ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha nne: Mtumishi wa Mungu

ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha nne: Mtumishi wa Mungu

개요: Ruth, Samuel, David, Elijah. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.

스크립트 번호: 421

언어: Swahili: Tanzania

주제: Sin and Satan (Sin, disobedience); Christ (Birth of Christ); Eternal life (Salvation); Character of God (Nature, character of God, Word of God (the Bible), Power of God / Jesus); Living as a Christian (Obedience, Faith, trust, believe in Jesus, Children of God, Humility); Bible timeline (Prophecy, fulfillment of, Gospel, Good News, People of God)

청중: General

목적: Teaching

Features: Monolog; Bible Stories; Extensive Scripture

지위: Approved

이 스크립트는 다른 언어로 번역 및 녹음을위한 기본 지침입니다. 그것은 그것이 사용되는 각 영역에 맞게 다른 문화와 언어로 조정되어야 합니다. 사용되는 몇 가지 용어와 개념은 다른 문화에서는 다듬어지거나 생략해야 할 수도 있습니다.

스크립트 텍스트

Utangulizi

Utangulizi

Waisraeli ndilo taifa lilo changuliwa na Mungu. Wakati mwingine walimuasi Mungu, na hivyo walipatwa na matatizo makubwa kwasababu ya kumuacha Mungu. Lakini kulikuwa na watu ambao walimpenda Mungu na kumfuata. Na watu hao waliitwa watumishi wa Mungu. Katika kitabu hichi cha njano au "yellow book", Bibilia inatuambia juu ya watumishi wa Mungu. Kaseti hii imetolewe na Language Recordings International. Sasa chukua kitabu cha njano na ufungue katika picha ya kwanza . Unaposikia sauti hii ___________ ufungue picha inayofuata.

Picha ya kwaza: Familia ilikimbia njaa

Picha ya kwaza: Familia ilikimbia njaa

Ruthu 1:6-22

Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Wakakaa huko yapata miaka kumi. Baada ya miaka mingi, Maloni na Kilioni wote wawili wakafa; na huyo mwanamke yaani Naomi akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.. Basi Naomi akaona kwamba Mungu alikuwa maemucha kwasababu ya mambo yaliompata katika nyumba yake.
**MB** Rafiki yangu, Wakati mwingine mambo mabaya kama haya yanaweza kutupata. Na nirahisi kufikiri kwamba Mungu ametuacha. Tukumbuke kwamba Mungu anatupenda na anatujali. Anatumia wakati mbaya ilitufundisha, pia anatumia wati mzuri kutufundisha. Mungu anaweza kutumia hata wakati mbaya ilikutufundisha, ili sisi tuone uweza wake.

Picha ya pili: Naomi na Ruthu warudi Israeli

Picha ya pili: Naomi na Ruthu warudi Israeli

Ruthu 1:6-22

Naomi alisikia ya kwamba Bwana amewajilia watu wake na kuwapa mvua na chakula. Basi Naomi akapanga safari ya kurudi Israeli. Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; Bwana na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia. Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutaenda pamoja nawe kwa watu wako. Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, rudini; kwanini kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? Enyi wanangu, mrudi; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa BWANA umeniacha. Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe akarudi nyumbani kwa mama yeke, lakini Ruthu akaambatana naye. Naye akasema, Tazama, Orpa amerudi kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urudi wewe umfuate mwenzako. Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, alimuacha aende naye. Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu, Rafiki zake Naomi walihuzunika sana kwasbabu mume wa Naomi na watoto wake alikufa. Basi Naomi na Ruthu wakakaa Bethlehemu.

Picha ya tatu: Ruthu akiwa katika mavuno

Picha ya tatu: Ruthu akiwa katika mavuno

Ruthu 2:1-23

Basi huyo Naomi alikuwa na ndugu wa mumewe, mtu mkuu mwenye mali, na jina lake aliitwa Boazi. Naomi na Ruthu hawakuwa na shamba. Naye Ruthu Mmoabi akamwambia Naomi, Sasa niende katika mashamba, niokote masazo ya mavuno yaliyo sazwa na watu. Naomi akamwambia, Haya, mwanangu, nenda. Basi akaenda, akaokota masazo shambani nyuma ya wavunaji; na bahati nzuri akafika sehemu ya shamba liliyokuwa mali yake huyo Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki. Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu kuwasalimu wavunaji, Kisha Boazi akamwuliza mtumishi aliyewasimamia wavunaji akisema, na huyu je! Ni msichana wa nani? Yule msimamizi aliyewasimamia wavunaji akajibu, akasema, Ni yule msichana Mmoabi aliyerudi pamoja na Naomi, kutoka nchi ya Moabu; naye alituomba akisema, tafadhali niruhusu kuokota masazo, basi tukamruhsu aokote masazo. Basi Boazi akamwambia Ruthu, Mwanangu, sikiliza; wewe usiende kuokota masazo katika shamba lingine, wala usiondoke hapa, lakini ukae papa hapa karibu na wasichana wangu. Na muweze kuvuna mavuno katika shama hili. Basi Ruthu alipo rudi nyumbani Naomi akamwuliza, Je! Umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Naye akasema, yule mtu niliyefanya kazi ya kuotoka masazo katika shamba lake, jina lake anaitwa Boazi. Ruthu akamhadithia Naomi mambo yote ambayo Boazi alimtendea. Naomi akasema na abarikiwe mtu huyo. Naomi alifurahi sana akasema, Mungu ni mwema amemtuma Boazi iliatusaidie. Ruthu akaendelea kufanya kazi ya kuvuna mavuno katika shamba la Boazi.

