ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha sita: Yesu Mwalimu na Mponyaji
طرح کلی: From Matthew and Mark. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.
شماره کتاب: 423
زبان: Swahili: Tanzania
موضوع: Sin and Satan (Deliverance, Light/Darkness, Sin, disobedience); Christ (Son of God, Life of Christ, Authority, Jesus, Our Shepherd); Eternal life (Salvation, Broad & Narrow Ways); Character of God (Grace and Mercy, Nature, character of God, Word of God (the Bible), Power of God / Jesus); Living as a Christian (Prayer, petition, Obedience, Forgiveness, Faith, trust, believe in Jesus, Children of God, Assurance, Spiritual Life, Christian values); Bible timeline (End Time, Second Coming, Gospel, Good News); Problems (Evil Spirits, demons, Sickness, Problems, troubles, worries)
مخاطبان: General
سبک و سیاق: Monolog
نوع: Bible Stories & Teac
هدف: Teaching
نقل قول کتاب مقدس: Extensive
وضعیت: Publishable
متن کتاب
Utangulizi
Mfululizo huu wa pichi na kanda umetolewa na Language Recordings Internaional. Hadithi zilizopo katika kitabu cha Bluu ni hadithi za kweli zilizo toka katika Biblia. Mungu aliwaambia Waisraeli kwamba siku moja atamtuma mtu ambaye atakuja kuwaokoa na dhambi zao. Waisraeli walimngojea mkombozi kwa miaka mingi. Ndipo Mungu akamtuma mwanawe wapekee Yesu Kristo, kuja kuishi hapa duniani. Yesu alikuja kama mtoto mdogo na akakuwa na watu wa Israeli walimuona. Na alipo kuwa mtu mzima alianza kuwafundisha watu maneno ya Mungu. Sasa chukua kitabu chako na ufungue katika picha ya kwanza . Unaposikia sauti hii ___________ ufungue picha inayofuata.
Picha ya Kwanza: Yesu Mwalimu wetu
Mathayo 5:1-2
Yesu alisafairi katika Israeli yote na kuwafundisha watu. Yesu alichagua baadhi ya watu ambao wange kaa pamoja. Watu hawa waliitwa wanafunzi. Yesu alichukua muda wake mwingi kuwafundisha wanafunzi wake, na wakati huo huo watu wengine walikusanyika ilikumsikiliza Yesu. Halitumia hadithi ambazo watu wangezielewa na kuzikumbuka. Siku moja Yesu alikaa katika mwinuko pamoja na wanafunzi wake watu wengi wakakusanyika basi Yesu akaanza kuwa fundisha. Watu waliomsikia Yesu walishaanga sana. Nao walitambua kwamba Yesu akufundisha kama waalimu wangine, bali aliwafundisha kama mtu mwenye mamlaka. Yesu alikuwa ni mwaliku aliye toka mbinguni kwa Mungu. Na aliwafundisha watu kwamba yeye alikuwa mwana wa Mungu, na kwama yeye na Mungu walikuwa kitu kimoja. Watu wengi walimsikia Yesu na mafundisho yake nao wakamfuata.
**MB**Rafiki mpendwa, Endelea kusikiliza na nitakuwambia, ni mambo gana ambayo Yesu aliwafundisha wale watu, nawe utapata kujua ukweli wa Mungu aliye hai.
Picha ya Pili: Nyumba Mbili
Mathayo 7:24-27
Yesu aliwafundisha watu habari za watu wawili waliojenga nyumba. Mtu wa kwanza lijenga nyumba yake juu ya mwamba(SE building). Baada ya muda mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga ile nyumba **SE wind, rain** Lakini, haikuanguka; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Yesu akasema, basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mtu wa pili alikuwa mtu mjinga, alijenga nyumba yake juu ya mchanga (**SE house building**) Na baada ya muda mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga ilenyumba (**SE wind, rain**) Nalo anguko lake likawa kubwa, kwasababu alijenga juu ya mchanga. Kisha Yesu akasema, Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
**MB** Rafiki Mpendwa, Ni vima kama tukijenga nyumba zetu katika mwamba. Tukitaka kujenga nyumba zetu juu ya mwamba ni lazima tufuate mafundisho ya Yesu na kuyafanya yale anayo tuamuru. Tukifanya hivyo, hata shetani hawezi kutuangushwa kwani tumesimama katika mwamba. Fikiria zaidi juu ya habari hii na wewe mwenyewe uchague, kuwa mtu mwenye hekima au kuma mtu mpumgavu.
