unfoldingWord 29 - Simulizi ya Mtumishi Asiye na Huruma
Omrids: Matthew 18:21-35
Script nummer: 1229
Sprog: Swahili
Publikum: General
Formål: Evangelism; Teaching
Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture
Status: Approved
Scripts er grundlæggende retningslinjer for oversættelse og optagelse til andre sprog. De bør tilpasses efter behov for at gøre dem forståelige og relevante for hver kultur og sprog. Nogle anvendte termer og begreber kan have behov for mere forklaring eller endda blive erstattet eller helt udeladt.
Script tekst
Siku moja, Petro alimuuliza Yesu "Bwana, ni mara ngapi inanipasa kumsamehe ndugu yangu akinikosea? Hadi mara saba?" Yesu akasema, "Sio mara saba, bali sabini mara saba!" Kwa hili, Yesu alimaanisha inatupasa kusamehe kila wakati. Yesu akawaambia habari hii.
Yesu akasema, " Ufalme wa Mungu unafananishwa na mfalme alie taka kukusanya madeni yake kutoka kwa watumishi wake. Mmoja wa watumishi wake alikua anadaiwa deni kubwa lenye thamani ya mshahara wa miaka 200,000."
Kwakua yule mtuishi hakuweza kulipa deni, mfalme alisema, 'muuzeni huyu mtu na familia yake kama watumwa ili kulipa deni lake.
Yule mtumishi alianguka na kupiga magoti mbele ya mfalme na kusema, ' naomba nivumilie, na nitalipa deni loote unalonidai.' Mfalme alimuonea huruma yule mtumishi, ndipo akafuta deni lake lote na kumuacha aende zake.
Ila baada ya mtumishi kutoka kwa mfalme, alimpata mtumishi mwenzake aliekua akimdai deni lenye thamani ya mshahara wa miezi minne. Alimkamata yule mtumishi mwenzake na kusema, ' Nilipe hela ninayo kudai!"'
"Yule mtumishi mwenzake alianguka na kupiga magoti na kumwambia, 'Tafadhali nivumilie, nitakulipa kiasi chote unachonidai.' Ila, yule mtumishi alimtupa mtumishi mwenzake ndani ya gereza hadi atakapo lipa deni lake.
Baadhi ya watumishi wengine walioona kilicho tokea walifadhaika sana. Wakaenda kwa mfalme na kumuambia kila kitu.
Mfalme alimwita yule mtumishi nakumuambia, 'Ewe mtumishi muovu! Nilikusamehe deni lako kwasababu ulinisihi. Ungefanya vivyo hivyo.' Mfalme alikasirika sana na kumtupa yule mtumishi muovu gerezani mpaka atakapo lipa deni lake lote.
Ndipo Yesu akasema " Hivi ndivyo baba yangu wa mbinguni atakavyo fanya kwa kila mmoja wenu kama hamtawasamehe ndugu zenu kutoka moyoni".