ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu Cha Nane: Matendo Ya Roho Mtakatifu
Kontur: The Young Church and Paul. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.
Skript nömrəsi: 425
Dil: Swahili: Tanzania
Mövzu: Sin and Satan (Spiritual Warfare, Deliverance); Christ (Ascension); Eternal life (Salvation); Character of God (Holy Spirit, Word of God (the Bible), Power of God / Jesus); Living as a Christian (Worship, Church, Christianity, No other gods, idols, Repentance, Faith, trust, believe in Jesus, Children of God, Spiritual Life, Christian values); Bible timeline (Gospel, Good News); Problems (Problems, troubles, worries)
Tamaşaçılar: General
Məqsəd: Teaching
Features: Monolog; Bible Stories
Vəziyyət: Approved
Skriptlər digər dillərə tərcümə və qeyd üçün əsas təlimatlardır. Onlar hər bir fərqli mədəniyyət və dil üçün başa düşülən və uyğun olması üçün lazım olduqda uyğunlaşdırılmalıdır. İstifadə olunan bəzi terminlər və anlayışlar daha çox izahat tələb edə bilər və ya hətta dəyişdirilə və ya tamamilə buraxıla bilər.
Skript Mətni
Utangulizi
Nifuraha yangu kwamba umejiunga pamoja nasi leo ilikusikiliza habari za kweli na picha kutoka katika kitabu cha Mungu, ambacho ni Biblia. Katika kanda hii pamoja na picha inatolewa na produced by Language Recordings International. Fungua katika picha ya kwana, kisha tutaanza. Unaposikia sauti hii ___________ ufungue picha inayofuata.
Picha Ya Kwanza:Bwana Yesu Apaa Kwenda Mbingun
Matendo ya Mitume 1:1-11
Tumesikia habari za Yesu. Yesu ni mwana wa Mungu. Alikuja ulimwenguni kuishi kama mwanadamu na kuwa fundisha watu habari za Mungu. Yesu alifanya mambo mengi sana kuwaonyesha watu kwamba yeye alikuwa Mungu. Lakini watu wengine walimchukia Yesu na kunena maneno ya uongo juu yake. Isitoshe wakamsulubisha Yesu msalabani. Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, lakini alifufuka tena. Akawatokea wanafunzi wake na kuwaonyesha kwamba alimshinda Shetani. Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Yesu akaja kwao, akasma nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari." Yesu akawaambai wanafunzi wake kwamba wakati wake wa kupaa mbinguni ulikuwa umewadia. Ndipo akawachukua wanafunzi wake hadi mlima wa Mizeituni. Yesu akawaambi wanafunzi wake wakae Yerusalemu na kungoja hata atakapo mtuma Roho Mtakatifu,. Ndipo Yesu akasema, "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, "Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni."
Picha ya Pili: Kuja Kwa Roho Mtakatifu
Matendo 2:1-12
Yesu alipopaa mbinguni, wanafunzi wake wakarudi Yerusalemu. Nao walikuwa wakingoja hadi ya Roho Mtakatifu. Hata walipokuwa wamekusanyika kukajaa ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Wanafunzi walifurahi sana kupokea Roho Mtakatifu. Ahadi ya Yesu ilikuwa imetimia. Na Roho Mtakatifu alikuwa mioyoni mwao, wanafunzi walifurahi sana kwani walijua kwamba Yesu atakuwa pamoja nao.
**MB** Rafiki Mpendwa, ahadi ambayo Yesu aliyowapa wanafunzi wake, ni ahadi ambayo ametupa sisi pia. Kama tukimpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wetu, Yesu atamtuma Roho Matakafu mionyoni mwetu. Roho Mtakatifu atatufundisha na kutusaida tuelewe Neno la Mungu. Mungu alipo mtuma Roho Matakatifu kwa wanafunzi wa Yesu, wanafunzi waliongea lugha mbali mbali ambazo hawakuzielewa. Na hiya yalitokea kwa wanafunzi ili watu wote wapate kuelewa Neno la Mungu na wapata kujua uwezo mkuu wa Mungu katika lugha. Utasikia mengi ukiendelea kusikiliza kanda hii.