Picha ya Tatu: Nuru Ionekane (Nuru ya ulimwengu)
Mathayo 5:14-16
Hakuna mtu apendaye kuona giza. Wakati mwingine tunapo kuwa katika sehemu ya gizani tunaogopa. Kunapokuwa katika sehemu ya giza tunaogopa na kuwaza, labda kuna adui au kitu furani kina kukaribia. Katika giza kuna mambo mengi ambayo yanatokea. Katika picha unamuona mtu mmoja ambaye ameshika nuru na anawapa watu wa nyumbani mwake nuru. Lakini mtu mwingine ameficha nuru yake katika kikapu. Yeye hawezi kuwasaidia watu wengine wapate nuru. Yesu alisema, (second voice) "Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba(Mungu) yenu aliye mbinguni."
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu ndiye hiyo nuru ya ulimwengu. Hanatuonyesha njia ya kwenda kwa Mungu. Nasi tunapo kubari kutii Neno la Mungu wengine wanapata nafasi ya kuona nuru yetu.
Picha ya Nne: Kulipiza kisasi
Mathayo 5:38-42
Yesu alipokuwa duniani aliishi kama Waisraeli wengine. Lakini Waisraeli waliacha sheri ya nchi yao. Na walitawaliwa na Warumi. Warumi walikuwa na nguvu juu ya Waisraeli. Na wakati mwengine Warumi waliwafaniya mbamo mabaya Wasraeli. Warumi waliwapiga Waisraeli na kupola vitu vyao kama unavyo ona katika picha, wakati mwingine waliwalazimisha kubeba mizigo mizito kwa mwendo mrefu. Jambo hili lili wakasirisha sana Waisraeli na wakaanza kulipoza kisasi. Lakini Yesu akawafundisha kitu cha tofauti. Yesu akasema, (second voice) "Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili......... Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili." Pengine watu wanatutendea mambo yasiofaa, tuwe wepese wa kulipiza kisasi. Lakini tukumbuke kwamba sisi ni wafuasi wa Yesu, na Yesu alisema, (second voice) "lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni"
**MB** Rafiki mpendwa, Sisi tulio wanafunzi wa Yesu tukiamua kuwafanyia mema wale wano tuudhi, watu wote watatambu kwamba sisi ni watu wa Yesu na watamtukuza Mungu kwa mambo tunayo yafanya.
Picha ya Tano: Kumwomba Mungu
Mathayo 6:5-15
Katika hizi picha mbili tunaona watu wawili wanamwomba Mungu. Yesu aliongea na wanafunzi wake juu ya hao watu na jinsi ambavyo iliwapasa kumumba Mungu. Yesu akasema watu wengine wanaenda katika mji ambapo kuna watu wengi ili kuomba na wanomba maombi marefu. Wanafanya hivyo ili waonekane mbele ya watu. Lakini Mungu hafurahishwi na maombi yao. Watu hao hawa muombi Mungu bali wanataka watu wawatazame. Yesu alisema, "Msiwe kama wanafiki; Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.", kama wanafiki wafanyavyo. Yesu anasema kunapo kuwa tukimba tusipayuke-payuke. Bali sisi tuombapo tuombe kimya kwa baba yetu aliye sirini naye atatusikia. Pia nilazima kumba msamaha wakati tunapo omba. Pia tuna weza kumuomba maitaji yetu. Tunaweza kumuomba atupe nguvu wakati tunapokuwa katika majaribu. Na tunaweza kumuomba atulinde na yule mwovu shetani. Rafiki yangu, tukumbuke kwamba Mungu wetu ni Mungu mkuu, Naye anatupena na kutujali sisi.
