unfoldingWord 47 - Paulo na Sila wakiwa Filipi

概要: Acts 16:11-40
スクリプト番号: 1247
言語: Swahili
観客: General
目的: Evangelism; Teaching
Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture
状態: Approved
スクリプトは、他の言語への翻訳および録音の基本的なガイドラインです。スクリプトは、それぞれの異なる文化や言語で理解しやすく、関連性のあるものにするために、必要に応じて適応させる必要があります。使用される用語や概念の中には、さらに説明が必要な場合や、完全に置き換えたり省略したりする必要がある場合もあります。
スクリプトテキスト

Sauli alianza kujiita Paulo, kwa jina lake la Kirumi, alipofanya safari katika ufalme wote wa madola ya Kirumi. Paulo na mtu wake wa Karibu aitwaye Sila walienda kuhubiri habari njema kuhusu Yesu katika mji wa Filipi. Walienda nje ya mji, kando ya mto mahali ambapo watu walikutana kusali. Walipokuwa hapo walionana na mwanamke mfanya biashara aliyeitwa Lidia. Alimpenda na alimcha Mungu.

Mungu alimwongoza Lidia kuupokea ujumbe wa Yesu, yeye, wakiwemo watu wa nyumbani mwake, wote walibatizwa. Paulo na Sila walikaa kwake na watu wake, aliwakaribisha nyumbani.

Kulikuwa na mahali ambapo watu walikuwa wakikutana na kusali. Hapo ndipo mahali Paulo na Sila mara nyingi walikutana na watu. Walipokuwa akienda mahali pale kila siku, mwanamke mmoja mwenye umri mdogo kabisa, akiwa mtumwa, na mwenye pepo, aliwafuata. Alikuwa akiwatabiria watu kwa kuongozwa na pepo, kutokana na uwezo kama huo aliwafaidisha waliomtumikisha, kwa kuwapatia fedha nyingi kwa kazi yake ya utambuzi.

Msichana mtumwa alikuwa akipaza sauti kila alipowaona wakitembea, na kusema, "Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye hai." Wanawaelezeeni njia ya kupata wokovu! Alifanya hivyo bila ya kuchoka kiasi cha kumkera Paulo.

Hatimaye siku moja msichana mtumwa alipoanza kupaza sauti, Paulo aligeuka kwake na kumkemea pepo aliyekuwa ndani yake, akisema, "kwa jina la Yesu toka," palepale pepo alimwacha.

Watumikishaji wa msichana walipotambua kuwa bila ya pepo mtumwa wao alikuwa hawezi kuwatabiria watu, walikasirika. Kwa kuwa hangewaingizia kipato cha fedha tena, kwa kulipwa wao ili afanye utabiri kwa watu.

Kwa sababu hiyo Paulo na Sila walipelekwa kwenye vyombo vya dola vya serikali ya Kirumi na Watumikishaji wa msichana mtumwa, watu hawa waliwapiga na kuwatia gerezani.

Paulo na Sila waliwekwa katika chumba cha ndani kabisa sehemu mojawapo ya gereza, kwa usalama wasitoroke na hata kufungwa miguu yao. Usiku wa manane walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu.

Kushtukia, kulitokea tetemeko kubwa lililosababisha milango ya gereza na pingu za minyororo ya wafungwa kufunguka na kuanguka kutoka mikononi.

Askari mlinzi wa wa wafungwa aliamuka, alijawa na hofu kubwa sana baada ya kuona milango ya gereza iko wazi, akifikiri kuwa, wafungwa wote watakuwa wametoroka, alikusudia kujiangamiza. (Alijua serikali ya Kirumi ingemhukumu kifo endapo aliwaachia wafungwa kutoroka). Lakini Paulo alipaza sauti kumkataza "Acha kujiangamiza, sisi sote hatujatoroka.

Mlinzi wa wafungwa alienda kwa Paulo na Sila akitetemeka na kuwauliza, "Nifanye nini nipate kusalimika?" Paulo alimjibu, "mwamini Yesu, Bwana, wewe na watu wa nyumbani mwako mtapata wokovu. Hivyo mlinzi wa wafungwa aliwakaribisha Paulo na Sila nyumbani kwake na kuwaosha majeraha yao. Kila mtu katika nyumba yake alipata kuhubiriwa na Paulo habari njema za Yesu.

Mlinzi wa wafungwa na kila mtu katika nyumba yake walimwamini Yesu na kubatizwa. Mlinzi wa wafungwa aliwahudumia chakula Paulo na Sila na walifurahi pamoja.

Siku iliyofuata, Paulo na Sila waliachiliwa huru kutoka gerezani na waliambiwa kuondoka Filipi na viongozi wa mji. Paulo na Sila walipata nafasi kumtembelea Lidia na wapendwa wengine na ndipo walipoondoka katika mji. Injili ya Yesu iliendelea kuenea na Kanisa liliendelea kukua.

Miji mingi ilifikiwa na Paulo pamoja na viongozi wengine wakristo waliosafiri kwenda katika miji hiyo wakihubiri na kufundisha habari njema za Yesu. Zaidi ya hapo waliandika barua nyingi za kuwatia moyo wakristo makanisani. Baadhi ya barua hizi ni sehemu ya vitabu vya Biblia.