Picha Ya Tatu: Petro Aanza Kuhubiri
Matendo 2:14-41
Na watu huo huo Waisraeli walioishi katika nchi mbali mbali walikuwepo Yerusalemu. Nao walikuja kwa ajili ya mkutano. Nao wakasikia habari za wanafunzi na jinsi upepo ulivyo ikumba nyumba ambayo wanafunzi walikuwamo. Na watu waliotoka katika nchi mbali mbali walisikia maneno ya Mungu katika lugha zao. Petro ambaye alikuwa mwanafunzi wa Yesu, alisimama na kuwaambia watu waliokuwa wamekusanyika, Petro akasema, mambo ambayo mnayasikia na kuyaona leo ni kwa ajili ya nguvu za Roho Mtakatifu wa Mungu. Petro akaendelea na kusema, "Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu." Watu wengi walimsikiliza Petro kwa makini sana na wengi wao wakaamua kumfuata Yesu na kutubu dhambi zao, nao wakapokea uwezo wa Roho Mtakatifu. Na hilo lilikuwa ni kundi la kwanza la watu waliompokea Yesu kwa kusikiliza mahubiri ya mitume.
Picha Ya Nne: Kanisa La Kwanza
Matendo 2:42-47
Watu wengi katika Yerusalemu walianza kumfuata Yesu. Na baadaye waliitwa Wakristo. Walikua ni watu wenye furaha sana na walikuwa wakikutanika kila siku. Walitumia mali zao kwa pamoja, na walisaidiana katika shida. Kila siku walikuta kumsifu Mungu na kumwomba Mungu. Watu wengi miongoni mwao hawakujua sana mafundisho ya Yesu, kwahivyo Petro na wanafunzi wengine walianza kuwafundisha Wakristo wapya katika nyumba zao. Hivyo walikuwa wakikutanika katika nyumba zao ili kujifunza. Pia Yesu alikuwa amewafundisha wanafunzi wake jinsi ya kumkumbuka. Usiku ule kabla Yesu ajateswa, Yesu alikula pamoja na wanafunzi wake. Na wakati wakula Yesu alichukua mkate, naye akaukata katika vipande, na akawapa wanafunzi wake. Yesu akawaambia wanafunzi wake kwamba mkate huu ni mfano wa kukumbuka mwili wake, ambao uliteshwa na kuvunjwa kwa ajili ya watu wote. Kisha Yesu akachukua akakitwaa kikombe, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu." Na hivyo ndivyo walivyo kuwa wakifanya wale watu wa kanisa la kwanza, yaani kumkumbuka Yesu.
**MB**Rifiki yangu, Wakristo wa kwanza walikusanyika pamoja, ili kumsifu Mungu, kumuomba Mungu na kusaidiana. Walifanya hivyo kwa upendo na waliona raha kubwa katika kushirikiana. Na watu wengine wasio mjua Mungu waliona ni vema kumfuata Yesu. Pia sisi Wakristo wasasa tunaitaji kuiga mfano huo. Je, tunakutanika pamoja kama wa walivyo fanya Wakristo wa kwanza? Je, una saidiana? Hebu tuombe ili kwamba watu wengine waone matendo yetu mema na wamfuate Yesu.
Picha Ya Tano: Kuvu Ya Kuponya
Matendo 3:1-16
Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. Mtu huyu alipowaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na Petro, akamkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao. Lakini Petro akasema, "Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende." Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.
**MB**Rafiki mpendwa, Roho Mtakatifu wa Mungu aliwapa wanafunzi nguvu na uwezo wa kuponya watu. Na Roho Mtakatifu aliwapa wanafunzi ujasilisi wa kuhubiri habari za Yesu. Ikiwa umempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, basi unaye Roho Mtakatifu ndani yako. Mwombe Roho Matakatifu ili akusaidie kufanya kazi ya Mungu na kuwaambia wengine habari za Yesu.
Picha Ya Sita: Kumtolea Mungu
Matendo 5:1-11
Wakristo walioko Yerusalemu walitaka kuwasaidia watu masikini. Hivyo walitoa pesa zao na mali zao ili kuwasidia masikini. Mtu mmoja jina lake Barnaba aliuza mali zake na kuleta pesa kwa viongozi wa Kanisa. Mtu mwingine jina Anania naye alifanya vivyo hivyo akauza mali zake na akaleta pesa kwa viongozi wa kanisa. Lakni Anania akaficha baadhi ya fedha. Petro akamuuliza Anania, "je, hii pesa uliyo leta thamani yake ni sawa na mali uliyo iuza?" Anania akasema ndiyo. Lakini Petro alijua kwamba Anania alikuwa ameficha baadhi ya fedha. Petro akasema, "Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja. Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu." Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamwambia, "Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo?" Akasema, "Ndiyo, kwa thamani hiyo." Petro akamwambia, "Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe." Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.