Picha ya Sita: Uovu katika ulimwengu
Mathayo 13:24-30,36-43
Yesu alitumia hadithi na mifano ili watu wote wapate kuelewa. Pia alitumi hadithi za mafumbo watu wengine walielewa na wengine hawakuelewa, na hivyo Yesu akatoa ufafanuzi juu ya adithi hiyo kawatolea mfano mwingine, akisema, (second voice) Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. (first voice) Na tafsiri yake ndiyo hii, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; lile shamba ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
**MB**Rafiki mpendwa, ukichagua kumfuata Yesu, utakuwa umechagua kuingia katika familia ya Mungu nawe utakaa na Mungu mbinguni milele na milele. Je, wewe ni mtu wa familia ya Mungu?
Picha ya Saba: Watoto wa Mungu
Mathayo 18:1-6, 19:13-15
Yesu aliwapenda watoto. Yesu aliongea na wanafunzi wake kuhusu watoto. Yesu alijua kwamba kuna mambo ya muhimu kuhusu watoto ambayo wanafunzi wake wanaiji kujifunza. Watoto hawawezi kujichangulia mambo mazuri ambayo yataweza kuwanufaisha baadaye. Lakini watoto wana wategemea wazazi wao na kuwatii. Yesu alitaka wanafunzi wake waige huo mfano. Yesu alitaka wanafunzi wake wajinyenyekeze wawe kama watoto wadogo. Siku moja watu wakaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea. Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao. Siku moja wanafunzi wa Yesu walikuwa kaibishana ni nani atakaye kaa mkono wa kuume wa Yesu atakapofika mbinguani. Yesu alipo yaona hayo kakamchukua mtoto ndogo akamuweka mbele yao akasema mtu yeyote akitaka kuingia katika ufalme wa Mungu ni lazima ajinyenyekeze awe kama huyu mtoto mdogo. Yesu hakupenda wanafunzi wake wajifikirie kwamba wenyewe ndio watu wa umimu sana. Yeu alitaka wao wajinyenyekeze na waache tofauti zao. Hii ndiyo maana ya kuwa mtoto mdogo.
**MB** Rafiki mpendwa, hao watu wanao jisifu wenyewe kuwa ni watu wakuu kuliko wengine, hawawezi kumfuata Yesu kweli kweli. Ni lazima tujinyenyekeze ili Mungu atusaidie.
Picha ya Nane: Kondoo aliye potea
Mathayo 18:12-14
Yesu aliwaambia wana habari za kondoo waliye aliyeenda mbali na mchungaji na kupotea. Yesu alitaka wanafunzi wake waelewe kwamba Yesu anawajali watu walionda mbali na Mungu na kupotea. Pia alitaka wanafunzi wake kuwajali watu waliopotea. Na hii ndiyo hadithi yenyewe. (Can use second voice) "Mtu mmoja alikuwa na kondoo mia, na kondo mmoja akampotea, Na yule mtu akawaacha wale kondoo tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Hata alipo mwona alimfurahia zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea. Yesu alisema mimi ndimi mchungaji mwema, mchungaji mwema utoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake. Yesu alitoa maisha yake kwa ajili yetu, Yesu alifanya hivyo ili sisi tuingie katika zizi la Mungu. Sisi tukimwamini Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Yeye ataziondoa dhambi zetu. Nasi tutafanywa kuwa kondoo wa Mungu.
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu hataki watu wapotee na kuwa mbali naye. Lakini watu wanapotea kwasababu wanafuata njia ya Shetani. Yesu anajitwa mchungaji mwema kwasababu alikuja kutoa uhai wake na kuwatafuta wale waliopetea katika dhambi. Ikiwa sisi ni watu wa familia ya Mungu. Mungu anataka sisi twende kuwatafuta wale walipotea na kuwaleta kwake.
