli walifiki kwamba Musa tu ndiye aliye kuwa kiongozi mkuu. Walikumbuka miujiza mingi aliyotendeka kupitia Musa. Walikumbu jinsi alivyo waongoza kutoka katika nchi ya kanaani. Walikumbu jinzi alivyo piga mwamba na maji yakatoka. Walikumbu hata mikate ya mana waliyo kula kule jangwani. Lakini Mungu alimtuma kiongozi mwingine ambaye alikuwa mkuu kuliko Musa na uweza wake ulikuwa na nguvu. Jina lake aliitwa Yesu. Yesu alifanya miujiza mingi sana ili kuwaonyesha watu kwamba yeye alikuwa mwana wa Mungu. Siku moja Yesu alipokuwa akiwafundisha watu, watu hao walikuwa na maitaji ya chakula walikuwa ni watu wengi zaidi ya elfu tano. Yesu akawauliza wanafunzi wake tutowapi chakula cha kuwalicha watu wote hawa? Mwanafunzi moja akamwambia Yesu, kuna kijana hapa ambaye anauza mikate. Yesu akasema mwitani. Yesu akaichukua ilemikate michache na samaki wawili akavibariki, chakula kikawa kingi sana. Kila mtu alikula na kuza. Watu wote wakashangaa kwa uweza wake. **MB** Rafiki mpendwa, Kupitia muujia huo Yesu aliwafundisha kwamba wasitegemee kupata vyakula tu kani vitu hivyo havi dumu. Lakini kama watu wakimpenda Yesu na kutii mafundisho yake, Yeye atawapa uzima wa milele.
Picha ya ishirini na mbili: Yesu aliongoea na Musa
Luka 9:28-36
Musa liwafundisha Waisraeli mambo mangi sana kusu Mungu, na vile Mungu anavyo takawao waishi. Baada ya Musa kufa watu wange walikuwa wanampenda, walitaka awafundishe habari za Mungu na kuwapa maagizo ya Mungu. Na palikuwa na nabii mwingine aliye itwa Eliya. Manabii alisema kwamba siku moja Mungu atamtuma mtu ambaye atawasaidia waisraeli Yesu ndiye mtu aliye ahidiwa na manabii. Yesu alijua manabii wote. Siku moja Yesu aliwachukua Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba. Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta. Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufa kwake Yesu. Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye. Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye, Petro alimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui asemalo. Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo. Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye. Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lo lote katika hayo waliyoyaona. Hii ilidhihirisha kwamba Yesu ndiye mwokozi aliye ahidiwa miaka mingi iliyo pita.
**MB** Rafiki mpendwa, Musa na Eliya walikuwa manabii wenye uwezo sana lakini Yesu yeye ni mkuu zaidi. Yesu ni mwana wa Mungu, tumsikilize yeye.
Picha ya ishirini na tatu: Yesu alikufa kwa ajili yetu
Yohana 3:14-16
Yesu alipokuwa duniani alifanya miujiza mingi na watu wangine walita wamfanye mfalme. Walifiki kwamba ndiye mtu aliye ahidiwa kwamba atakuja kuwasaidi. Lakini watu wengine walimkana. Mwishowe waka jadiliana juu ya kuuwa. Yesu alipokufa msalabani, hakufa kwasababu alifanya kosa, La Yesu alikufa kwa ajili ya ulimwengu wote. Yesu anauwezo wa kutupa uzima wa milele. Wana Israeli walimzama nyoka wa shaba aliye wekwa na Mungu ili wapone. Sisi tumtazame Yesu anye atatuokoa.
**MB** Rafiki mpendwa, Ilitupasa sisi tufe kwa ajili ya dhambi zetu, lakini Yesu alifanya hivyo kwa ajili ya dhambi zetu . Tukitaka uzima wa milele, tumuendee Yesu naye atatupa.
Picha ya ishirini na saba: Yesu yuhai leo
Matendo 1:6-11
Mwili wa Yesu uliwekwa kaburini, Lakini baada ya siku tatu akafufu, Yesu yuhai leo anaishi sasa. Baada ya kufuka kwake watu wengi waliongea naye. Baada ya siku arobaini Yesu alipaa kwenda mbinguni kama unavyo ona katika picha. Yesu anaishi leo. Musa laikuwa nabii mzuri wa Mungu, lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Yeye ni mkuu sana kuliko Musa naye alikuja kuokoa watu wote. Siku moja Yesu atarudi tena. Atawachukua watu wote walio mwamini na kwenda nao mbinguni.
**MB** Rafiki mpendwa, Je, upotayari kwenda na Yesu? Hanaweza kuja! Biblia inasema " ukimwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako utaokoka"