**MB** Rafiki yangu, Si vema kupenda pesa kuliko kumpenda Mungu. Mungu anakasirika sana napoona watoto wake wanapenda pesa kuliko kumpenda Yeye. Hatuna budi kumpenda Mungu.
Picha Ya Saba: Stefano—Mwaminifu Mpaka Kufa
Matendo 6:1 - 8:3
Katika Yerusalemu kulikuwa na watu wengi ambao wamekubari kufuata Yesu. Wa Wakristo walikuwa wakiendelea kuwasaidia watu masikini. Kwasababu kazi ya kuwahudumia wajane ilikuwa kubwa. Mitume wakaona ni vema kuchagua watu ambao watawasaidia katika kazi ya utumishi. Basi Stefano mtu aliyejawa na Roho, na ni mtu aliye shuhuduiwa kuwa mwema alichaguliwa kuwa msaidizi. Stefano alikuwa ni mtu aliyependa kuhubiri habari za Yesu. Basi viongozi wa Wayahudi wakatafuta njia ya kumua. Siku moja viongozi wa wadini wa kiyahudi walimsitaki Stefano nao wakamuweka Stefano mbele ya mbalaza ili ajitete. Lakini Stefano alitoa maneno ya ukweli ambayo alichoma mioyo yao. Basi hao walioshitaki wakakasirika sana, na wakaanza kumpiga Stefano kwa mawe. Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, "Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Walipoyasikia maneno hayo, wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia Stefano kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
Picha Ya Nane:Neno Habari Njema Yaenezwa
Matendo 8:4-8, 26-40
Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. Hivyo Wakristo wakakimbia na kutawanyika. Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri Neno la Mungu. Na Mtu mmoja aliyeitwa Filipo akabaki Yerusalemu na akawa akiwahubiria watu Neno la Mungu. Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiria habari za Kristo. Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini mpaka njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Unayaelewa hayo unayosoma? Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba unieleweshe, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu. Basi Filipo akambatiza, naye akaondoka kwa furaha.
**MB** Rafiki yangu, Filipo ni mfano mzuri kwetu. Alikwenda sehemu mbili mbali kutangaza Neno la Mungu. Naye alikuwa tayari kumtii Roho wa Mungu. Sisi pia tuwe tayari kuwaambie watu habari za Yesu.
Picha Ya Tisa: Maono Ya Petro
Matendo 10:9-18
Wakristo waliendelea kufunya kazi ya kuwaambia watu wengine habari za Yesu. Kwasababu hao wakristo wengi wao walikuwa ni Waisraeli, hawakuwaambia watu wa mataifa mengine habari za Yesu bali walikenda kwa Waisraeli tu na kuwaambia habari za Yesu. Lakini Mungu alitaka watu wote wapate kusikia habari njema. Na hivi ndivyo ilivyo kuwa.. Basi Petro akakaa siku kadha wa kadha huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simon. Siku moja Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana; akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi; ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani. Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule. Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi. Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapaa na kupokelewa mbinguni. Petro akashituka katika ndoto yake.
**MB** Endelea kusikiliza kanda hii nawe utasikia mengi juu ya hadithi hii. Ukumbuke kwamba kumtii Mungu ndilo jambo la muhimu sana kwetu. Mungu anajua tunayo yahitaji naye atatupa.