Picha ya Tisa: Kusameheana
Mathayo 18:21-35
Mala nyingi Yesu aliongoa na wanafunzi wake kuhusu msamaha na jinsi ilivyo kuwa muhimu kuwasamehe wengine. Yesu akawafundisha hadithi hii: (second voice) Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Talanta moja ni kama shilingi 5,000. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja ambaye alikuwa akimdai, aliyemwia dinari*fd* mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe langu. Dinari moja ni kama senti 75. Basi mdeni wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi watumwa wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza yule mfalme yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mdeni wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. (First voice)
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu anatusamehe kwa maovu yetu yote tunayo yafanya, pia sisi tunatakiwa uwasamehe wale wano tukosea.
Picha ya Kumi: Thawabu ya Mungu
Mathayo 20:1-16
Yesu akawafundisha wanafunzi wake habari za mkulima mmoja ambaye aliitaji wafanya kazi katika shamba lake. Yesu akaanza na kusema Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana nao juu ya malipona, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. Akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni katika shamba langu la mizabibu. Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe mshahara wao, ukianzia wa mwisho mpaka wa kwanza. Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu tiasi cha fedha sawa na wengine. Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu sawa na wale wengine. Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia yule aliyewaajili, wakisema, Hao wa mwisho wamefanya kazi saa moja tu, nawe umewapa mshahara sawa na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa. Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; si tulipatana kwa kiasi hicho nilicho kulipa? Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama ipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema? Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho. (first voice)
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu akawapa uzima wa milele wale wano mwamini Yesu. Si kwa kufanya matendo mazuri, la uzima huo ni wa bure na ni zawadi kutoka kwa Mungu tunavyo takiwa kufanya ni kumkubari Yesu.
Picha ya Kumi na moja: Jiandae!
Mathayo 25:1-13
Wanafunzi wa Yesu walimuuliza Yesu maswali mengi. Namoja ya swali walilo muuliza lilikuwa Yesu atarudi rini. Yesu akawatolea hadithi nyingi ambayo ingeweza kuwakumbusha (second voice) Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wasichana kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wajinga, na watano wenye busara. Wale wajinga walizitwaa taa zao, bila kuchukua mafuta ya hakiba. Likini wale wenye busara walitwaa mafuta ya hakiba katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakaziwasha taa zao. Wale wajinga wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wasichana wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, ondokeni, siwajui ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa. (first voice)
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu yupo mbinguni sasa lakini siku moja atakuja nasi hatujui siku la saa. Hatujui atakuja lini. Inatupasa tujiandae wakati wowote. Kwa wale walio mwamini watachukuliwa kwenda naye mbinguni, lakini kwa wale ambao watakuwa hawaja mpokea wataachwa. Nilazima tujue kwa hakika kwamba sisi tupo katika familia ya Mungu.
Picha ya Kumi na mbili: Kumngojea Yesu
Mathayo 25:14-30
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwamba siku moja atarudi tena. Yesu aliwafundisha mambo ya kufanya wakati wakiwa wanamngojea Yesu. Yesu akawafundisha mfano huu: (second voice) Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja elfutano, na mmoja elfumbili, na mmoja elfumoja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Kisha yule aliyepokea elfutano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida elfutano nyingine. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea elfutano, akaleta elfutano nyingine, akisema, Bwana, uliweka kwangu elfutano; tazama, elfutano nyingine nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Bwana wao walifurahishwa sana na wale watumwa wawili. Lakini alipokuja yule wa tatu aliyepokea elfumoja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; basi nikaogopa, nikaenda nikaificha elfu yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu. Bwana wake akakasirika sana akawambi wale watumwe, mnyang'anyeni hiyo aliyo nayo kisha mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
**MB** (first voice) Rafiki yangu, Yesu anafafa na huyu bwana aliye kwenda katika safari. Na wale watumishi ni kama wafuasi wa Yesu. Mungu amempa kila moja wetu uwezo wa kufanya kazi yake. Wengine wetu wamepewa uwezo wa kuhubiri, na wengine kutengeneza vitu kwa ajili ya kazi ya Mungu, na wengine wamepewa uwezo wa kusidia wengine. Yesu anataka sisi tutumie vile tulivyo pewa ilitumtumikie yeye. Naye atakapo rudi atasema, "vema mtumishi mwema na uaminifu, ingia katika raha ya Bwana wako.