Picha ya nne: Ruthu na Boazi wakia katika sakafu ya kupuria nafaka

Picha ya nne: Ruthu na Boazi wakia katika sakafu ya kupuria nafaka

Ruthu 3:1-18

Basi wakati wa mavuno ulipo pita, Naomi akamwambia Ruthu akisema, ni vizuri nikutafutie mume ili uwe na furaha katika maisha yako. Boazi ni mtu mwema sana na ni jaama yetu wakaribu. Basi kwakuwa Naomi alijua utamadumi wa Waisraeli, kwamba mwanamke akifiwa anaweza kurithiwa na ndugu yake. Bazi Naomi akamfundisha Ruthu jinsi ya kufanya ili ambape Boazi. Naomi akasema, Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye sehemu ya kupuria nafaka, walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa. Na utakapofika wakati wakulala, utapaangalia mahali alalapo, nawe uingie, uifunue miguu yake ujilaze hapo; na yeye atakuambia utakalofanya. Basi Ruthu akamwambia, Hayo yote unenayo mimi nitayafanya. Basi akaenda ; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza. Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo. Na ikawa usiku wa manane Boazi akasituka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake. Akasema, Ama! "Ni nani wewe?" Akamjibu, "Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu." Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonyesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, na umeamua kuolewa nami. Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa aana mji wote pia wa watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema. Tena ndiyo kweli ya kuwa mimi ni wa jamaa yako aliye karibu; lakini kuna mtu wa jamaa aliye karibu kuliko mimi. Ambaye angeweza kukuoa Wewe ungoje usiku huu; kisha, subuhi, kama akikubali kufanya ipasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia ipasavyo jamaa. Bazi ulale wewe hata asubuhi. Basi Ruthu akalala miguuni pa Boazi mpaka asubuhi.

Picha ya tano: Boazi na Wazee wa Bethelehemu

Picha ya tano: Boazi na Wazee wa Bethelehemu

Ruthu 4:1-22

Asubuhi yake Boazi akaenda mpaka langoni pa mji, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi. Kisha akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, Ninyi nanyi, ketini hapa. Wakaketi. Kisha akamwambia yule jamaa, Huyu Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi aliyokuwa nayo ndugu yetu, Elimeleki; nami ilikuwa nia yangu nikujulishe wewe, na kukuambia, Uinunue mbele ya hawa waliopo na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya, uikomboe; lakini kama hutaikomboa, uniambie ili nijue mimi; kwa kuwa hakuna mtu wa kuikomboa ila wewe, na kama si wewe ni mimi. Naye akasema, Nitaikomboa mimi. Ndipo Boazi aliposema, Siku ile utakapolinunua shamba mkononi mwa Naomi, unamnunua Ruthu pia, huyu Mmoabi, mkewe marehemu, ili makusudi umwinulie marehemu jina katika urithi wake. Basi yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa. Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadilishana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli. Basi yule jamaa akamwambia Boazi, Wewe ujinunulie mwenyewe. Akavua kiatu chake. Naye Boazi akawaambia wale wazee na watu wote, Leo hivi ninyi ni mashahidi ya kwamba mimi nimenunua yote yaliyokuwa ya Elimeleki, na yote yaliyokuwa ya Kilioni na Maloni, mkononi mwa Naomi. Tena, huyu Ruthu Mmoabi, mkewe Maloni, nimemnunua awe mke wangu, makusudi nipate kumwinulia marehemu jina katika urithi wake, jina lake marehemu lisikatike miongoni mwa ndugu zake, wala langoni pa mji wake; leo hivi ninyi ni mashahidi. Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika sana, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu. Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume. Nao wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

Picha ya Sita: Mariamu na Malaika wa Mungu

Picha ya Sita: Mariamu na Malaika wa Mungu

Luka 1:26-38

Miaka mingi iliyo pita baada ya kizazi cha Ruthu, Mungu alimchagua mwanmke mwingine kwa kazi ya utumishi na jina lake aliitwa Mariamu. Mariamu alikuwa mshichana ambaye hakumjua mwanaume. Naye alikuwa ameposwa na na Yusufu. Na kabla ya kufunga ndoa Malaika kamtokea na kumwambia, "Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema"
**MB** Rafiki mpendwa, Mariamu aliamini kwamba Mungu atafanya kama alivyo sema. Mariamu alimpenda Mungu na alimwamini Mungu. Mariamu akapata mimba kama malaika alivyo sema. Na akamza mtoto na wakamwita jina lake Yesu. Alikuwa mtoto wa Mariamu na Mungu. Yesu alikuwa mtumishi mwema wa Mungu. Yesu alitoa maisha yake kwa ajili ya dhambi zetu.