Picha Ya Kumi:Wokovu Ni Kwa Wote
Matendo 10:1-8, 17-48
Wagani ambao Mungu aliwatuma, walifika nyumbani kwa Petro. Walikuwa Wayunani. Kisha Petro aligundua kwamba Mungu anataka Petro awaone Wayunani kama anavyo waona Waisraeli. Yaani Wayunani sio watu najisi. Kisha Petro na rafiki zake Waisraeli, pamoja na Wayunani watatu waliondoka. Yopa na walienda mahali palipoitwa Kaisarea. Kisha wakaenda nyumbani kwa Kornelio. Kornelio alikuwa Myunani. Pia alikuwa jemedari wa jeshi la Warumi. Kornelio alikuwa mtu mcha Mungu. Familia nzima ya Kornelio alikuwa wanampenda Mungu. Kornelio alifanya mambo mazuri mengi kwa watu wa Israeli. Siku chache zilizopita, Mungu alimtuma malaika kuongea na Kornelio, " Malaika akasema, Kornelio Mungu amependezwa na sadaka zako na maombi yako yamekubaliwa na Mungu". Sasa uwatume watu waende Yopa. Na wamtafute mtu anayeitwa Petro na wamwalike aje akutembelee. Wakati huo ndipo Kornelio alipo watuma watu waende Yopa. Petro na rafiki zake wakafika nyumbani kwa Kornelio. Na walipoingia ndani Kornelio akapiga magoti mbele ya Petro (ili kumheshimu). Lakini Petro akasema, "Hapana usimame! Mimi sio mungu, mimi ni mtu tu" Kisha Petro akaongea na watu ambao walikuwa ni Wayunani waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa Kornelio. Petro akasema, " Enyi Wayunani manajua kwamba ni kinyume cha sheria ya Waisraeli kwa mwisraeli kama mimi kuingia katika nyumba ya Wayunani. Lakini Mungu alinionyesha katika maono. Kwamba nisiwaone Wayunani kama watu najisi. Kwahivyo nimekuja kwenu. Kornelio akamwambia jinsi malaika wa Mungu alivyoongea naye. Kisha Petro alimwambia Kornelio habari za Yesu. Kornelio na familia yake wakamwamini Yesu na kupokea Roho Mtakatifu.
**MB** Rafiki yangu, Mungu anawapenda watu wote, haijalishi lugha, kabila au rangi za ngozi. Anataka watu wote wamwamini Yesu Kristo na wamtumikie.
Picha Ya Kumi Na Moja:Petro Akiwa Gerezani
Matendo 12:1-11
Watu wengi waliamua kuwa Wakristo na walianzisha vikundi kwa ajili ya maombi. Jambo hili iliwakasirisha viongozi wa Wayahudi. Mfalme Herode aliaza kuwafanyia wakristo mambo mabaya sana. Alimuwa Yakobo ambaye alikuwa kiongozi wa Wakristo, na limuweka Petro gerezani. Na aliweka walinzi wengi iliwamlinde Petro. Siku moja Petro alikuwa amelala katika gereza huku mikono yake ikiwa imefungwa minyororo. Gafla malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaota ndoto. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, na mlango ukafunguka wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua hakika kuwa Bwana amemtuma malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode. Hata kulipopambauka askari wakaingiwa na hofu nyingi, maana hawakumuona Petro. Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwauliza-uliza wale walinzi, akaamuru wauawe.
**MB**Rariki yangu, tunajua kwamba wakati mwingine wakristo wanapatwa na matatizo mengi na kuteseka. Tukumbuke kuwa Mungu anatawala vitu vyote. Tumtegemee Mungu iliatulinde katika matatezo yetu.
Picha Ya Kumi Na Mbili:Nguvu Za Maombi
Matendo 12:12-19
Mfalme Herode alipomfunga Petro gerezani, Wakristo walikushanyika na kumuombea Petro. Baada ya malaika wa Mungu kuomtoa Petro gerezani, Petro aliamua kwenda nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza. Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. Wakanena, Ni malaika wake. Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Na watu wote wakafurahi sana. Petro akakaahuko na kuwafundisha watu habari za Yesu.
**BM**Rafiki mpendwa, Mungu anasikia maombi yetu, na antaka sisi tuombe kila wakati. Mungu ni Mungu mwenye nguvu nyingi. Anatawa la vitu vyote. Mungu anasema hivi katika Neno lake, "Niite nami nitakuitikia, nitakuonyesha mambo makubwa usiyo yajua."
