unfoldingWord 44 - Petro na Yohana Wamponya Ombaomba
Ուրվագիծ: Acts 3-4:22
Սցենարի համարը: 1244
Լեզու: Swahili
Հանդիսատես: General
Ժանր: Bible Stories & Teac
Նպատակը: Evangelism; Teaching
Աստվածաշնչի մեջբերում: Paraphrase
Կարգավիճակ: Approved
Սցենարները հիմնական ուղեցույցներ են այլ լեզուներով թարգմանության և ձայնագրման համար: Դրանք պետք է հարմարեցվեն ըստ անհրաժեշտության, որպեսզի դրանք հասկանալի և համապատասխան լինեն յուրաքանչյուր տարբեր մշակույթի և լեզվի համար: Օգտագործված որոշ տերմիններ և հասկացություններ կարող են ավելի շատ բացատրության կարիք ունենալ կամ նույնիսկ փոխարինվել կամ ամբողջությամբ բաց թողնել:
Սցենարի տեքստ
Siku moja, Petro na Yohana walikuwa wakihudhuria Hekaluni. Na walipokaribia kwenye lango la hekalu, walimwona kiwete aliyeketi langoni na kuomba fedha.
Petro akamtazama yule kiwete na kumwambia, "Sina fedha za kukupa. Japo nitakupa kile nilichonacho. Kwa jina la Yesu Kristo, simama na utembee!"
Mara tu, Mungu akamponya yule kiwete akaamka na akaanza kutembea na kurukaruka hapa na pale na kumsifu Mungu. Watu wote waliokuwa kwenye ua wa Hekalu walishikwa na mshangao mkubwa.
Watu wengi wakakusanyika kwa haraka ili kumwona yule kiwete aliyeponywa. Petro akawaambia, "Kwa nini mnashangazwa na uponyaji ambao mtu huyu ameupata? Uponyaji huu haujafanyika kwa sababu ya wema na nguvu zetu. Bali ni kwa nguvu na imani itokayo kwa Yesu Kristo."
Ninyi ndio mliomshawishi Mtawala kutoka Rumi kumuua Yesu. Mlimuua mwanzilishi wa uzima, lakini Mungu alimfufua katika wafu. Ingawa hamkujua kile mlichokuwa mkikifanya, Mungu alitumia matendo yenu maovu kwa kutimiza unabii wa kwamba Masihi atateswa na kufa. Kwa hiyo mnapaswa kutubuna kurudi kwa Mungu ili msamehewe dhambi zenu.
Viongozi wengi wa Hekalu walisikitishwa sana na yale maneno ya Petro na Yohana. Kwa hiyo wakawakamata na kuwaweka gerezani. Pamoja na hayo, bado watu wengi walimwamini Yesu kwa ujumbe wa Petro, na idadi ya wanaume waliomwamini Yesu siku hiyo walikuwa 5,000.
Siku iliyofuata, viongozi wa hekalu waliwaleta Petro na Yohana kwa kuhani mkuu na mbele ya viongozi wa kidini na kuwauliza, "Ni kwa nguzu gani mlimponya huyu kiwete?"
Petro akawajibu, " Mtu huyu asimamaye mbele yenu, aliponywa kwa nguzu za Yesu. Ambaye nyinyi mlimsulubisha, lakini Mungu alimfufua katika wafu. Hamkumkubali, ila hakuna njia jingine duniani inayoweza kuokoa isipokuwa kwa nguvu za Yesu Kristo!"
Wale viongozi wa dini walipowatazama na kuwasikiliza Petro na Yohana na ujasiri wa hotuba yao, na kuowaona kuwa walikuwa watu wa kawaida na wasio na elimu, walishitushwa. Walikumbuka kuwa walikuwa pamoja na Yesu Kristo. Baada ya kuwatisha waliwaruhusu waende zao.