Picha ya Saba: Hana amuomba Mungu

Picha ya Saba: Hana amuomba Mungu

1 Samweli 1:1-12

Palikuwa na mtu mmoja wa nchi ya Israeli, jina lake aliitwa Elkana. Najina na mke wake aliitwa Hana, lakini Hana hakuwa na watoto. Elikana na Hana walikuwa wakisafiri kwenda Shilo kila mwaka ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu. Hana alikuwa na uzuni sana kwa sababu hakuwa na mtoto. Sikumoja walipo kwenda kuomba. Hana aliinga katika hakalu ilikuomba akamkuta mtumishi wa Mungu najina lake aliiwa Eli. Naye Hana alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana, akasema, "Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso langu na kunipa mimi mtoto wa kiume, nitakupa wewe Bwana ili akutumikie wewe siku zote za maisha yake" Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za BWANA, Eli akamwangalia kinywa chake. Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako. Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA. Usinidhanie kuwa mimi ni mwanamke asiyefaa kitu. Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba. Basi Hana akaenda zake kwa furaha, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena. Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akalala na mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka. Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli.
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu anasikia maombi yetu, na anajua nikitu gani tunacho penda. Nilazima tuwe na subila tunapo kuomba Mungu. Nilazima tuwe na tumaini kwamba yeye atatupa kile tuombacho, kwa wakati wake.

Picha ya nane: Mtoto Samweli katika nyumba ya Mungu

Picha ya nane: Mtoto Samweli katika nyumba ya Mungu

1 Samweli 1:24-28, 2:12-21, 31:1-21

Naye Hana alipokuwa amekwisha kumwachisha maziwa, akampeleaka mtoto Samweli nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo. Hana akamkuta Eli akamuuli je, unanikumbuka? mimi ndimi yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba BWANA anipe mtoto. Nilimuomba Bwana anipe mtoto huyu; BWANA akajibu dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Basi Eli akamfundisha Samweli kazi ya utumishi. Eli alikuwa na wana wawili, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali BWANA, Hivyo dhambi yao wale vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa BWANA; kwa maana hao watu walidharau sadaka ya BWANA. Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana. Basi, mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli. Na neno la BWANA lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu; basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. BWANA akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena. Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. BWANA akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemwita yule mtoto. Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake. BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. BWANA akamwambia Samweli, nitaiangamiza nyumba ya Eli kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia. Naye Samweli akalala hata asubuhi, akaifungua milango ya nyumba ya BWANA. Samweli akaogopa kumjulisha Eli maono hayo. Basi Eli akamwita Samweli, akasema, Samweli, mwanangu. Naye akajibu, Mimi hapa. Akamwuliza, Ni neno gani alilosema nawe? Nakusihi, usinifiche; Basi Samweli akamwambia kila neno, asimfiche lo lote. Samweli akakua, naye BWANA alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini.
**MB** Ni vizuri tumsikilize Mungu kama Samweli alivyo fanya, ni lazima tumtii Mungu. Pia ni vizuri tuwafundishe watoto wetu maneno ya Mungu.

Picha ya tisa: Samweli awaombea Israeli

Picha ya tisa: Samweli awaombea Israeli

1 Samweli 7:2-14

Samweli akawa mtu mzima nae akawa kiongozi mzuri sana. Akamtumika Mungu, akawafundisha watu wa Israeli maneno ya Mungu. Elia akafa na watoto wake wakafa kwa ajili ya dhambi zao (kwamaana Bwana alisema atawaangamiza). Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua sanduku la Mungu kwa muda wa miaka ishirini; na nyumba yote ya Israeli wakamwombolezea BWANA. Basi Samweli akawaambia watu wote wa Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, mkamtumikie Bwana yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti. Ndipo wana wa Israeli wakaiondoa miungu migeni, wakamtumikia BWANA peke yake. Samweli akasema, Wakusanyeni Israeli wote, nami nitawaombea ninyi kwa BWANA. Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za BWANA; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia BWANA dhambi. Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, mashehe wa Wafilisti walipanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti. Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia BWANA, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti. Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia. Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; walakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, (SE) juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli. Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga. Israeli wakapata ushindi mkuu.