Picha Ya Kumi Na Tatu:Habari Ya Paulo – Jinsi Alivyo Badilishwa
Matendo 9:1-19
Tumesikia habari za Paulo aliyeitwa Sauli, jinsi alivyo watesa Wakristo waliyo kuwa wakiishi Yerusalemu. Ingawa aliwatesa, watu wengi zaidi waendelea kumfuata Yesu. Siku moja Sauli alikua akisafiri kwenda Dameski ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu. Sauli akainuka katika Yesu akamwambia Sauli nimekuchagua wewe ili uwe mtumishi wangu nawe utawaambia watu habari njema. Nawe utawafumbua watu masikio yao ili wasikie ukweli. Utawasaidia wapotevu waache njia zao mbaya na kumgeukia Mungu. Nami nita wasamehe.nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
**MB** Hadithi hii inatusaidia tuelewe kuwa nguvu za Mungu ni kubwa. Watu wengine wanaweza kujaribu kusimamisha kazi ya Mungu. Lakini hawata weza kushindana na Mungu kamwe. Mungu ni Mungu wa ajabu anaweza kuwabadirisha watu. Mungu anaweza kuzisamehe dhambi mtu. Na kumpa moyo mpya. Naye atakuwa na moyo wa kumpenda Mungu.
Picha Ya Kumi Na Nne:Mtii Mungu –Usiogopa
Matendo 9:10-20
Paulo alikuwa Dameski kwa siku tatu bila kula wala kunywa. Na hakuweza kuona: alikuwa akimuomba Mungu. Basi wakampeleka Sauli kwa mtu aliye kwa mcha Mungu jina lake Anania. Basi Anania akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; akala chakula, na kupata nguvu. Kisha Anania akamwambia kwamba Yesu ni mwana wa Mungu.
**MB** Rafiki yangu, wakati mwingine Mungu anaweza kutuambia tufanye kitu ambacho kwetu ni kigumu. Tusiogope bali tufanye kama Mungu anavyo taka. Tunajua kwamba Mungu anatujali na kutusaidia. Mungu anaweza kututumi sisi kuongea na watu wengine. Tukimtii Mungu tunaweza kuwasaidia watu wengine wawe wafuasi wa Yesu.
Picha Ya Kumi Na Tano:Kanisa Litume Watu Waende Kuwa Huhubiria Wapotevu
Matendo 13:1-3
Paulo na Barnaba walisafiri mpaka sehemu hinayo itwa Antiokia. Walianza kuwafundishwa Wakristo wapya huko Antiokia, na baada ya muda kulikuwa na kundi kubwa la Wakristo wanao mpenda Mungu na kufanya kazi yake. Na siku moja walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Na kazi hiyo ilikuwa ni kwenda sehemu mbali mbali na kufungua makanisa. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu Paulo na Barnaba, kisha wakawaacha waende kufanya kazi walioitiwa.
**MB** Rafiki yangu, Hata leo hii kuna watu wengi sana ambao hawa mfahamu Yesu. Ni kazi wa Wakristo kuenda kwa watu wasio mjua Mungu na kuwaambia habari za Yesu. Roho wa Mungu akituita tunatakiwa kuwe tayari kuenda. Tuna hitaji kuwaendea na kufunga nao urafiki pia tuwaombee.
Picha Ya Kumi Na Sita:Ujumbe Kwa Watu Wanao Enda Kuwambia Wengine Habari Njema
Matende 13:4-52
Paulo na Barnaba walisafiri sehemu nyingi na kuwaaambia watu habari za Yesu. Kila wiki walikutana pamoja katika sehemu inayo itwa (Sinagogi) Paulo na Barnaba walikuwa wakiwapa watu ujumbe kutoka kwa Mungu. Kama hivi:- Paulo akasimama, akawapungia mkono, akasema, "nyi waume wa Israeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni. Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza. Mungu akawafanyi mambo makuu ya ajabu. Hatimaye Mungu akawapa Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote. Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi. Naye alikaa katika yetu. Lakini viongozi wa Wayahudi hawakumwamini Yesu kama ni mwana wa Mungu Yesu akufanya jambo lolote baya lakini watu walimsulubisha msalabani. Lakini Mungu akamfufua katika wafu. Sasa Wayunani na Waisraeli wanaweza kuokoka. Mkimwamini atawasamehe dhami zenu." Watu wote alishangaa kusikia habari hizo. Watu wengi wa Israeli waliamini Paulo alivyo sema. Na Wayunani wengi waliamua kufuata Yesu, Lakini baadhi ya Waisraeli walimkasilikia Paulo kwa ajili ya neno alilo litoa. Kwahiyo walikataa kumsikiliza Paulo, nao wakawafukuza Paulo na Barnaba. Basi Paulo na Barnaba waliwahubiria Wayunani sawa sawa na Waisraeli. Kwahivyo Wakristo wakaongezeka.