Picha ya Kumi na tatu: Yesu Abatizwa
Marko 1:4-11
Yesu aliwafundisha watu habari za Mungu, pia aliwaonyesa watu kwamba alikuwa na uweza mkuu. Miaka mingi iliyopita, mtu mmoja aliyeitwa Yohana Mbatizaji, alitumwa na Mungu ili awe nabii kwa watu wa Israeli. Yohana aliwaambia watu, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Yohana alikuwa akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba uletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Yohana akawa akihubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza kamba ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu. Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. Yesu alitaka kuwaonyesha watu kwamba yeye alitaka kumtii Mungu, pia alitaka kuwaonyesha watu kwama kazi yake ilikuwa imeanza. Hivyo Yohana akambatiza Yesu. Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; na sauti ikatoka mbinguni, "Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe."
**MB** Rafiki yangu, Yesu alikuwa ni mtu aliye mtii Mungu, pia alikuwa mwana wa Mungu, kila alisho fanya ni kumpendeza Mungu. Yesu alikuwa tayali kuanza kazi yake ya kuwaambia watu maneno ya Mungu. Rafiki endelea kusikiliza na utasikia mambo mengi ya ajabu aliyo yafanya Yesu.
Picha ya Kumi na nne: Yesu Achangua Wasaidizi wake (Wanafunzi)
Marko 1:14-20
Mungu alimtuma Yesu kuja duniani kufanya kazi maalum. Yasu akaanza kazi yake. Yesu akazunguka Israeli na kuwafundisha watu habari za Mungu. Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, "Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili." Yesu alitaka watu ambao watakuwa karibu naye ili wafanye kazi hii pamoja. Naye Yesu alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa nyavu baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao. Mara akawaita, wakaacha vyote ndani ya chombo, wakaenda, wakamfuata. Yesu akachagu watu kumi na mbili na hao waliitwa wanafunzi. Yesu akawafundisha hao wanafunzi habari za Mungu Baba, Mungu Mwana(ambaye ndiye Yesu mwenyewe) na Mungu Roho. Yesu akawafundishwa wanafunzi wake mambo mengi, kwamba yeye ni mwana wa Mungu na siku moja atakufa na kufufuka. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake ili wao nao wawafundishe na wengine
**MB** Rafiki yangu. Hata leo Yesu anataka watu wawe wafuasi wake. Yesu anataka wanaume na wanawake na watoto, wawe wafuasi wake, pia anataka sisi kuwaambie wengine habari njema.
Picha ya Kumi na tano: Mwanaume Atakaswa
Marko 1:40-45
Yesu aliendelea kuhubiri habari njema za Mungu. Siku moja akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika. Mtu yule akafurahi sana. Yesu alikuwa na uweza mkuu wa ajabu. Aliweza kufanya miujiza hambayo watu wengine hawawezi. Yesu ni mwenye huruma, alimuhurumia sana yule mtu mwenye ukoma.
**MB**Rafiki yangu, Yesu anatupenda sisi sote, ingawa anafahamu dhambi zilizomo mioyoni mwetu lakini yeye bado anatupenda. Dhambi ni kama ugongwa wa ukoma. Kwani dhambi inatufanya sisi tusiwe wasafi, na kwasababu ya uchafu katika mioyo yetu, dhambi inatutenganisha sisi na Mungu kwasababu Mungu ni mtakatifu. Kama tukimuendea Yesu na kumuomba azioshe dhambi zetu, Yeye atafanya hivyo yaani atatuondolea dhambi na kufanya utuwe safi, maana ametuahadi katika Neno lake.