Picha ya kumi: Samweli ammiminia Sauli mafuta

Picha ya kumi: Samweli ammiminia Sauli mafuta

1 Samweli 8:1 - 10:1

Samweli alijua kwamba Mungu ni mwenyi nguvu naye ndiye mfalme. Lakini watu wa Israeli walita kuwa na mflame wao. Samweli hakufurahia jambo hilo. Lakini Mungu akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ambayo Bwana alimwambia. Kisha Samweli akawaambai wale watu waliotaka mfalme akisema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa Wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. Naye atawatumikisha ninyi. Hata Samweli alipomwona Sauli, BWANA akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu. Naye Sauli alikuwa kijana mrefu na mwenguvu tena mzuri. Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, BWANA mekutia mafuta uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa na mikono ya adui zao.
**MB** Rafiki mpendwa, Nilazima tuwe waangalifu kwani sisi wenyewe hatuwezi kujiongoza. Tusiache watu wengine watuwale nakututumikisha. Nilazima tuakikishe kwamba Mungu ndiye Mfalme wetu na kiongoiz wetu

Picha kumi na moja: Sauli achana joho la Samweli

Picha kumi na moja: Sauli achana joho la Samweli

1 Samweli 15:1-29

Sauli alikuwa kiongozi mzuri. Sauli aliwasaidia wana wa Israeli walipokuwa wakipigana na Wafilisti. Na Israeli walishinda. Siku moja Mungu akamwambia Samweli akisema, Umwambie Sauli enda akawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala asiwaachilie; bali awaangamize, watu wote, na watoto wote, na ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. Basi Sauli akakusanya majeshi yake, wakaenda kuwapiga Ameleki. Akamkamata mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la BWANA likamjia Samweli, kusema, Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha. Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli. Samweli akamwambia Sauli "Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme." Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema uliko wewe.
**MB** Rafiki yangu, mara kwa mara kunafuata njia zetu na mipango yetu wenyewe na tunamsahau Mungu. Nilazima tuwe wepesi kumtii Mungu, kwani Mungu anapendezwa sana anapo ona sisi tunamtii.

Picha ya kumi na mbili: Yesu akiwa nyumbani mwa Baba

Picha ya kumi na mbili: Yesu akiwa nyumbani mwa Baba

Luka 2:41-50

Miaka mingi baada ya Samweli, Mungu alimtuma mwana wake Yesu Kristo ili aje aishi duniani kama mwana damu. Yesu alikuja kuokoa watu wote. Lakini Yesu akuja kama mtu maarufu. Yesu alizaliwa kimasikini sana. Yesu alikuja kama mtumishi. Yeye alikuwa mtumishi wa Mungu na alikuwa mtumishi wa watu wote. Kila mwaka Waisraeli walikendwa Yelusalemu kusherehekea sikuku ya masaka. Yesu alipofikisha umri wa miaka kumi na mbili mama yake na baba yake, walimchukua Yesu ili kwenda kusherehekea sikuku ya pasaka. Na walipo anza kurudi safari yao ya kuelekea nyumbani hawakumuona Yesu, hivyo iliwabidi warudi hadi Yelusalemu na kumtafuta. Baada ya siku tatu walimkuta hekaruni. Alikuwa maekaa na viongozi wa dini, Yesu alifundisha hao watu habari za Mungu. Watu wote walishanga sana kusikia kijana mdogo akiongea maneno ya Mungu kwa hekima. Wazazi wake walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, "Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni." Akawaambia, "Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?"
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu alipokuwa mtoto mdogo kama Samweli alimtii Baba yake ambaye ni Mungu. Yesu alikuja ili awemtumishi wa Mungu na watu wote. Yesu alimtii Mungu kwa kila jambo. Unakumbuka habari za Samweli, Samweli alisikia sauti ya Mungu na akatii. Pia ukumbe kwamba Sauli hakutii sauti ya Mungu na Mungu akamwacha.

Picha ya kumi na tatu: Daudi Mchungaji wa Kondoo

Picha ya kumi na tatu: Daudi Mchungaji wa Kondoo

1 Samweli 16:1-13, 17:34-35

Mungu alipo mkataa Suli asiwe mfalme. Mungu alimchagua mtu mwingine ambaye aliitwa Daudi. Daudi alikuwa ni kijana aliye mpenda Mungu. Alitaka kumpendaza Mungu kwa yale alio sema na kutenda. Daudi alikuwa akichunga kondoo za baba yake Yese. Daudi alipokuwa akichunga kondoo aliimba nyimbo nzuri za kumsifu Mungu Siku moja Daudi alimuona simba akija kukamata kondoo. Daudi akamuua yule simba. Daudi alikuwa ni kijana mdogo tu, lakini Mungu alimsaidia kumuua simba. Siku nyingine Dubu alikuja ili akamate kondoo. Daudi alimtegemea Mungu iliamsaidie. Na Mungu akamsaidia kumuua yule dubu. Mungu akamwambia Samweli uenda katika nyumba ya Yese mtu wa Bethelehemu nahuko ndiko nitakapo jichagulia mfalme wa Israeli. Basi Samweli akaenda hadi katika nyumba ya Yese. Samweli akamuomba Yese awalete wanawe. Yese akawaita wanawe. Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, bila sha huyu ndiye aliye chakuliwa na Bwana. Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, BWANA hakumchagua huyu. Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala BWANA hakumchagua huyu. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, BWANA hakuwachagua hawa. Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja. Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Huyo ndiye Daudi, naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
**MB** Rafiki mpendwa, Daudi alikuwa mtu mdogo, lakini Mungu alimchagua awe mfalme, kwasababu Daudi alimpenda Mungu na alitaka kumtumikia kwa moyo wake wote.