**MB**Rafiki yangu, kama watu wengine wanavyo pata matatizo wanapo waambia wengine habari za Yesu, sisi tuwaige watu hao hebu tuige mfano wa Paulo na Barnaba. Tusiche kufanya kazi ya Mungu uendelee kama Mungu alivyo tuita. Tutafurahi sana watu watakapo mwamini Yesu.
Picha Ya Kumi Na Saba:Mungu Alimlinda Paulo
Matendo 16:6-10
Baada ya Paulo na Barnaba kufukuzwa katika nchi ya Antiokia, waliona ni vema warudi katika kanisa lao la lililo watuma laikiwa lipokuwa njia Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi alipokwisha kuyaona yale maono, wakaona ni vema waenda Makedonia, kwa kuwa waliona hakika ya kwamba Mungu amewaita tuwahubiri Habari Njema. Kesho yake asubuhi Paulo na rafiki yake Sila wakajiangaa kwa ajili ya safari ya kwenda Makedonia.
**MB** Rafiki yangu, Roho wa Mungu akatulinda hata leo. Tunapo soma Neno la Mungu, Roho uongea nasi. Tunapo muomba Mungu, Roho anaongea nasi. Wakati mwingine anaweza kuongea nasi katika maono. Lakini ni lazima kwanza mionyo yetu iwe wazi mbele za Mungu kila wakati, na tuwe tayari kufanya kazi yake.
Picha Ya Kumi Na Nane:Paulo Na Sila Walipokuwa Katika Shida
Matendo 16:16-35
Paulo na Sila wakasafiri sehemu za Filipi, Makedonia, na kukauko kwa siku chache. Na huko waliaanza kuwafundisha watu habari za Yesu. Watu wengine walimini Neno la Mungu, lakini watu wengine walikuwa na hasira juu yao. Basi wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji, wakawachukua kwa madiwani, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi. Basi wakuu wa mji waka amuru wapigwe kwa vipoko. Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alichukua upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. Aka amuru taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila, kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Basi yule askari pamoja na familia yake wakamwamini Yesu. Na familia yao kiwa na furaha kwabwa.
**MB**Rafiki yangu, mambo yaha yanatokea hata siku hizi, Wakristo wana teseka na kufungwa bila ya kufanya kosa lolote. Lakini Tukumbu kwamba Roho wa Mungu yupo pamoja nasi kila wakati. Anaweza kutupa furaha katika mioyo yetu, na kutusaidia waambie wengine habari za Yesu, hata tukiwa katika wakati usio tufaa.
Picha Ya Kumi Na Tisa: Paulo Na “Mungu Asiye Julikana”
Matendo 17:16-34
Paulo akaenda sehemu inayo itwa Athene. Huko Athene aliiona miungu mingi ya sanamu. Na watu wa Athene wakamuomba Paulo awe muongeaji katika mkutano, na watu wengi walikusanyika ili kumsikiliza Paulo. Na maneno haya ndiyo Paulo aliyo yasema " Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, "Kwa Mungu asiyejulikana. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono, wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. Mungu wetu ni Mungu aliye hai. Watu wakanyamaza kimya wakimsikiliza. Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena katika habari hiyo. Basi hivi Paulo akaondoka akawaacha. Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamwamini Yesu.
**MB** Rafiki yangu, Ni Roho wa Mungu tu ndiye aliye msaidia Paluo kusema maneno ya Mungu. Watu hawa ilikuwa ni mala yao ya kwanza kusikia habari za Yesu, lakini sasa walikua kwamba Mungu anawapenda. Na walijua kwamba Yesu alikufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi za watu wote. Wengi wao waliamua kumpenda Yesu na kumfuta. Kupitia Yesu Kristo tunaweza kumjua Mungu wa kweli.
Picha Ya Ishirini:Mapigano Huko Korintho
Matendo 18:1-17
Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho. Akamwona Muisraeli mmoja, jina lake Akila pamoja na Prisila mkewe. Na kazi yao ilikuwa kufuma mahema. Bwana akaongea na Paulo katika maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu. Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu. Hata Galio alipokuwa liwali wa Akaya, Wayahudi walimkamata Paulo kwa nia moja, wakampeleka mbele ya kiti cha hukumu, wakisema Mtu huyu huwavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria. Wakaleta lawama nyingi mble ya Galio. Lakini Galio hakuya sikiliza maneno yao, bali Akawafukuza waondoke mbele ya kiti cha hukumu. Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi akilihubini Neno la Mungu.