Picha ya Kumi na sita: Mtu Mwenye Ugonjwa wa Kupooza Atemebea
Marko 2:1-12
Yesu Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, "umesamehewa dhambi zako." Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu? Na huyu ni mtu tu wala si Mungu. Waliwaza hivyo maana walitaka kumshitaki. LakiniYesu akamwambia yule aliyekuwa mapooza, Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako. Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata watu wote wakastaajabu wakamtukuza Mungu, wakisema, hajawahi kutokea mtu kama huyu. Na watu wote waliokuaw mahali pale walitambua kwamba Yesu alikuwa na nguvu. Yesu alikuwa mwanadamu, pia alikuwa Mungu, na alikuwa na uweza wa kufanya miujiza.
**MB** Rafiki yangu, labda wewe ni kama yule mtu mwenye kupooza. Uwezi kutembea kwa unanguvu katika mwili wako. Unaweza kumuomba Yesu naye ataweza kukusamehe dambi zako na kukufanya uwe na nguvu.
Picha ya Kumi na saba: Mkono Uliopooza
Marko 3:1-6
Miaka mingi iliyopita Mungu aliwapa Waisraeli amri kupitia mtumishi wake Musa. Hizo amri au sheria ziliwasaidia Waisraeli kuelewa Mungu na jinsi ya kuishi kwa kumpendeza Mungu. Waliambiwa katika sheria ya Musa kwamba waikumbuke siku ya sabato na kuifanya takatifu kwa Bwana, siku hizi siku hiyo ni juma pili. Waisraeli hawakutakiwa kufanya chochote siku ya sabato. Siku moja ilikuwa siku ya sabato, Yesu alikuwa ameingia katika sinagogi; na huko palikuwako na mtu mwenye mkono uliopooza . Basi hapo palikuwa na wakuu wa dini nao wakamvizia ili kuona kama atamponya huyo mgojwa siku ya sabato; wapate kumshitaki. Wao hawakumjali yule mtu, wao walitaka kufuata sherea ya Waisraeli. Lakini Yesu Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza. Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. Yule mtu akafurahi sana lakini wale wakuu na waandishi walikasirika sna walipona kwamba yule mtu amepona.
**MB** Rafiki yangu, nilazima kumwabudu Mungu, pia ni vizuri kuwasaidia na wengine, bila kuwasaidia wengine, kuabudu kwetu kutakuwa hakuna maana.
Picha ya Kumi na nane: Yesu Akomesha Dholuba
Marko 4:35-41
Yesu alikuwa amekaa chomboni kandokando ya maji akiwafundisha watu habari za Mungu. Na kulipokuwa jioni, akawaambia, wanafunzi wake na tuvuke mpaka ng'ambo Galilaya basi wakauacha mkutano, wakavuka. Naye Yesu kwasababu alikuwa amechoka akajilaza katika mtumbwi. Walipokuwa wakivuka, mara Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. Naye Yesu mwenyewe alikuwa amelala, wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?
**MB** Rafiki mpendwa, Yesu ananguvu juu ya vitu vyote vilevyo umbwa. Tusiogope tunapo kumtumaini yeye. Yesu anajua vile tunavyo teseka. Yeye tu ndiye anaye weza kutupa amani katika mioyo yetu.
Picha ya Kumi na tisa: Mwanamke Mwenye Kutokwa na Damu
Marko 5:15-34
Yesu na wanafunzi wake wakavuka mpaka ng'ambo. Na walipofika walikuta kusanyiko kubwa la mkutano likimgojea Yesu.
Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona tatizo ile. Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa? Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo. Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na tatizo ilo tena.
**MB** Yesu aliwaonyesha watu kwamba alikuwa na uweza wa kuponya magonjwa. Pia aliwaonyesha watu wakwamba yeye anajua siri za mioyo ya watu. Ni vema kama tukimuomba Yesu atusamehe dhambi zetu bila ya kuficha uovu wetu. Tukifanya hivyo tutakuwa na nguvu ya kumtumikia Yeye na kumpendeza.