Picha ya kumi na nne: Daudi na Goliathi

Picha ya kumi na nne: Daudi na Goliathi

1 Samweli 17:1-54

Wakati huo Wafilisti walikusanya majeshi yao kwa vita, nao wakakusanyika ili kupigana na Israeli. Naye Sauli na watu wa Israeli wakakusanyika, nao wakapanga vita juu ya hao Wafilisti. Wafilisti wakasimama juu ya mlima upande huu, na Waisraeli wakasimama juu ya mlima upande wa pili, napo palikuwa na hilo bonde katikati. Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, naye alikuwa murefu sana, mtu aliye zoe vita, naye alikuwa ni mtu shujaa katika jeshi zima la Wafilisti. Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli kila siku akiwaambia, chagueni mtu ambaye ataweza kupigana na mimi na kama akiweza kupigana nami na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu; nami nikimshinda yeye na kumwua, ninyi mtakuwa watumwa wetu. Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane. Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana. Daudi alikuwa kijana mdogo, lakini siku moja baba yake alimtuma Daudi awapelekee kaka zake chakula, kwani kaka zake Daudi walikuwa watu wa vita. Daudi alipofika katika jeshi la Israeli akamsikia yule Mfilisi akiwa tukana Waisraeli. Daudi akasema ni kwa nini mtu huyu ayatukane majeshi ya Mungu aliye hai? Nitakwenda kupigana naye. Ndipo Sauli akamruhusu Daudi akapigane na Goliathi. Daudi hakuogopa kwani alijua Mungu atakuwa pamoja naye. Yule Mfilisti akainuka, akaenda akamkaribia Daudi. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti akamwua. walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake. Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wa yule Mfilisti, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakaogopa sana, wakakimbia.
**MB** Rafiki mpendwa, Daudi hakuogopa alijua kwamba Mungu atamsaidia. Tunapokuwa katika hali hiyo sisi wenyewe tunaogopa na tunafikiri kwamba tutashindwa. Lakini nilazima tumtegemee Mungu, Yeye ni mwenye nguvu naye atatusaidia ili tupate ushindi.

Picha ya kumi na tano: Sauli Ajaribu Kumuua Daudi

Picha ya kumi na tano: Sauli Ajaribu Kumuua Daudi

1 Samweli 18:1 - 23:39

Watu wa Israeli walimpenda sana Daudi. Daudi akawa askari mzuri na kiongozi mwema. Watu wa Israeli wakaimba nyimba za kumsifia Daudi kwa ushindi alio wapatia Israeli. Lakini Sauli alikasirika sana juu ya jambo hilo, naye Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. Na wakati huo Roho wa Mungu alikuwa amemwacha Sauli kwasababu alikuwa amemuasi Mungu, na roho mbaya ikamuingia Sauli. Na Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake. Mbele ya mfalme Sauli. Naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake. Sauli akajaribu kumpiga Daudi hata ukutani kwa mkuki wake, ila Daudi akakwepa, nao huo mkuki akapiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule. Yonathani mwana wa Sauli alikuwa rafiki mkubwa sana wa Daudi. Naye Yonathani alimsaidia Daudi. Hivyo ilimbidi Daudi aondoke nyumbani mwa mfalme. Basi Daudi akaimbia na kwenda kujificha ili Sauli asimpate. Lakini Daudi hakuwa peke yake. Baada ya muda wana ume wa Israeli walienda kukaa naye, kisha Daudi akawa mfalme wa Israeli.
**MB** Rafiki mpendwa, Daudi alijua kwamba Mungu alikua pamoja naye. Daudi alijua kwamba Mungu aliye mrinda na makucha ya simba alipokuwa akichuna kondoo, Huyo Mungu atamlinda katika kila jambo. Ingawa wakati huu ulikua wakati mgumu kwa Daudi, lakini yeye hakuacha kumtegemea Mungu.