**MB**Rafiki yangu, sisi pia tunaweza kupatwa na majaribu na shida kama alizo pata Paulo. Ingawa tunaishi maisha ya Kikristo na yakumpendeza Mungu, na kuwaambia watu wengine habari za Yesu. Mungu anatuambia "Usiogope, bali nena, wala usinyamaze" Mungu anatuambia tusiache kazi yake. Tukumbuke kwamba Yeye yupo pamoja nasi.
Picha Ya Ishirini Na Moja:Paulo Alikuwa Ladhi Kuteseka
Matendo 21:17 - 22:24
Paulo alisafiri sehemu nyingi akiyatembelea makanisa na kuhubiri habari njema za Yesu. Kisha Paulo alihisi kama Mungu anataka yeye aende Yerusalemu. Lakini watu wengi walimwambia asiende, kwani kuna watu wengi huko ambao wanakata kumuua Paulo. Laini Paulo. Lakini Paulo alisema mimi niko tayari kuwa kwa ajili ya Kisto hikiwa hayo ni mapendi yake. Basi Paulo akaenda mpaka Yerusalemu na akaka huo, baada ya siku chache Wayahudi waliotoka Asia wakamwona Paulo ndani ya hekalu, wakawafukuza watu wote, kisha wakamkamata Paulo. Mji wote ukawa na gasia, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paulo, wakamkokota, wakamtoa hekaluni, mara milango ikafungwa. Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, habari zikamfikilia jemadari wa kikosi ya kwamba Yerusalemu imechafuka, mji mzima. Mara akatwaa askari akawaendea mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo. Askari wakampelaka Paulo hadi gerezani ilifafanye uchunguzi. Na walipo kuwa wakienda Paulo alimuuliza yule askari, ninaweza kusema na watu hawa? Basi, alipompa ruhusa, Paulo akasimama akawapungia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania, Na waliposikia kiongoea kwa lunga yao waka nyamaza kimya, wakamsikiliza. Baada ya hapo wakampeleka Paulo gerezani.
**MB**Rafiki yangu, Watu wengi sana walitaka kumkamata Paulo, lakini Paulo hakulalamika. Paulo alijua kwamba Mungu anampango na maisha yake. Pia alijua kuwezo wa Mungu na jinsi anavyo weza kumlinda. Je, unakuwa na furaha watu wanapo taka kukudhuru kwasababu ya kumfuata Yesu? Uwe na furaha tu maana makao yetu ni mbinguni.
Picha Ya Ishirini Na Mbili:Ujumbe Kwa Mfalme
Matendo 25,56
Askari walimfunga Paulo katika geraza, Paulo alikaa gerezani kwa muda wa miaka miwili. Lakini Wayahudi bado walitaka kumuua, lakini Yesu akamtoketa Paulo na kumwambia, Usiogope, kuwatangazia Warumi habari zangu. Kisha Paulo akapelekwa mbele ya mfalme Agripa ili kushitakiwa. Paulo alipofika mbele ya mfalme akanyosha mkono wake, akajitetea, akisema ninasimama hapa nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi baba zetu waliyopewa na Mungu. Kwa maana Wayahudi wote wanajua maisha yangu tangu ujana, najisi nilivyo liudhi kanisa la Mungu. Na Yesu akanitokea nilipokuwa naenda Demeksi, akaniagiza niende kwa Wayunani na Waisraeli nikaambia habari njema za Yesu, ili watu waziache njia zao na wamgeukie Mungu. Ndugu zangu ninahukumiwa kwa kutii maagizo ya Mungu, ambayo kabila zetu kumi na mbili wanatarajia kuifikia, wakimwabudu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, Ee Mfalme. Paulo alitoa ujumbe huu kwa watu wote. Na Paulo alipo maliza kujitetea Mfalme na mawazili wake wakasemezana, wakisema, Mtu huyu hutenda neno linalostahili kifo wala kufungwa. Mfalme alijua kwamba Paulo hakufanya jambo lolote baya. Lakini Paulo alitakiwa kwenda Rumi ili kuonana na Mfamle. Naye Paulo akasafiri kwenda Rumi.
