언어선택

mic

unfoldingWord 23 - Kuzaliwa kwa Yesu

unfoldingWord 23 - Kuzaliwa kwa Yesu

개요: Matthew 1-2; Luke 2

스크립트 번호: 1223

언어: Swahili

청중: General

목적: Evangelism; Teaching

Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture

지위: Approved

이 스크립트는 다른 언어로 번역 및 녹음을위한 기본 지침입니다. 그것은 그것이 사용되는 각 영역에 맞게 다른 문화와 언어로 조정되어야 합니다. 사용되는 몇 가지 용어와 개념은 다른 문화에서는 다듬어지거나 생략해야 할 수도 있습니다.

스크립트 텍스트

Mariamu alikuwa amechumbiwa na mtu mwadilifu aitwaye Yusufu. Yusufu kwasababu ya uhaki hakutaka Mariamu apate aibu kwaajili ya ujauzito ambao haukumhusu hivyo akaanza kutafuta njia akwepe kwa siri. Malaika akamtokea Yusufu katika ndoto.

Ndipo Malaika akamtahadharisha Yusufu kwamba asimwache Mariamu kwasababu mimba hiyo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu hivyo asiwe na wasiwasi. Mtoto atakayezaliwa ni wa kiume ataitwa jina lake Yesu (yaani Yehova huokoa), kwa kuwa atawaokoa watu waondoke dhambini.

Yusufu aliamua kumchukua Mariamu kuwa mkewe; lakini, hawakukaribiana mpaka pale Mariamu atakapomzaa mwana.

Wakati Mariamu alipokaribia kuzaa, ni kipindi kile utawala wa Rumi ulielekeza kila mtu ahesabiwe katika jamii anayotokea. Hapa inabidi sasa Yusufu na Mariamu wasafiri safari ndefu waelekee Bethlehemu tokea Nazareti kwa sababu ndiyo mji wao kwa asali yaani mji wa Daudi.

Baada ya kufika Bethlehemu hapakuwa na mahali ya kujihifadhi. Nafasi waliyopata ni pale mifugo ilihifadhiwa, ndipo mtoto alipozaliwa na mama yake alimlaza kwenye lishio la ng'ombe kwa kuwa hakuna kitanda; jina lake aliitwa Yesu.

Usiku ule ule walikuwepo wachungaji wa maeneo jirani wakilinda mifugo yao. Ghafla waliona malaika akin'gaa mbele yao wakatekewa; Malaika akasema, "msiwe na wasiwasi ninazo habari nzuri. Kristo Bwana amezaliwa Bethlehem!"

Akaongeza; "nendeni kwa mtoto, mtamuona amefungwa nguo akiwa amelazwa kwenye lishio la mifugo." Mawinguni walionekana Malaika, wakitukuza na kuimba Utukufu uko mbinguni kwa Mungu na amani duniani kwa wapendwa."

Wachungaji walifika mahali pale alipokuwa Yesu kama maelekezo ya malaika yalivyokuwa wakiwa wamejawa furaha. Baada ya hapo wakarudi ilipokuwa mifugo yao; wakimtukuza Mungu kwa yale waliyosikia na kuyaona.

Badaye wenye ujuzi tokea mashariki ya mbali wakiongozwa na nyota walifika Bethlehemu na hapo wakatambua ile nyota ilimaanisha Mfalme wa Wayahudi. Hivyo wakasafiri safari ndefu na wakaipata nyumba alimokuwa Yesu akiwa pamoja na wazazi wake.

Na wataalamu hawa walipomuona Yesu na mama yake, wakainama na kumwabudu. Ndipo walimpa Yesu zawadi za gharama kubwa. Wakarudi kwao mashariki.

관련정보

생명의 말씀 - GRN 은 성경에 기반한 구원과 그리스도인의 삶에 대한 수천개의 오디오 복음 메시지를 가지고 있습니다.

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares its audio, video and written scripts under Creative Commons