Picha ya kumi na sita: Daudi ahurumia maisha ya Sauli

Picha ya kumi na sita: Daudi ahurumia maisha ya Sauli

1 Samweli 26:1-25

Mfalme Sauli aliendelea kumtafuta Daudi kwa miaka mingi. Lakini Mungu alikuwa pamoja na Daudi. Basi Sauli akaondoka, akaenda katika msitu ili amtafute Daudi, naye alikuwa na watu elfu tatu, pamoja naye. Naye Sauli akapiga hema katika kilima cha Hakila, kilichoelekea Yeshimoni, barabarani; lakini Daudi alikuwa akikaa nyikani, akaona ya kwamba Sauli amemfuata mpaka nyikani. Basi Daudi akatuma wapelelezi, akapata habari ya hakika ya kwamba Sauli amefika. Daudi akainuka, akafika mahali pale alipokuwa Sauli; Daudi akapaangalia mahali alipolala Sauli, na Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi lake; naye Sauli alikuwa amelala kati ya magari, na hao watu wamepiga hema zao wakimzunguka. Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hata nchi kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili. Lakini Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize; Si vema kumfanyia hivyo mfalme aliye chaguliwa na Bwana. Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia. Kisha Daudi akaenda ng'ambo ya pili, akasimama juu ya kilima, mbali sana, naye Daudi akawapigia kelele watu wale, na Abneri, mwana wa Neri, akasema, Abneri, hujibu? Ndipo Abneri akajibu, akasema, U nani wewe? Naye Daudi akamwambia Abneri, Wewe si mtu shujaa? Mbona, basi, hukumlinda bwana wako, huyo mfalme? Kwa maana mtu mmoja aliingia ili amwangamize mfalme, bwana wako? Tazameni, liko wapi fumo la mfalme, na gudulia la maji lililokuwa kichwani pake? Naye Sauli akaitambua sauti ya Daudi, akasema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Daudi akasema, Ndiyo, ni sauti yangu, bwana wangu, mfalme. Akasema, Bwana wangu ananiwinda mimi mtumishi wake kwa sababu gani? Nimefanya nini mimi? Ni uovu gani nilio nao mkononi mwangu? Ndipo Sauli akasema, Nimekosa; rudi, Daudi, mwanangu; maana sitakudhuru tena, kwa kuwa maisha yangu yalikuwa na thamani machoni pako leo; angalia, nimetenda upumbavu, nimekosa sana.
**MB** Rafiki unaye nisikiliza, Daudi hakuwa na haja ya kumuua Sauli. Alisema kwamba haita impendeza Mungu. Kweli Daudi alikuwa mtumishi mwema wa Mungu na Mungu alikuwa pamoja naye. Ni vizuri kwetu sisi kama tukichagu akufanya vitu ambayo vina mpendeza Mungu.

Picha ya kumi na saba: Daudi Awa Mfalme

Picha ya kumi na saba: Daudi Awa Mfalme

1 Samweli 31:1-7; 2 Samweli 5:1-16

Sauli alikuwa mfalme wa Israeli lakini Mungu hakuwa pamoja naye. Baada ya miaka mingi kupita Israeli walikuwa na vita na Wafilisti. Sauli na mwanawe Yonathani wali kufa katika vita hivyo. Hivyo Israeli ikawa haina mfalme. Basi watu wakamfanya Daudi awe mfalme wa Israeli yote. Na Dadui alikuwa mfalme mwema. Daudi aliwaombea watu wake kwa Mungu, na aliomba Mungu amlinde. Tunakumba Daudi alikuwa kijana tu aliye chunga kondoo za baba yake, lakini sasa Mungu alimfanya awe mfalme wa Israeli. Daudi alimtii Mungu na alitaka watu wake wamtii Mungu. Daudi alikuwa kiongozi mzuri na Mungu akampa nguvu za kutawala na kuilinda nchi ya Israeli isiingiliwe na maadui.

Picha kumi na nane: Daudi na Bath-sheba

Picha kumi na nane: Daudi na Bath-sheba

2 Samweli 11:1 - 12:20

Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke aliyeitwa Bath-sheba anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye. Wakati huo mume wake Bath-sheba aliyeitwa Uria alikuwa vitani. Basi Daudi akatuma ujumbe kwa amirijeshi mkuu akisema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe. Kisha Daudi akamchukua Bath-sheba awe mke wake. Naye akamzalia mtoto wa kiume. Daudi alifikiri hakuna mtu anaye ona dhambi yake. Lakini Mungu alichukizwa sana na dhambi hile, ndipo Mungu akamtuma nabii aliyeitwa Yonathani aende nyumbani kwa Daudi. Yonathani alipofika kwa Mfalme Daudi, akamwambia Daudi akisema, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nalikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa na mkono wa Sauli; nami nikakupa nyumba ya bwana wako, nikakupa ufalme. Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako. Basi, sasa mabaya hayataondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau. Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa. Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa. Naye Nathani akaondoka kwenda nyumbani kwake. Basi BWANA akampiga yule mtoto ambaye mkewe Uria alimzalia Daudi naye akawa hawezi sana. Basi Daudi akafunga, akaingia ndani kwake, akalala chini usiku kucha. Daudi akamlilia Bwana amsamehe dhambi yake.
**MB** Rafiki mpendwa, Hatuwezi kujificha. Mungu anaona kila mahali naye anajua kila kitu, lakini tukiungama dhambi zetu Yeye atatusamehe. Tunapo kuwa na dhambi tunawapa madui nafasi. Yatupata tuungame dhambi zetu na kutii Neno la Mungu.