**MB**Rafiki yangu, Mfalme na watu wake walimsikilia Paulo kwa makini sana. Mungu alikuwa pamoja na Paulo. Mungu hakumuacha Paulo hata dakika moja, bali akikuwa pamoja naye katika kila neno lilosema mbele ya mfalme. Mungu anaweza kututumia sisi kama livyo mtumia Paulo. Lakini yatupasa tuwe tayari. Mungu anaweza kutuma maneno ya kuonge mbele ya watu wakuu.
Picha Ya Ishirini Na Tatu:Mungu Alikuwa Pamoja Na Paulo Katika Hatari
Matendo 27:1-44
Basi Festo, ambaye alikuwa mtu mkuu katika utawala wa Kaisari, akawaamuru askari wa kirumi wamchukue Paulo na kumpeleka Rumi. Safari ya kwenda Rumi ilikuwa ni safari ndefu sana. Iliwalazimu kusafili kwa mashua na kuvuka bahari. Na kwa msimu huo wa mwaka haikuwa vizuri kusafiri baharini. Kwasababu ya hali ya hewa na mawimbi mengi baharini. Na walipokuwa wakisafiri kulitokea dholuba kari. Hivyo iliwalazimu kupiga makasia kwa kasi ili chombo kisizame. Watu wote waliokua katika chombo waliongopa sana kwani walijua kwamba watapoteza maisha yao. Lakini Malaika wa Bwana akamtokea Paulo na kumwambia, "Usiogope. Imekupasa kusimama mbele ya mkuu wa Warumi. Mungu atakuokoa wewe pamoja na watu wote waliomo katika chombo hiki. Na siku ya pili asubuhi walijalibu kutia nanga katika kisiwa, lakini upepo ulikuwa ukivuma kwa kasi, wakaamua kung'oa nanga na kuendelea na safari. Wote walifurahi sana walipofika wakiwa salama.
**MB** Rafiki yangu, wakati huu ulikuwa wakati mgumu sana kwa Paulo na wote waliosafiri. Lakini walijua kwamba Mungu alikuwa pamoja nao, Naye ndiye aliye wasaidia. Sisi pia tunaweza kupatwa na shida kama alizo pata Paulo. Lakini tukumbuke kwamba Mungu yupo pamoja nasi, Naye atatusaidia. Pia tunaweza kuwasaidia wengine walio na hofu.
Picha Ya Ishirini Na Nne:Paulo Alipokuwa Rumi
Matendo 28:16-31
Paulo alikaa Rumi kwa miaka miwili. Walipofika Rumi Paulo alipewa ruhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda. Paulo alikuwa na hamu ya kuyatembelea makanisa ya huko Rumi lakini alishindwa, kwani alikuwa katika hulinzi wa askari. Na watu wengi waliposikia kwamba Paulo yupo rumi walikwenda kumsalimu. Paulo alipokuwa Rumi alianza kuandika barua kwa makanisa. Na barua hizo zilieleza habari za Yesu na jinsi makanisa yanavyo paswa kuenenda. Na barua hizo zipo katika Biblia, na zinaendelea kuwafundisha Wakristo wa sasa ulimwenguni mwote. Ulikuwa wakati mgumu kwa Paulo. Lakini Mungu alimsaidia. Kwasababu hiyo Paulo aliweza kuwasaidia watu wengine katika barua zake.
**MB**Rafiki yangu, Na haya ndiyo baadhi ya maneno ambayo Paulo aliyaandika katika barua zake:- "Mungu yu upande wetu na anafanya kazi na sisi. Kwahivyo mtu yoyote anaye sindana nasi hawezi kushinda. Mungu ametupa mwanawe wa pekee Yesu Kristo. Yesu alifufu katika wafu iliatupatanishe sisi na Mungu. Tuna weza kushinda mambo yote kwamaana Yesu anakaa ndani yetu. Na hakuna kitu kinacho weza kututenga na upendo wa Mungu" Haya ni mambo mazuri kwetu ambayo yatupa tutafakari. Je, Yesu anakaandani yako? Je, unanguvu za kumsinda Shetani? Je, unanguvu za kushinda dhambi, na maisha yako yanambendeza Mungu?