unfoldingWord 06 - Mungu anamjalia Isaka
개요: Genesis 24:1-25:26
스크립트 번호: 1206
언어: Swahili
청중: General
장르: Bible Stories & Teac
목적: Evangelism; Teaching
성경 인용: Paraphrase
지위: Approved
이 스크립트는 다른 언어로 번역 및 녹음을위한 기본 지침입니다. 그것은 그것이 사용되는 각 영역에 맞게 다른 문화와 언어로 조정되어야 합니다. 사용되는 몇 가지 용어와 개념은 다른 문화에서는 다듬어지거나 생략해야 할 수도 있습니다.
스크립트 텍스트
Wakati Ibrahimu alipokuwa mzee sana, mtoto wake wa kiume, Isaka alikuwa amekuwa mtu mzima. Ibrahimu alimtuma mmoja wa watumishi wake kwenda katika nchi walioishi ndugu zake na Ibrahimu ili kumtafutia mke kwa ajili ya mtoto wake, Isaka.
Baada ya safari ndefu ya kwenda walikoishi ndugu zake na Ibrahimu, Mungu alimwongoza mtumishi wa Ibrahimu kwa Rebeka. Rebeka alikuwa ni mjukuu wa kaka yake na Ibrahimu.
Rebeka alikubali kuiacha familia yake na kwenda pamoja na yule mtumishi wa Ibrahimu hadi nyumbani kwa Isaka. Na mara baada ya kufika huko, Isaka alimuoa Rebeka.
Baada ya muda mrefu, Ibrahimu alifariki na ahadi zote alizokuwa ameahidiwa na Mungu katika agano zilihamishwa kwa Isaka, mwanae. Mungu alikuwa ameahidi kuwa Ibrahimu atakuwa na uzao mwingi usiohesabika, lakini Rebeka, mkewe Isaka, hakujaliwa kuwa na watoto.
Isaka alimwombea Rebeka. Mungu alimjibu na Rebeka akabeba mimba ya mapacha. Wale watoto wawili walikuwa wakishindana tumboni mwa Rebeka. Rebeka akamwuliza Mungu juu ya hicho kilichokuwa kikitokea tumboni mwake.
Mungu akamwambia Rebeka, " Mataifa mawili yatatokea kutokana na watoto wawili wa kiume walio tumboni mwako. Na kutakuwa na ushindani kati yao, na mtoto mkubwa atamtumikia mdogo."
Na siku ile walipozaliwa watoto wa Rebeka, mtoto mkubwa alitoka akiwa mwekundu na mwenye nywele nyingi katika mwili wake; walimwita jina lake, Esau. Mtoto mdogo alizaliwa huku akiwa amekishikilia kisigino cha Esau, naye walimwita jina lake, Yakobo.