unfoldingWord 50 - Yesu Anarudi

unfoldingWord 50 - Yesu Anarudi

Schema: Matthew 13:24-42; 22:13; 24:14; 28:18; John 4:35; 15:20; 16:33; 1 Thessalonians 4:13-5:11; James 1:12; Revelation 2:10; 20:10; 21-22

Numero di Sceneggiatura: 1250

Lingua: Swahili

Pubblico: General

Scopo: Evangelism; Teaching

Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture

Stato: Approved

Gli script sono linee guida di base per la traduzione e la registrazione in altre lingue. Dovrebbero essere adattati come necessario per renderli comprensibili e pertinenti per ogni diversa cultura e lingua. Alcuni termini e concetti utilizzati potrebbero richiedere ulteriori spiegazioni o addirittura essere sostituiti o omessi completamente.

Testo della Sceneggiatura

Kwa zaidi ya miaka 2,000, zaidi na zaidi watu ulimwenguni kote wamekuwa wakisikia habari njema kuhusu Yesu Masihi. Kanisa limekuwa likikua. Yesu aliahidi angerudi mwisho wa dunia. Ingawa bado hajarudi, ataitimiza ahadi yake.

Wakati tunamsubiri Yesu kurudi, Mungu anataka tuishi maisha ya utakatifu na ya kumweshimu. Tena anatutaka tuwaambie wengine habari za ufalme wake. Wakati Yesu alipokuwa akiishi duniani alisema, "Wanafunzi wangu wataihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu kwa watu wote ulimwenguni na ndipo mwisho utawadia."

Makundi ya watu wengi bado hawajasikia habari za Yesu. Kabla hajarudi mbinguni, Yesu aliwaambia wakristo kuitangaza habari njema kwa watu ambao kamwe hawajasikia. Alisema, "Enendeni na kufanya wanafunzi kwa watu wa makundi yote!" na "Mashamba yamekomaa kwa mavuno!"

Pia Yesu alisema, "Mtumwa si mkuu juu ya bwana wake. Kama ilivyo mamlaka ya dunia hii inavyonichukia mimi, watawatesa na kuwaua kwa sababu yangu. Ingawaje katika dunia hii mtateswa, iweni na ujasiri kwa sababu nimemshinda Shetani, ambaye anatawala dunia hii. Ikiwa mtabaki waaminifu kwangu hadi mwisho, kisha Mungu atawaokoa!"

Yesu aliwaambia wanafunzi wake simlizi juu ya namna itakavyotokea kwa watu wakati dunia itakapokwisha. Alisema, "Mtu alipanda mbegu njema katika shamba lake. Wakati alipokuwa amelala, adui yake alikuja na kupanda mbegu za magugu sambamba na ngano na kisha akaenda zake."

Wakati mimea ilipoota, watumishi wa bwana walisema, 'Bwana, ulipanda mbegu njema katika shamba lile, Je, kwanini kuna magugu ndani yake?' Bwana akajibu, 'Lazima adui ameyapanda.'

Watumishi wakamjibu bwana wao, 'Je, tunaweza kuyang'oa magugu?' Bwana akasema, 'Hapana. Mkifanya hivyo, mtang'oa na ngano pamoja. Subirini hadi mavuno kisha mkusanye magugu katika matita na kuyateketeza kwa moto, bali muilete ngano gharani mwangu.'

Wanafunzi hawakufahamu maana ya simulizi, hivyo walimwomba Yesu awafafanulie. Yesu alisema, "Mtu aliyepanda mbegu njema anawakilisha Masihi. Na shamba linawakilisha ulimwengu. Mbegu njema inawakilisha watu wa ufalme wa Mungu.'"

Magugu yanawakilisha watu wa milki ya mwovu. Adui aliyepanda magugu anamwakilisha Ibilisi. Mavuno yanawakilisha mwisho wa dunia, na wavunaji wanawakilisha Malaika wa Mungu.

Wakati wa mwisho wa dunia, malaika watawakusanya pamoja watu wote walio wa milki ya Ibilisi na kuwatupa katika moto, mahali watakapolia na kusaga meno katika mateso ya kutisha. Kisha wenye haki watang'aa kama jua katika ufalme wa Mungu Baba yao."

Pia Yesu aliwaambia kwamba angerudi duniani kabla ya mwisho wa dunia. Atarudi kwa namna ilie ile alivyoondoka, kwa hali hiyo, atakuwa na mwili na atakuja na mawingu katika anga. Wakati Yesu akirudi, kila mkristo aliye kufa atafufuka kutoka wafu na kukutana naye mawinguni.

Kisha wakristo watakaosalia hai watanyakuliwa juu katika mawingu na kuungana pamoja na wakristo waliofufuka kutoka wafu. Wote watakuwa pamoja na Yesu huko. Baada ya hapo, Yesu atakaa na watu wake katika amani timilifu na umoja wa milele.

Yesu aliahidi kuwapa taji kwa kila mtu amwaminiye yeye. Watakaa na kutawala pamoja na Mungu katika amani timilifu ya milele.

Lakini Mungu atamhukumu kila mmoja ambaye hakumwamini Yesu. Atawatupa wote jehanamu, mahali watakapolia na kusaga meno katika mateso ya milele. Moto usioweza kuzimika utaendelea kuwaunguza, na funza hawatakoma kuwatafuna.

Wakati Yesu akirudi, atamwangamiza kabisa Shetani na ufalme wake. Atamtupa Shetani Jehanamu ambapo atachomwa milele, pamoja na kila mmoja aliyechagua kumfuata yeye badala ya kumtii Mungu.

Kwa sababu Adamu na Eva walimwasi Mungu na kuleta dhambi humu ulimwenguni, Mungu aliilaani na kukusudia kuiangamiza. Lakini kuna siku Mungu ataumba mbingu mpya na nchi mpya itakayokuwa kamilifu.

Yesu na watu wake wataishi katika nchi mpya, na atatawala milele juu ya kila kitu kilichopo. Atafuta kila chozi na hapatakuwa tena na mateso, huzuni, kilio, uovu, maumivu, au kifo. Yesu atatawala katika ufalme wake kwa haki na amani, na atakuwa na watu wake milele.

Informazioni correlate

The GRN Audio Library - Evangelistic and basic Bible teaching material appropriate to the people's need and culture in a variety of styles and formats.

Choosing the audio or video format to download - What audio and video file formats are available from GRN, and which one is best to use?

Copyright and Licensing - GRN shares its audio, video and written scripts under Creative Commons