Picha ya kumi na Tisa: Nyumba ya Mungu

Picha ya kumi na Tisa: Nyumba ya Mungu

1 Mambo ya Nyakati 22:1-19

Mungu alimsamehe Daudi na dhambi yake. Daudi alikuwa mfalme wa Israeli kwa miaka mingi. Daudi alimpenda Mungu na kumtii. Daudi alitaka kumjengea Mungu nyumba nzuri kwa ajili ya kuabudia. Basi Daudi akafanya mipango mingi inayo usika na ujenze wa nyumba hiyo. Lakini Mungu akamwambia, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu. Lakini mwano Suleman huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu. Basi Daudi akaweka akiba tele kabla hajafa ili mwanawe Suleman awe na hakiba ya kutosha kujenga nyumba Bwana. Suleman alimpokuwa mtu mzima akaanza kuijenga nyuma ya Bwana, naye alikuwa na wafanyakazi wengi. Ilichukua muda wa miaka saba kujenga hiyo nyumba. Nyumba hiyo ilikuwa nyumba nzuri sana na Waisraeli walipenda kwenda katika nyumba hiyo na kuabudu. Rafiki mpendwa, Daudi alikuwa mfalme mzuri sana wa Israeli. Lakni kuna mfalme mwingine ambaye alikuja, naye ni mwenye uweza mkuu kuliko Daudi.

Picha ya Ishirini: Yesu Aingia Yerusalemu

Picha ya Ishirini: Yesu Aingia Yerusalemu

Mathayo 21:1-11

Miaka mingi baada ya mfalme Daudi, Yesu alizaliwa katika Bethelehemu na mwanamke aliye itwa Mariamu. Mariamu alitokana na uzao wa mfalme Daudi. Yesu ni mwana wa Mungu, pia ametokana na uzao wa mfalme Daudi. Yesu aliwafundisha watu habari za Mungu. Yesu alifanya mambo mengi na miujiza mingi ili kuwa onyesha watu kwamba yeye alikuwa mwana wa Mungu. (Mungu alimchagua) Siku moja Yesu alienda Yerusalemu. Na watu wengi walisimama njiani ili wamsalimu. Yesu aliingia Yerusalemu akiwa amepanda punda. Watu wengine waliweka mavazi yao chini ili punda apite juu yake. Na watu wengine walipungia mikono na wengine matawi ya miti wakisema "Osana mwana wa Daudi" Mshukuru Mungu kwasababu Yesu alikuja duniani. Unabii umetimia, uliosema "mfalme amekuja akiwa amepandwa mwana-punda"
**MB** Rafiki yangu, Yesu ndiye mfalme wa Israeli. Pia yeye ni mfalme wa watu wote. Pia Yesu alikuwa mtumishi mwema. Alikuja kuwaokoa watu wote. Yesu ni mfalme lakini yeye hawatumikishi watu, Bali anawapenda watu wote naye anataka kuwasaidia. Je,Yesu ni mfalme wako?

Picha ya ishirini na moja: Ndege ampa chakula Eliya

Picha ya ishirini na moja: Ndege ampa chakula Eliya

1 Wafalme 17:1-6

Baada ya mfalme Daudi na mfalme Suleman kufa. Kulikuwa na wafalme wengi waliotawala Israeli wengine walikuwa wazuri lakini wafalme wengine walikuwa wabaya. Mfalme moja aliyekuwa mbaya aliitwa Ahabu na mkewe aliitwa Yezebeli. Yezebeli hakuwa Muisraeli. Yezebeli aliabudu mwiungu mingine aliyo itwa baali na alitaka watu wote wa Israeli waabudu baali. Mungu alikasirishwa sana. Mungu akamtuma Eliya aende kwa Ahabu. Na aliyekuwa nabii siku hizo. Basi Eliya akaenda kwa Ahabu na kumwambia, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu. Basi toka siku hiyo mvua haikunyesha katika Israeli kwa muda wa miaka mitatu. Na nchi yote ya Israeli ikwa na ukame. Kisha Mungu akamwambia Eliya, Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. Basi kaenda akafanya kama alivyosema BWANA; akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.
**MB** Rafiki mpendwa, Eliya hakuogopa kusema maneno ya Mungu bali alifanya kama Mungu alivyo mwambia, ingawa alijua Ahabu na watu wake wasinge penda kusikia maneno ya Mungu. Eliay alijua umuhimu wa maneno ya Mungu, naye alitaka kumtii Mungu. Rafiki, nivema kama tukiwaambia wengine maneno ya Mungu, tukifanya hivyo itaonyesha kwamba utamtii Mungu.

Picha ya ishirini na mbili: Eliya na Moto wa Mungu

Picha ya ishirini na mbili: Eliya na Moto wa Mungu

1 Wafalme 18:16-46

Katika miaka hiyo mitatu ya ukame, Eliya kaenda kwa mfalme Ahabu kamwambia awakusanye watu wote wa wa Israeli. Basi mfalme akawakusanya watu wote wa Israeli katika mlima wa Karmeli, na wale manabii wa Baali mia nne na hamsini. Basi Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mumkate-kate na kumweka juu ya kuni, wala msitie moto chini; Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu. Basi wale manabii wa Baali wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya. Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na nyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika. Lakini hapakuwa na jibu lolote. Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya BWANA iliyovunjika. Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo. Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni. Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu. Yale maji yakaizunguka madhabahu. Kisha Eliya nabii akakaribia katika madhabahu, akaomba, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu.
**MB** Rafiki mpendwa Eliya alimtumikia Mungu kwa uaminifu ingawa maadui zake walikuwepo. Eliya hakuona haya kumtumikia Mungu. Mungu anataka watumishi waaminifu kama Eliya. Wanaume na wanawake wano mtii Mungu watachekwa na watu . Lakini Mungu atakuwa pamoja nao.