Picha ya Ishirini: Mtoto Aliye Kufa Awamzima Ten
Marko 5:22-24,35-43
Na mtu mmoja mkuu wa sinagogi aliyeitwa Yailo. Alimwendea Yesu na kumuomba amwombee mtoto wake maana likuwa naumwa sana. Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. Lakini Yesu hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo. Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana. Akamshika mkono kijana, akamwambia, Msichana, nakuambia, Inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu. Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula.
**MB** Rafiki yangu, Shetani anafikiri akimuua mtu ndio amefauru., lakini Yesu anauwezo wa kumfufua mtu. Watu waliokolewa hawaitaji kuopoga kifo kwani Yesu alishinda kifo naye anauwezo wa kumshinda Shetani na mauti. Kama tukimwamini Yesu yeyatakupa uzima wa milele.
Picha ya Ishiri na moja: Imani Ya Mwanamke Mgeni
Marko 7:24-30
Basi Yesu akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu, lakini haikuwezekana, maana watu walimfuata kokote alipokwenda. Na mwanamke, mmoja ambaye binti yake alikuwanapepo mchafu, alisikia habari za Yesu, akaja akamwangukia miguuni pake. Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake. Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto. Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako. Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.
**MB** Tumejifunza katika habari hizi kwamba Shetani akajaribu kuwatesa watu na kuwaongoza katika njia zake. Lakini nguvu za Yesu zina uwezo mkuu. Tunapo shindwa tunaweza kumuomba Yesu ili atusaidie. Yesu anaweza kutuweka huru, tuwe mbali na mateso ya shetani. Yesu anawapenda watu wote naye anataka kuwasaidia.
Picha ya Ishirini na mbili: Mtu Aliyekuwa Kiziwi na Bubu, Aongea na Kusikia
Marko 7:31-37
Yesu na wanafunzi wake wakatoka tena katika mipaka ya Tiro, wakapita katikati ya Sidoni,wakaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. Wakamletea kiziwi, naye ni bubu, wakamsihi amwekee mikono. Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akamhurumia, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari; wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema,viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme
**MB** Rafiki yangu, Yesu anaweza kufungua masikio yetu nasi tunaweza kusikia na kuelewa Neno la Mungu, pia kuwatangazia wengine.
Picha ya Ishirini na tatu: Yesu Amponya kipofu
Mark 8:22-26
Hata Yesu na wanafunzi wake walipofika Bethsaida, watu wa huko wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda. Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. Mkutano mzima ukapatwa na mshangao. Lakini yeye aliyeponywa akaenda zake kwa furaha akimsifu Mungu. Yesu alifanya mujiza mingi sana ambayo watu wengine hawakuweza kufanya.
**MB** Rafiki yangu, Shetani amewapofusha watu iliwasione ukweli wa Yesu. Lakini yatupasa tumuombe Mungu awafungue ili macho na wapate kuona, na wafungue masikio iliwasikie ukweli wa Mungu.
Picha ya Ishiri na nne: Nguvu za Yesu zime Mshinda Shetani
Marko 9:14-27
Siku moja Yesu aliwachukua wanafunzi wake, Petro, Yakobo na Yohana. Na hao wanafunzi wengine wakabaki, na mtu mmoja kamleta mtoto wake ambaye alikuwa mgonjwa. Yesu na hao wanafunzi walipo rudi walikuta wakibishana. Hata walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao; mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikawaomba wanafunzi wako wamtoe pepo, nao hawakuweza. Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Mleteni kwangu. Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. Yesu akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Yule baba akajibu, tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama.
**MB** Rafiki mpendwa, Habari hizi zinatufundisha na kutuelewesha kwamba nguvu za Yesu ni kubwa kulik nguvu za Shetani. Yesu ni mwana wa Mungu. Na anauwezo mkuu hakuna kitu kinacho weza kumshinda. Ikiwa tutamkubari Yesu angie katika mioyo yetu yeye atakaanasi na nguvu zake zitakuwepo katika maisha yake. Pia tunahitaji kuwaomba kwa bidii. Na watu wengine wataweza kuonga ngu za Mungu katika maisha yetu