Picha ya ishirini na tau: Eliya Apaa Mbinguni

Picha ya ishirini na tau: Eliya Apaa Mbinguni

1 Wafalme 19:1-21; 1 Wafalme 2:1-14

Kwa miaka mingi Eliya aliwafundisha wana wa Israeli habari za Mungu. Maadui wa Eliya walijaribu sana kumshinda Eliya, lakini Mungu hakumuacha Eliya bali alikuwa pamoja naye. Mungu akamwambia Eliya amtie mafuta Elisha mwana wa Shafati ili awe nabii mahali pako. Mungu akamwambia Eliya kwamba wakati wake wa kunda minguni umekaaribua, na Elisha atanya kazi ya unabii bala yako. Siku moja Eliya na Elisha walikuwa wakitembea, ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli. Elisha alishanga na kuogopa sana alipoyaona hayo. Basi Eliya akapaa kwenda mbinguzi. Na Elisha akalitwaa lile vazi la Eliya, hiyo ikawa ishara kwamba Elisha amekuwa nabii badala ya Eliya.
**MB** Rafiki mpendwa, Haikuwa rahisi kuwa mtumishi wa Mungu siku zile, lakini Eliya na Elisha alimheshimu Mungu na kumtii. Pia alimpenda Mungu na walifanya mambo yanayo mpendenza Mungu. Sisi pia yatupasa tuige mfano wao.

Picha ya ishirini na nne: Eliya pamoja na Yesu na Musa

Picha ya ishirini na nne: Eliya pamoja na Yesu na Musa

Luka 9:28-36

Miaka mingi iliyo pita baada ya Eliya, Mungu alimtuma mwanawe wa pekee Yesu ili aishi hapa tuniani. Yesu aliwaambia watu habari za Mungu, na aliwafundisha watu habari za Mungu. Na baadhi ya Waisraeli walitaka kumuua, kama walivyo taka kumuua Eliya, laini watu wengine walimsikilize Yesu na kumfuata na waliamini yale aliyo wafundisha. Siku moja Yesu aliwachukua wanafunzi wake kwenda mlimani kuomba. Naye Yesu alipokuwa akiomba sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta. Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufa kwake Yesu. Na baada ya muda wakasiuti ya Mungu ikisema," Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye". Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Eliya na Musa walikuwa watumishi walio mpenda Mungu. Baada ya Eliya na Musa kwenda mbinguni waliendelea kumtumikia Mungu. Bado wapo hai ata leo wanamsifu Mungu.
**MB** Rafiki yangu unaye nisikiliza, Je, wewe unampenda Mungu na kutii Neno lake? Je, wewe ni mmoja wa watumishi wa Mungu? Je, wewe umemwamini Yesu na kumpekea? Yesu alikuja kuokoa watu wote. Alikufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi zetu naye amelipa deni ya dhambi zetu. Sasa ni rahisi kuokoka na kuwa watumishi wa Mungu. Na Yesu ametuahidi kuwa pamoja nasi. Tukimwamini na kutii Neno lake tutakapo kufa tutaendelea kumsifu Mungu na kumtumikia huko mbinguni.

관련정보

무료 다운로드 - 여기에서 다운로드 가능한 여러 언어로 된 주요 GRN 메시지 스크립트, 그림 및 기타 관련 자료를 찾을 수 있습니다.

"Look, Listen and Live" 시청각 자료 - 8개 프로그램의 24개 그림은 각각 체계적인 전도와 그리스도 교육에 매우 적합합니다. 이 시리즈는 구약의 등장 인물과 예수님의 삶, 그리고 젊은 교회에 대하여 배울 수 있으며 수백개의 언어로 제공됩니다.

GRN 시청각 자료 활용 하기 -파트1: 복음 공유를 쉽게 - 이 글은 사역에 사용될 수 있는 다양한 GRN 시청각 자료에 대해 소개합니다.

GRN 시청각 자료 활용하기-파트2: 더 많이 배우기 - 이 글은 어떻게 사람들이 이야기로부터 배우는지, 그리고 왜 이야기에 많은 주석이 없는지에 대한 이유에 대해 추가적으로 설명 합니다.

GRN 오디오 도서관 - 전도와 기본 성경 가르침을 위한 자료는 mp3, CD, 카세트 테이프 형태로 사람들의 필요와 문화에 맞추어졌습니다. 녹음은 성경이야기, 전도 메시지, 말씀 읽기, 노래를 포함하여 다양한 스타일로 구성되었습니다.

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares it's audio, video and written scripts under Creative Commons

Creating DVDs using the GRN Slide show Videos - How to burn DVDs for specific people groups you are trying to reach